Kipindi cha miezi 6 wawekezaji wamevunja rekodi ya kuja wengi nchini

Unaiamini hii Serikali iliyojaa waongo wanaodai nchini kuna Vibrant democracy na good record on human rights? Wawekezaji na Covid-19 hii?
🤣😳😳😳

 
Pesa ipi? Ulikuwa uchumi feki!
Uchumi feki ndio tunataka sasa,uchumi original ndio ule mlikuwa mnapora wafanyabiashara? Mwambie dabu na genge lenu anyanyue Domo aone moto..

Kwani uchumi feki kama unanipa pesa wewe unateseka na nini? Uchumi feki ndio huo Sasa unamuwezesha mama kujenga vyumba 15,000 vya madarasa ,,vituo vya afya 250 na milioni 500 kila Jimbo huku akidabo bajeti ya Tarura na miradi mliyoshindwa kukamilisha miaka 6 itaisha ,kenge nyie mna nini cha kutuambia?
 
Ni jambo jema sana kupata wawekezaji wenye nia ya kuja kuweka mitaji yao ili kuwekeza na kupata faida na sisi kama nchi tupanue tax base.


Ila ijulikane, kupata certificate ya uwekezaji na kuleta fedha za kuja kuwekeza ni mambo mawili tofauti. JPM amewahi kutembelewa na Germany investor back in 2016/17 na baadae mambo yakanoga mpaka akahakikishia na Chancellor Angeka Merkel kuhusu uwekezaji huo, ila mpaka ameaga dunia hamna hata jiwe la msingi la hao wawekezaji.


Naipogenza TIC, naipongeza awamu ya 6 ila yasije yakawa yale ya kuwa biashara nyingi zimesajiliwa BRELA na watu kuandikisha nia ya kuwekeza TIC yet baada ya muda tunafanya tathmini na kugundua tumepiga hatua kiasi kidogo sana au kuna majamaa yanaweka mambo sawa, wanavuta fedha zinaingia kwenye local banking systems baadae zinakwenda kwingineko; sometimes hayatokeaga haya na huwa ni sehemu ya biashara bila kuvunja sheria.
 
Kwa kweli hata hamueleweki mnatakaje hasa.
Wawekezaji wasipokuja mnalaumu sera, wakija wawekezaji mnadai wanyonyaji.
Mwatakaje haswa!!!
Hata mie sifahamu wabongo wanataka nini. Wawekezaji usipowekea mazingira mazuri wanakimbilia kwengine. Kumbukeni muekezaji ana fedha mkononi au mtaji, ana channels nyingi za kwenda.

Suala la mikataba nadhani hii mikataba ni public records, mtu kama anao ushahidi wa mkataba mbovu basi aeke tuu kwenye mitandao au awape wabunge watuekee wapi tuone. Lakini wawezekaji ni muhimu katika kukuza uchumi.
 
Biashara nyingi zikisajiliwa na watu kufanyaa biashara wewe unateseka nini? Sekta binafsi itakuwa imetatua tatizo la ajira Sio kila ajira lazima TRA wachukue pesa..

Turudi Uchumi wa JK ndio uchumi wa kumpa purchasing power mtu na kumtoa kwenye kuishi kama mashetani ..

Kwani hukumbuki kipindi Cha JK watu walikuwa wanaacha Kazi ya serikali na kujiajiri? Spirit ya kujiajiri ilianza kujengeka,sasa tuulizane nani alipenda kujiajiri awamu ya Dhalimu Mwendazake?
 
Achana na kuwajibu wapumbavu na misukule ya mwendazake,usituhusishe wote unaposema wabongo.
 
Mkuu sina hisia yoyote ya kuteseka na mafanikio yanayochochea mtiririko wa fedha mtaani kupitia shughuli za kibiashara halali.

Kutoa tahadhari sio kukosoa/kuwa na nongwa; ila kama tutafikia kwenye mambo ya kughushifi kama boss mmoja wa TRA zamani na kupiga cha juu kama ndio Tanzania tunayoitaka, hakuna atakaezuia.
Cha msingi tu kusiwa na kampuni kama Kagoda and the like, zinasajiliwa hapa, wanakwapua BoT then vijinsenti vinabaki hapa, lion share inaondoka
 
Hii ya madarasa ni unyang'anyi kupitia kitu kinaitwa tozo,halafu nia na matokeo ni vitu viwili tofauti,sema mna nia ya kujenga vyumba 15k vya madarasa
 
Labda wawekezaji wa kuuza alkasusu na urojo
 
Hata kipindi cha mwendazake mlimwambia anavunja rekodi kila siku [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…