Kipindi Simba wanaanza kujipanga kwa ajili ya Msimu huu wa Ligi, sisi Yanga...

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Tulikuwa busy sana na kuandaa namna ya kuwabeba akina kisinda, Sarpong, Hersi, Mukoko n.k hii ilinipa shida kiasi kikubwa sana kwa ile imani kuwa tumesajili team kabambe na hakuna team ambayo itatuzuia. Huu wazimu nikikumbuka huwa naumia sana maana nilikuwa mmoja ya watu ambao walipinga sana jambo hili.

Nikaonekana mimi ni mamluki nk. niliwauliza wenzangu kama sisi wenye akili tukichambua mnatuzogoa na kusema kuwa ni mashabiki au mamluki wa Simba je, hii maana yake ni kuwa wenye akili ni Simba tu?

Utamaduni wa kuwabeba wachezaji na viongozi uliasisiwa msimu huu kwa makusudi maalum. Sisi wenye akili tulifahamu kilichokuwa kinaendelea. ni suala la siasa chafu za mpira. Niliwahi waambia GSM maneno flani kuwa wawe serious na uwekezaji wao. kiukweli tunataka wawekezaji ambao wana nia ya dhati ya maendeleo ila si wajanja wanjanja na wenye kutufanya sisi hatuna akili.

Simba walipoteza matches mbili kipindi ambacho sisi tulikuwa hatujapoteza match hata moja. Waliendelea kujenga utulivu. kwa team kama ya Simba ilikuwa rahisi kuamini kuwa haitotokea kupoteza match hata moja.

Walipoteza wakakaa na kuangalia tatizo nini wakajirekebisha. Hukusikia wakilalamikia waamuzi kwenye press au TFF ingawa kuna match kama ile ya T Prisons kiukweli kuna uhuni mwingi ulifanyika. Waliendelea na ligi wakijua kila kitu kinaweza kutokea.

Sisi tulipomleta Kaze ilikuwa issue Duniani nzima ikajua tumemleta Kaze. tukampa mzigo mkubwa sana kisaikolojia tulimwathiri. lakini pia GSM imetengeneza matabaka kwa wachezaji. Kwa sasa kuna wachezaji wa GSM na wachezaji wa Yanga ya Msolla.

Haya yamekuwa matatizo. Kuna wachezaji wanacheza Yanga lakini hawana furaha ya kuwa Yanga. wengi tu nafahamu kuna baadhi ya wachezaji wanatamani sana kwenda SIMBA na wanacheza kwa nia kubwa ya kwenda Simba. wapo. kuna wachezaji hawana mikataba ya ukweli. Hawa wapo Yanga kwa ajili ya kutafuta soko la Kisoka. wachezaji wengi wa nje hamna kitu kinachoeleweka pale Yanga.

Yanga tunapaswa kutulia na kujipanga kuangalia ni wapi tulianguka. ingawa pia kuna maneno mengi sana kuhusiana na Senzo. Yapo nachelea kutoyasema haya sababu sitaki kuleta taharuki. Ila ni kipindi cha kuangalia sana wahujumu wa Yanga wamo ndani ya Yanga kwa Maslahi binafsi na kwa maslahi ya makundi yao. Tujipange team icheze bila pressure matokeo yatakuwepo tu. Lakini kuiweka team katika pressure ni kuukosea sana mpira wa Miguu tunashindwa elewa mpira wa miguu una nidhamu yake.
 
Duh so details report which has been analysed

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo waliamnshwa Sana kwamba msimh huu kombe lao so wanapopata matokeo mabaya wanaanza kulaumiana Cha msng yanga waangalie Sana
--uongozi; je unawajibika ipasavyo
--Benchi la ufundi; Litakalokuja ltakidhi matarajio Yao
--Aina ya wachezaji; je wanafanania na matarajio ya kubeba ubngwa
 
Your browser is not able to display this video.
 
Umenena vyema ila watopolo watakuita majina yote mabaya,hawataki kuambiwa ukweli wao wanataka kuambiwa kile wanataka kusikia kama zile porojo za kidoti.
 
sishangai kuona dirisha kubwa la usajili mkivunja kikosi chote cha wachezaji na kusajili kingine, alafu uwadanganye tena mashabiki kuwa mnachukua ubingwa.
kikosi bora hakijengwi kwa msimu mmoja, kinahitaji muda sanaaa
Hawa mpaka utumie hii ID yako ndio watakuelewa.

Ebu Watombise kwanza
 
Mleta mada hebu wacha ulevi wa mchana, hii inayoshindwa kuifunga Prison ikiwa pungufu ndio ilijipanga na ligi? Hii timu ni overrated, pale ni kikundi cha wapigaji tu.
 
Mzee akili zote hizi unakuwaje utopolo...tunakaribisha mashabiki wanaojielewa dirisha dogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…