Kipindi Cha "Wana wa town" kinaleta ujumbe gani kwenye jamii?

Sister Abigail

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
2,886
Reaction score
9,088
Kazi ya sanaa ni kufikisha ujumbe, kuburudisha, kuonya na kadhalika, lakini mi sielewi kuhusu hiki kipindi kipya kilichoanza juzi kuonyeshwa kwenye channel pendwa ya Maisha Magic Bongo DStv.

Kilipigiwa promo ya kutosha hatimaye siku ikafika. Nliyoyaona na niliokua nimekaa nao wakabaki wanauliza, "Nini hiki?"

County Wizzy, Calisah na Whozu. Kuna ulazima wa kuonyesha mkiwa uchi wa mnyama bafuni naoga?

Kwanini msifanye cameraman anaishia kuonyesha unaingia bafuni kisha anaonyesha unatoka umevaa taulo, kitapungua nini?

Kuna ulazima wa kushoot mwanume unakojoa toi?
Kuna ulazima wa kutembea na vichupi na vipedo?
Kuna ulazima wa kuonyeshwa ufuska wenu mnakulana mate na kushikana matako na malaya zenu huko club?
Mpo Tanzania sio Marekani.

Najua mmelenga kuonyesha real life kama macelebrity but please ficheni uchafu wenu mnaharibu matineja na hata watoto bahati mbaya wanaangalia!

Huyu Calisa ndio kabisa mfano mbovu wa mwanaume! Yaani mtoto wa kiume akimwangalia huyu hesabu hasara.

Ni hayo tu.
I come in peace. ✌️
 
Kwa upande wangu binafsi nashukuru kwa taarifa mkuu, inabidi nikalifanyie kazi hili suala maana ni muhimu kuwalinda watoto na huu uvunjifu wa maadili.
 
Na hili nalo nendeni mkalitizame..
 
Inategemea inaonyeshwa muda gani, na umri wa kuangalia umeainishwa ni upi? Pia kuna chanel nyingi sana zaidi ya 300, zipo za dini, mapambio n.k , na inawezekana kuna chanel nyingi huwa hatuziangalii; kwa mazingira hayo, kama chanel fulani kuna mambo yanakukera, unaamia chanel nyingine.
Kwa sababu wanachokionyesha hakuna cha ajabu ambacho dunia haijui.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…