Kisa cha ajabu cha mabinti wawili waliopotea katika mazingira ya kutatanisha

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,468
Reaction score
32,167
Kris+Kremers+&+Lisanne+Froon+disappearance.png

Tarehe 1, mwezi wa 4 mwaka 20014, mabinti wawili Kris Kremers and Lisanne Froon waliondoka katika makazi ya mwenyeji wao kwa ajii ya kumpeleka mbwa matembezi kwenye msitu unaozunguka Mlima wa Volkano wa Baru unaopatikana katika mji wa Boquete, nchini Panama. Hii ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuonekana wakiwa hai.

Kremers and Froon walikuwa wanafunzi kutoka Amersfoort katika nchi ya Netherland. Walikuwa wameandaa safari ya kutembelea nchi ya Panama kwa miezi sita, kwa lengo la kujitolea katika kufundisha watoto. Pia walikuwa wamepanfa kutumia baadhi ya muda wao kutembelea sehemu za milimani na misitu na kujifunza lugha ya Kispaniola ambayo ndiyo lugha inayozungumza nchini Panama.

Kabla ya kupotea, walikuwa tayari wametumia muda mwingi wakizurula kwenye misitu ya Panama kwa kipindi cha wiki mbili. Pia walikuwa bado wana wiki nne za kuendelea kuwa Panama kabla ya kurudi kwao.

Lakini siku hiyo ya tarehe 1 mwezi wa 4, 2014 saa tano asubuhi, waliaga mwenyeji wao kuwa wanaenda matembezi na mbwa na hawakuwahi kuonekana tena.

Kurasa zao za Faceboo zinaonyesha kwamba walipost jumbe zinazoonyesha wkamba walikuwa na lengo la kutembelea kijijji cha karibu. Pia waliandika kwamba walikuwa na mazungumzo na vijana wawili kabla ya kuendelea na matembezi yao.

Usiku ulipoingia, mwenyeji wao aligundua kuwa kuna jambo ambalo halikuwa sawa. Mbwa alikuwa amerudi nyumbani lakini mabinti hao hawakuwa wamerudi. Mwenyeji wao pamoja watu wengine waliokuwa wakiishi hapo nyumbani waliwatafuta kwenye eneo la karibu na nyumbani lakini hawakuwaoni. Waliamua wasubiri mpaka asubuhi kama hawatorudi, basi wajulishe vyombo husika.

Tarehe 2, mwezi 4, 20014 yani siku moja baada ya kupotea kwao, Kremers na Foon walikuwa wana miadi ya kukutana na mtembeza watalii wa maeneo hayo (tour guide). Lakini hawakutokea. Huyu jamaa ilikuwa awapeleke katika matembezi kuzunguka mji wa Boquete. Hili jambo lilonyesha kuwa kuna haja ya kutaarifu vyombo vya usalama. Siku iliyofuata ulifanyika msako kwa kutumia ndege kuzunguka msitu huku watu wakiungana kufanya msakao nfani ya msitu pia.

Tarehe, 6 bado mabinti hawa walikuwa bado hawajapatikana. Wazazi wa mabinti hawa waliamua kusafiri kutoka Netherlands kwenda Panama huku wakiwa wamekuja na makachero wapelelezi pia. Kwa kushiriakina na askari wa Panama, mbwa, na wakazi wa pale waliwasaka hao mabinti katika msitu kwa siku kumi mfululizo.

Siku ziligeuka kuwa wiki, mpaka wili ya kumi hakukua dalili yoyote ya kuwapata hawa mabinti waliopotea.

Wakati Polisi wakiwa wamekata tamaa na shughuli za kuwatafuta zikiwa zimeanza kukoma, mwanamke mmoja mkazi wa maeneo hayo aliwaletea begi la mgongoni la rangi ya blue, akidai kuwa aliliookota katika jaruba la mpunga katika kingo za mto. Ndani ya begi hilo kulikuwa na pea mbili za miwani, pesa kiasi cha $83, Passport ya Frroon, chupa ya maji na sindiria mbili.
bras.jpg

Na jambo zuri zaidi, ndani ya begi hilo kulikuwa na kamera ndogo ya Froon pamoja na simu zote mbili za hao mabinti.

Mara moja, polisi walianza kuchunguza simu na kamera na walipigwa butwaa kwa kile walichogundua.

Simu zilionyesha zilikuwa zinatumika kwa kipindi cha siku 10 toka mabinti hao wapotee. Ndani ya siku nne, kulikuwa kuna majaribu zaidi ya 77 ya kupiga simu polisi kwa namba ya dharula. Inaonyesha majaribio ya kupiga 112 ambayo ni namba ya dharura ya Netherlands na 911, ambayo ni namba ya dharura ya Panama yalifanyika. Kwa kutumia kumbukumbu za call logs, polisi waliweza kutambua muda ambao madada walipotea msituni.

Kumbukumbu zilionyesha kuwa kulikuwa na majaribio mawili ya kupiga 112 ndani ya muda mfupo toka mabinti hao waliondoka nyumbani kuanza matembezi yao. Kutokana na msitu kuwa mkubwa, kuna tatizo la mtandao hivyo simu zilishindwa kuungana na mtandao hivyo zoezi lilishindikana.

Polisi waligundua kati ya majaribbio yote 77, ni simu moja tu iliyofanikiwa kuungwa na kituo cha dharura na simu hiyo ilidumu kwa sekunde mbili tu.

dark.jpg

Pia polisi waligundua kwamba tarehe 6, kulikuwa na majaribio kadhaa ya kufungua simu ya Kremers kwa kutumia Nywila isiyo sahihi. Inaonyesha kuanzia tarehe 6, simu ya Kremers ilikuwa ikigoma kufunguka kwakuwa mtu aliyekuwa akijaribu kuifungua alikuwa akiweka nywila isiyo sahihi. Kufikia tarehe 11, simu zote zilikuwa zimezima kutoakana na kuishiwa moto.

Japokuwa haya mambo yote waliyogundua kwenye simu yalikuwa yanastaajabisha lakini si kwa kiwango kile kwa mambo waliyoyagundua kwenye kamera.

Picha za awali katika kamera zilionyesha kuwa zilichukuliwa asubuhi ya tarehe 1, pale tu mabinti hao walipoondoka nyumbani. Picha hizo ziliwaonyesha mabinti hao wakiwa kwenye njia karibu na eneo linalojulikana kama Continental Divide kwenye msitu huo. Katika picha hizo hakuna jambo lolote linalotia shaka.

Hata hivyo picha zinazofuata zilikuwa ni za kushtusha.

kremer.jpeg

Picha ya kwanza inayoshtua ni hii hapa. Picha zote za awali zilionyesha mabinti hao wakiwa wanatabasamu na wenye furaha ila hii picha ilionyesha kama vile alikuwa ana wasi wasi kama vile anatazama jambo lenye kuleta wasiwasi.

Pia picha zinazofuata zinaonyesha kuwa zimepigwa usiku kati ya saa saba na kumi usiku wa tarehe 8. Picha hizo zinaonyesha vitu vya binti hao vikiwa vimetapakaa chini kwenye miamba. Pia picha moja inaonyesha sehemu ya nyuma ya kichwa cha Kremers kikiwa kina matone ya damu inayovuja kutoka kwenye utosi.

Pia kuna zaidi ya picha 99 zilizopigwa anga bila mpangilio maalum kama vile mtu alikuwa anapiga piga tu ambazo polisi walishindwa kuelewa zilikuwa zina lengo gani. Maana upigai wake hauna focus wala angle ya kueleweka na zimepigwa katika kipindi cha masaa manne usiku.

Polisi waliamua kuchunguza eneo walilookota begi hilo, ambapo polisi waigundua nguo za Kremers karibu na eneo hilo zikiwa zimekunjwa vizuri, zikiwa pembeni mwa kingo ya mto. Baada ya miezimiwili, katika eneo hilo hilo, mfupa wa kiunoni na mguu ukiwa ndani ya kiatu, ulikutwa eneo hilo.

Baada ya hapo, mifupo ya mabinti wote wawili iligunduliwa. Mifupa ya mguu wa Lissane ikiwa inaondekana mwili wake ulioza kawaida, kwasababu kulikuwa bado na vipande vya nyama kwenye mfupo iliokotwa.

Lakini mifupa ya Kremers ilikuwa myeupe na iliashiria kwamba mwili wake ulimwagiwa chemicali maalum ya kuuharibu.

Polisi waliwahoji watembeza watalii wa mji huo na watu wengine ambao walikuwa katika eneo hilo wakati mabinti hao walipopotea, lakini hakuna taarifa yenye manufaa waliyoipata. Pia hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kufahamu nini kilisababisha vifo vyao.

Polisi waliamua kuwa vifo vyao vilitokana na ajali ya kuanguka wakati wakivuka daraja la kamba na kwamba walibebwa na maji mpaka eneo yalipokutwa mabaki yao. Lakini hii iliacha maswali ambayo hayana majibu.
1. Mbona mabaki yao yanaonyesha kwamba miili yao ilkatwa vipande vipande maana baadhi ya mifupa haikuwa kupatikana.
2. Kwanini begi lilikutwa likiwa kavu bila maji kama kweli walianguka kwenye mto na kubebwa na maji na ilikuwa ni kipindi cha mvua muda wote waliokuwa wanatafutwa mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.
3. Ilikuaje nguo za Kremers zikakutwa zikiwa zimekunjwa vizuri na kuwekwa pembeni ya kingo za mto?

Hakuna ajuaye kilichowapata mabinti hao hata baada ya familia kutoa zawadi ya $32000 kwa yeyote atakayetoa taarifa .
 
View attachment 1631245

View attachment 1631254

View attachment 1631258

View attachment 1631262

Duuu,Visa vingine vina maumivu sana,Mungu ndo ajuaye kilichowapata
 
Ahsante sana ...
Ila inashangaza kweli-kweki kwamba hadi sasa FBI wameshindwa kung'amua
Mkuu ni Panama walikopotelewa FBI wanafanya kazi ndani ya USA kwa ajili ya raia wa Marekani siyo taifa jingine. Halfu hata hivyo kila mwaka Marekani wanapotea watu 600,000 na wengi hata FBI na polisi wanashindwa kung'amua nini kiliwapata. Kuna visa vingi vya kushangaza vya watu waliopotea Marekani nikipata muda nitakuletea baadhi. Vingine vinastajaabisha sana sana kuliko hata hiki.
 
Back
Top Bottom