JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Ndugu zangu kauli hz zimezoeleka sana tunapokuwa tunaelekea kwenye uchaguzi na tukiwa kwenye uchaguzi vilevile,je Hv ni kweli mtu anaweza kula pesa ya mtu na asimpe kura?,na je aliyetoa pesa hizo anajua kweli kwamba waliokula fedha zake hawakumchagua, je anaweza kuamini rahisi kiasi hicho.
Mimi nadhani wakati umefika Watanzania tubadilike tukatae rushwa kwa kumaanisha tuwaachie wagombea fedha zao na tuzikatae kwa kumaanisha ALAFU twende sasa tukachague Viongozi safi wasio kula wala kugawa rushwa,tukifika hapo tutadai haki yetu hata tukiibiwa kura na kunyang'anywa ushindi kwenye chaguzi na MUNGU atatembea na sisi.
Lakini tukiruhusu rushwa na tukashiriki kuila MUNGU atakaa mbali na sisi na tutaendelea kupata viongozi punguani kila baada ya miaka mitano. Ili tudai ushindi kwa nguvu zote na sikuzote lazima tuwakatae watoa rushwa ya uongozi na fedha zao ili tupate kile ambacho sisi watanzania tunadhani kinatufaa.
Soma Pia:
Ukila fedha za watu nguvu yako inapungua katika kudai haki yako ya msingi kwa sababu mifuko yako ina fedha za watu nafsi itakusuta.Watanzania wanaonekana wamechoshwa na uongozi wa hovyo,Sasa KATAA RUSHWA CHAGUA KIONGOZI BORA na sio bora Kiongozi.