Kirefu cha MAU MAU

Kirefu cha MAU MAU

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Tangu ujana wangu na kusoma kwangu,sijawahi kujua kirefu cha maneno maarufu Barani Afrika : MAU MAU. MAU MAU lilikuwa jina la vuguvugu za kupigania na kudai Uhuru nchini Kenya katika miaka ya 1950. Vuguvugu hili lilikuwa likiongozwa na Dedan Kimathi,Jomo Kenyatta na wengineo. Ni vuguvugu hili lililosaidia Kenya kupata Uhuru mnamo mwaka 1963.Kirefu cha MAU MAU ni : Mzungu Arudi Ulaya,Mkenya Apate Uhuru.Nimefurahi sana leo. Mwenzangu vipi? Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mbona mau mau wote walikuwa wakikuyu? Au ndio maana idadi kubwa wa marais kutawala kenya wanatoka kabila hilo-jomo kenyatta, mwai kibaki, uhuru kenyatta.
 
harakati za kimungiki wakikuyu wameanza zamani eehhh......
 
Tangu ujana wangu na kusoma kwangu,sijawahi kujua kirefu cha maneno maarufu Barani Afrika : MAU MAU. MAU MAU lilikuwa jina la vuguvugu za kupigania na kudai Uhuru nchini Kenya katika miaka ya 1950. Vuguvugu hili lilikuwa likiongozwa na Dedan Kimathi,Jomo Kenyatta na wengineo. Ni vuguvugu hili lililosaidia Kenya kupata Uhuru mnamo mwaka 1963.Kirefu cha MAU MAU ni : Mzungu Arudi Ulaya,Mkenya Apate Uhuru.Nimefurahi sana leo. Mwenzangu vipi? Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Sasa na wewe unajiitaje Mzee wakati sisi wengine hili swala tumelifahamu tangia miaka ya sitini? Yaani unataka sie tujiitaje sasa?
 
Enzi zetu tulijua hivi! Mwingereza Arudi Ulaya Mwafrika Apate Uhuru. Ukichukulia kuwa hata Tanganyika nao tulikuwa na waingereza. Kwa hiyo vuguvugu la kumtaka mwingereza lilikuwa ni jambo la Africa mashariki kuhanikiza warudi kwao. kwa hiyo ilikuwa siyo Mkenya apate uhuru bali Mwafrika Apate uhuru!
 
Back
Top Bottom