Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Karibu kila Mwananchi anajionea hali jinsi ilivo mtaani, ngano bei juu, mafuta ya kupikia,mchele,nk. kulinganisha na hali ya pesa mtaani ilivo mbaya wengi wanashindwa kununua mahitaji ya msingi nyumbani
Watu wamekuwa wakilalamika kwenye mitandao bila kujua wafanyeje maana kilio Chao kimekuwa kikiishia hewani tu, kulia sana mitandaoni haitaondoa hali halisi iliyopo hivyo ni bora kufunga mkanda haswa.
Ulevi, kulingana na hali ilivyo mitaani watu wazima na vijana wameamua kunywa pombe za bei rahisi kuanzia 500 alewe ilimradi kujitibu na stress,. Maana wengi wao hawaijui kesho yao.
Uraibu wa mtandaoni, vijana wengi kutokana na Kukosa ajira. Kayumba kibiashara,pesa kidogo wanayoomba kwa wazazi, ndugu huitumia kwa vocha kushinda mitandaoni ilimradi tu kujipa furaha maana furaha ya kweli mitaani na kwenye familia hakuna.
Viwanda vidogo kwa vikubwa vimekuwa vikijitahidi kutengeneza pombe kali tena za bei rahisi na hii ni Kutokana na uhitaji wa soko lenyewe na pombe hizi mwisho zinaleta athari kwa watumiaji.
Vijana ambao ni nguvu kazi kwa Taifa wamekuwa wakifanya juu chini kwenda Ng'ambo wakiamini ni bora zaidi kuondoka nchini kuliko kuendelea kuumia nchini kwao.
Viongozi wetu kwa sasa hawana msaada wa moja kwa moja kwa wananchi na hii imesababisha kuwa na mstari mkubwa kati ya viongozi na wananchi, kwani wananchi wamekuwa wakipapambana wenyewe kiuchumi, kiafya hadi kilimo.
Hali ni Ngumu kweli wote yatupasa kufunga mkanda huku tukiamini kuwa baada ya muda uchumi unaweza kukaa sawa hivyo tuwe wavumilivu