Kipo tunachokihitaji sasa zaidi ya ripoti za Ukaguzi

Kipo tunachokihitaji sasa zaidi ya ripoti za Ukaguzi

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
TUNAHITAJI NINI SASA KULINGANA NA RIPOTI YA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI.

Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali imekuwa ikijitahidi sana kufuatilia matumizi bora ya raslimali za Umma na kutoa taarifa zinazoonesha namna gani raslimali hizo hutumika kwa maslahi mapana ya Taifa hili.

Takwimu za hasara zinazosomwa kila mwaka kwa kweli zinaumiza masikio na akili za Watanzania wengi. Tumekuwa tukisikia mabilioni ya hasara mara kadhaa sasa. Hali hii imenisukuma kuandika kuwa "KIPO TUNACHOHITAJI ZAIDI YA UKAGUZI".

Naipongeza ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa kazi nzuri na ngumu wanayoifanya ila napenda kuweka wazi kuwa Watanzania sasa tunahitaji zaidi ya UKAGUZI wa hesabu za Serikali.

Kwa dhati kabisa Watanzania tunachokihitaji kwa wakati huu ni UTHIBITI MAKINI. UKAGUZI aghalabu umekuwa ukionesha picha inayosukuma kubaini ni nini kifanyike na sasa kinachoonekana pasi na shaka ni udhaifu katika uthibiti.

Tunahitaji kuona nia ya dhati kwenye uthibiti katika kumbo hili la wakati kuliko wakati wowote ule ili kuepuka kufa kwa miradi mingi mikubwa iliyoanzishwa na kuhaishwa na Serikali.

Viongozi wenye dhamana ni vyema nguvu kubwa zikaelekezwa kwenye kuthibiti ubadhirifu kuliko kukagua ili kubaini ubadhirifu. Nieleweke kuwa ninaafiki suala zima la ukaguzi wa hesabu za Serikali ila ninachosisitiza ni hitaji kubwa la uthibiti katika wakati huu. "TUKAGUE KWA NGUVU KUBWA NA TUTHIBITI KWA NGUVU KUBWA".
 
Back
Top Bottom