Kisa cha Adam Mchomvu kumuumbua Fid Q kwenye Interview ni nini?

Kisa cha Adam Mchomvu kumuumbua Fid Q kwenye Interview ni nini?

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
Hi good people,

Leo wakati msanii Fareed Kubanda - Fid Q yuko ndani ya XXL ya Clouds fm anatambulisha ngoma yake mpya inaitwa Bongo Hip Hop, mtangazaji Adam Mchomvu amekuwa anambana na maswali sana kiasi cha Fid kumtolea uvivu kuwa "najua umeagizwa kuja kuni-harass kwenye interview yangu".

Adam alikuwa anambana sana na maswali ya kwanini amerudia ngoma hii kutoka Tongwe Records aliyomshirikisha Juma Mohamed Mchopanga (Jay Moe) na kuirudia Bongo Records akimshirikisha P.Funk Majani?

Adam anaonekana kumind hii kitu kiasi cha kulazimisha kuipiga ngoma ile version ya mwanzo ya Tongwe baada ya hii version ya Bongo Recz kumalizika (ingawa kibishi sana maana B12 alikuwa anataka kubana. Ila kabla ya ngoma kuisha B12 akaikata na Adam anasikika akimind na kusema kesho atashusha mzigo mwingine.

Kilichonipa maswali hapa ni Je Adam ni ile loyalty yake ya kuwa Record Label kule Tongwe Records ama ana ubia kule Tongwe ndiyo sababu ya kuishupalia hii kitu namna hii? Hebu mwenye idea na hii kitu atujuze wadau.
 
BONGO HIPHOP by FID Q ft P.FUNK

VERSE 1:

Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/
Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua/
Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko/
Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/
Sikusound garbage au kuchange suddenly../
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely/
Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni/
I started young.. I made my mother's womb a drum/
My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/
BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in between

Chorus:

Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2

VERSE 2:

Kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami/ na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani/
For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey/
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee/
Waufuate mkumbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari/ ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari/
Sio tu bongo.. mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari/ kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali/
Kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi/ unachosema ni.. kamwe IPP haitompinga Mengi/
Unawakumbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia/ na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia/
Mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati/ mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji/
Amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate/
Uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate

Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2

VERSE 3:

Mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu/
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu/
Inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na Hasheem/
Na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?/
Nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya/
Naspit fire bila hennessy.. au kula kaya/
I want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways NI HAYO TU/
Beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop/
MC anayetaka beef.. amlete maza ake kwa strip club/
BONGOFLAVA wananipima.. kama nimeiva kimasomo/ wanagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common/
Cha ajabu humitempt.. ili nikuache hiphop/ anaahidi atanipa good sex.. wewe unanipa true love/
Hajui ' who's next.. wewe unanipa tu mashavu/
Nikipaa.. anaumia.. anatamani nishuke chini/
Nami sikuutamani ustaa.. ustaa ulinitamani mimi/
Nilichohitaji.. nikuitumia hii sanaa.. nishee na nyinyi hii zawadi, niliyopewa na mpaji ninayemuamini/
MPAJI aliyenivika taji ilimradi incharge ni wini/ na ninaamini.. kuna muda huongea kwa kupitia mimi/
Na hunisamehe ninapokosea.. ni vyema mkanizoea nyinyi/
Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha/
Nikitoa ngoma wanaitaka wanaipata coz wewe ni special....

Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
 
P si aliwananga clouds na kuwachana kuwa wamemnyonya sana ngwea mpaka kafa masikini?..labda ndo sababu
 
Hao Ni MaBesteeeee...Wanapenda Kuchangamsha Baraza...
 
Yaani wale madogo wa XXL kila wanachoongea kuna watu wanachukulia serious kweli ........ Hivi vijana mnaosikiliza muziki siku hizi hamuwezi kuchuja na kunote vitu serious kidogo ....kama kuna vitu technical kwenye version ya Bongo Rec tofauti na Tongwe si ndio ingekuwa topic na akina sisi ambao hatujasikiliza tukaelewa ........
 
skilizeni rdio one ijumaa saa nne na robo mpaka saba kipindi hizi nazo au magic jumapili saa tatu mpaka tano kipindi wazee wetu ndio mtajua the rise and fall of tanzania music,
 
skilizeni rdio one ijumaa saa nne na robo mpaka saba kipindi hizi nazo au magic jumapili saa tatu mpaka tano kipindi wazee wetu ndio mtajua the rise and fall of tanzania music,

Sisi na engine bado tupo na mawingu...bado mtakondaaa
 
Hivi theme nzima ya XXL ni nini??? Nilikuwa nasikiaga watu wanjiropokea tu kama machizi ila sikuelewa, nikaacha kusikiliza
 
Mchomvu ameona ile nymbo y tongwe ndo kali ila perfect,stamina na b12 wameona nyimbo ile fid Q alyomshrikisha majan ndo kali! Ubishi ndo ulikuwa hivyo m naungana n wakna stamina nymbo na majan n kali naipa 100%
 
Back
Top Bottom