Kiredio na Vee Dollar: Hivi Mapenzi Hufia Kwenye Mafanikio au Umasikini Ndio Unaounganisha Watu?

Kiredio na Vee Dollar: Hivi Mapenzi Hufia Kwenye Mafanikio au Umasikini Ndio Unaounganisha Watu?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Mtengenezaji wa maudhui maarufu mtandaoni, Kiredio, ameingia kwenye trending kufuatia madai ya kuachana na mpenzi wake, Vee Dollar.

Baada ya taarifa hizo kuibuka, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wameanza kusambaza video zao za zamani, zilizorekodiwa kipindi ambacho Kiredio na Vee Dollar walikuwa bado kwenye hatua za kujitafuta na kujenga maisha yao kupitia utengenezaji wa maudhui.

Video hizo zimeibua hisia na mijadala mbalimbali, kutokana na namna wawili hao wanavyoonekana wakishirikiana kutengeneza maudhui kipindi ambacho hawakuwa na umaarufu mkubwa kama walivyo sasa.

Soma pia: Mdau wa JF: Kiredio na Demu wake wameachana

Kwa miaka iliyopita, Kiredio na Vee Dollar wameonekana wakipiga hatua kubwa katika maisha yao, huku kila mmoja akifanikiwa kujenga jina, kupata umaarufu na idadi kubwa ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.

Kinachowafanya watu wengi kujiuliza zaidi ni madai ya kuachana kwao wakati ambapo tayari wamefikia mafanikio makubwa, tofauti na kipindi ambacho walikuwa wakianza safari yao na kujitafuta pamoja.

Hali hiyo imeibua swali miongoni mwa mashabiki: imekuwaje wamefikia hatua ya kuachana baada ya kupitia safari ndefu pamoja, kutoka kipindi cha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa?

Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Kiredio au Vee Dollar zinazothibitisha sababu ya madai hayo ya kuachana, hivyo mjadala huo unaendelea kushika kasi mitandaoni.


Source: flux media

​
 
Waache utoto WATULIE hata mi napenda couple Yao, lakini wasilazimishwe kua pamoja mkipendana kweli havinaga mambo ya kusuluhishwa mnamalizana wenyewe
 
Kuna demu WANGU nilisha wahi leta picha yake humu mkuu, mazingira tulio Anza nae mahusiano yetu basi tu, tylivumiliana lakini haimanishi ndo hatuachani muda ukifika riziki Huwa zzinaisha kila mtu anashika yake unavuta chuma kipya Mzee life continues
 
Mambo yao waachie wenyewe.

Yale Yale ya Diamond kuachana na Zuchu.

Halafu ghafla mnashtukizwa na Baby shower. Mliodhani wameachana wanakaribisha mtoto wao kwa sherehe kubwa.
 
Shida ni moja huyo demu watu wamejua kwa shepu lake matata wanamjaza kwamba kuwa kiredio sio level yake lakini kiredio ndio kamfanya afahamike na hata Hilo shape lake halikuwa hivyo kipindi hajulikani
 
Shida ni moja huyo demu watu wamejua kwa shepu lake matata wanamjaza kwamba kuwa kiredio sio level yake lakini kiredio ndio kamfanya afahamike na hata Hilo shape lake halikuwa hivyo kipindi hajulikani
Mbona huyo demu ni wa kawaida sanaaaa
 
Back
Top Bottom