Mohamed Said nashukuru sana kwa clip yako na juhudi zako ktk kufukua historia ya harakati za uhuru. Ila mim na wewe tutatofautiana ktk interpretation. Kuna jambo kubwa sana hapa umeliibua lakin kwakuwa wewe ni msimulizi mzuri umelipotezea. Jambo hilo ni kuwa kuna waislam mashuhuri sana waliokuwa mstari wa mbele ambao walikuwa vibaraka wa wazungu-kwao mzungu alikuwa mtu mwema tu. Mbwembwe zote za KK kumbe alikuwa 'Usalama wa Taifa' wa mkoloni. Hii ni aibu kubwa. Kwa hili, huwezi tena kutaja neno uhuru halafu ukataja jina KK au Tambwe.
Kuna wazo kwamba nyie wazee wa Dar mlikuwa comfortable na ukoloni maana mlikuwa na nafasi nyeti ktk serikali ya mkoloni. Kimsingi kama mlishiriki harakati za uhuru, basi lengo lilikuwa vyeo vya wazungu mlivyokuwa mnataman maana mlishaonjeshwa utamu. Mtafiti mzuri ni yule ambaye anafanya ukweli ndio uongee, sio hisia na maoni yake. Wewe mzee wetu ulipaswa kuongelea kwa kina u-snitch wa waislam ktk harakati za uhuru.
Pia sasa tunajua, wazee wako walimuunga mkono kwa sababu ya imani yake, sio uwezo wake. Ndio sababu kuu ya kuwepo manung'uniko mara tu baada ya uhuru. Kwa wazee wa Dar, Nyerere hakuwa na umuhimu tena maana kazi yake ilikuwa kuleta uhuru tu. Kufutwa kwa EAMWS ilikuwa ni matokeo ya mawimbi ya chini kwa chini ya wazee wako kumhujumu Nyerere. Na hapa bado hatujazungumzia harakati za Bibi Titi na jaribio la mapinduzi.