Kisa ambacho mpaka leo huwa sielewi sababu yake

Kisa ambacho mpaka leo huwa sielewi sababu yake

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,497
Reaction score
16,180
Hili ni tukio la kweli kabisa.

Sehemu / Nyumba ninayoishi ni self contained vyumba viwili na public washroom/lavatory.

Sasa kuna siku mwaka jana nimekaa zangu nacheki TV nikabanwa na mkojo so mdogo mdogo nikasimama nielekee lavatory ku-empy my bladder.

Sasa ile nimekaribia mlango wa choo nikaona upo wazi nikajua huenda kuna mtu aliingia kujisaidia wakati wa kutoka akasahau kufunga, nikaona isiwe kesi nikapitiliza LAAHAULA nilichokuta sikuamini macho yangu na mpaka kesho sijajua why!

Ni kwamba nilimkuta jamaa / rafiki yangu ambae tulikua nae tunaceki tv ila alitoka nikajua kaenda kuongea na simu nje or some... nikamkuta amekaa anajisaidia kwenye choo cha kuchucumaa!🙄 (just imagine mtu kakaa kwenye choo cha kuchuchumaa) na sio kwamba jamaa alikua na matatizo hapana ni mzima wa afya, sio kwamba ni mshamba hapana.

Niliishia tuu kusema WE UNAACHAJE MLANGO WAZI? nikatoka, jamaa alipomaliza nae akapitiliza nje na mpaka leo sijamuona tena.
 
Kwahiyo una choo cha kuchuchumaa ndani ya self contained!
Sijawahi kusikia hii aisee! Hakitoi harufu ndani ya Nyumba?
 
bora wee mi nilimkuta bi kizee kakalia kinu kikubwa usiku anakata gogo..nilikimbia hatari
 
Kama ambavyo wadada huchuchuma kwenye choo cha kukaa..

Ngojeni siku kije kufumuka hamjui ni udongo ule..??
 
Kwahiyo una choo cha kuchuchumaa ndani ya self contained!
Sijawahi kusikia hii aisee! Hakitoi harufu ndani ya Nyumba?
Choo Cha kukaa ni changamoto ndugu siyo kila nyumba self lazima iwe nacho na harufu ya choo inategemea na muusika mwenyewe ule mfuniko sidhani kama unaweza kuzuia harufu kama muusika ni mchafu
 
Back
Top Bottom