Kipindi gani kilichokuvutia redio Tanzania miaka hiyo?

Kipindi gani kilichokuvutia redio Tanzania miaka hiyo?

Kile kipindi cha salamu kwa wagonjwa ilikua ni baada ya habari ya saa kumi alasiri.
 
1.Uje tena shangazi shangazi shangazi eeh shangazi..uje tena shangazi

2.Wosia wa baba wa taifa

3.majutooo ni mjukuu

4 michezo akitangaza enock mwigane
 
Kipindi nilichokuwa nakipenda ni safiri na PB kilikuwa kinaongozwa na Uncle J kama sikosei na na kingine kilikuwa Out and about RTD English service
 
Kile kipindi cha salamu kwa wagonjwa ilikua ni baada ya habari ya saa kumi alasiri.
Kama unazungumzia kipindi cha UGUA POLE, rtd, kilikuwa ni saa tatu asubuhi hadi saa nne siku ya j,2.

Walikuwa wana utaratibu wa kutembelea wagonjwa hospitali flani na kuongea nao. Kilikuwa ni kipindi kizuri sana kwani kilikuwa kikiwapatia wagonjwa faraja flani, na pia walikuwa wakipewa nafasi ya kutuma salamu kwa wapendwa wao na kuchagua muziki.

OLD IS GOLD aiseee!


YESU NI BWANA.
 
Back
Top Bottom