Kipindi kigumu ligi kuu Uingereza (EPL)

Kipindi kigumu ligi kuu Uingereza (EPL)

Dkileo

Member
Joined
May 23, 2017
Posts
51
Reaction score
46
Mara nyingi katika hiki kipindi mechi huwa zinachezwa nyingi kwa siku chache..Pia hali ya hewa huwa inakuwa ya baridi sana..wachezaji huwa wanapata majeraha mno..Wanatumia energy nyingi sana kipindi hiki..Ndio hapa utaona umuhimu wa kuwa na kikosi kipana na rotation ya wachezaji..Kuna baadhi walibishana na mimi sana..Waliamini kuwa naipondea timu fulani..Lakini hii hutokea kwa timu yeyote

Jana Man united wamepata injury ya Lukaku..Leo Man city wamepata injuries mbili..De Bruyne na Gabriel Jesus..Hiki huwa ni kipindi kigumu sana Epl..Huwa inakuwaga ngumu kumaliza kipindi hiki bila injury…Wenger analifahamu hili vizuri..Ni kipindi hiki ambacho timu zinatumia nguvu nyingi sana..

Tunaelekea katika dirisha dogo la usajili..Wenzetu Liverpool wameanza na Virgil Van Djik..Tungojee tuone timu zetu zitafanya usajili gani..

Kumbuka kuwa mwezi June kutakuwa na World cup Russia hivyo tutegemee sajili nyingi zitatokea kwa kuwa kila mchezaji anatafuta namba katika timu yake ya taifa 2018 Russia

Follow me @dickykileo on instagram
 
Well well ....kipindii hiki kinatesa sana timu
 
Back
Top Bottom