Nadhani hapa swali ni kwanini miezi inatofautiana idadi ya siku.
Anyway mimi najua kwanini February nyingine zina siku 28 ilhali nyingine zina siku 29.
Jambo hili limefanyika makusudi kwenye design ya Gregorian calendar kwasababu dunia inatumia siku 365¼ kulizunguka jua. Lakini wasingeweza wakaweka robo siku kwenye design ya calendar lakini pia wange round-off iwe siku 365 au 366 kamili kila mwaka basi hiyo tofauti ya robo siku ingekuja kusababisha misimu (kiangazi, masika, autumn na spring) ipishane miezi. Yani, lets say mwaka huu masika inaanza December, ila baada ya miaka 200 ile tofauti ya robo siku inakua imeusogeza mbele/nyuma msimu huo kwa siku 50 kwahiyo 200 years later masika inakuwa inaanza say March au September (misimu haitegemi tarehe, binadamu ndio tume engineer tarehe ziendane na misimu) Hii inconsistency ingeleta shida sana kwa civilization ndio maana kila baada ya miaka minne wakaongeza siku moja nzima kwenye calendar (February 29) ili kunyoosha mambo.