Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Dereva gari dogo alikuwa na stress za mapenzi ehh...na mke wake [emoji848]

Wazee wa kata ndoa mmeiona hii

Ova
Ndio uhalisia huo kiongozi! Ndoa ni mateso! Ndoa ni njaa?doa ni tabu ndoa ni kifo! Faida kuwa kwenye ndoa ni chache,hasara ya kuwa kwenye ndoa ni kubwa,kataa ndoa.
 
Hii ndio hoja na hasa baada ya kujua serikali Ina mkono wake
Siyo kila mtu ana smart phone na si kila mmoja hufuatilia media hapa tz, mwamba Osman ni baharia, ngumu kufuatilia maisha ya baharia
 
Up to all yule jamaa wa gari ndogo alikamatwa?, maana kwenye sinema hapo anaonekana alimenya mbuga kwa speed kubwa sana.
Lile pigo lilimtoa kwenye control ya gari na kupelekeshwa uelekeo ambao hakuwa anaelekea. Sio kwa kupenda.
 
Huenda Osman aliaga anaenda Mtwara atakaa wiki 2 ndipo arudi Dsm.
Vinginevyo familia yake hawako siriaz.
Yaani kwa kifupi hawa jamaa hata mawasiliano ya simu hawana! Sitaki kuamini mume anaweza kuaga anasafiri na asipige simu hata kwa mkewe kumjulisha kuwa amefika salama au hata mke kumpigia simu mumewe kuulizia maendeleo ya safari yake. Umasikini kweli unaleta kutokujali.
 
Huna ukichoandika, ile CCTav haikuonyesha sura na si rahisi kumjua. Na mtu alishaaga anaweza kusafiri na chonbo, sasa wasiwasi utoke wapi
Ina maana mume na mke huwa hawapeani taarifa mmoja anaposafiri kama amefika salama!?
 
Wazee siyo kila mtu anazo hizo jerojero za vocha
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa ukiwa masikini unakuwa huna ndugu WA karibu,

Watu wanakupa thamani ya chini sana

Ndio maana vijana wengi wanasaka Hela za ndumba.
Hili ndio jibu ukiwa huna hela watu wanakua hawana mpango na wewe hata demu wako hakujulii hali had uanze....
Ni kawaida tu ukifulia kukaa siku nzima simu haijaita so unaeza potea watu wakastuka baadae sana
 
Samahani mkuu umeshawahi kukaa uswahilini na maanisha uswazi kweli mke hana simu mume hana simu mume anaondoka kwenda, kutafuta kibarua akipata sawa akikosa sawa na ndo mtindo wao wa maisha akiondoka atarudi tuu kwa sababu Niko uswazi familia kama hizo nyingi mwingine alizikwa mpka na manispaa mke hajui
 
Ishu ya information kusaka taarifa ni kwa zile Jamii zilizostaarabika. Na sio uswahili wao uchagua taarifa za kuzifatilia.
Umasikini unaleta roho mbaya
Kweli, tunaona watoto wa kishua wanapelekwa school, mguu kwa mguu hadi getini, hata shule ikiwa mita chache toka nyumbani, sisi masikini hatuna time, mtoto anapiga makasia kuvuka mto kwenda shule mwenyewe
 
Lile pigo lilimtoa kwenye control ya gari na kupelekeshwa uelekeo ambao hakuwa anaelekea. Sio kwa kupenda.
Ukiangalia footage ya sinema utaona jamaa alikanyaga mafuta na kusepa, inaonekana alijua kachemka so bora akamatwe siku nyingine akiwa katulia ila siyo siku ya tukio damu ikiwa inachemka!.
 
Ukiangalia footage ya sinema utaona jamaa alikanyaga mafuta na kusepa, inaonekana alijua kachemka so bora akamatwe siku nyingine akiwa katulia ila siyo siku ya tukio damu ikiwa inachemka!.
Hapana ile gari baada ya kupigwa ilikwenda wangu wangu ikikosa kosa watu mpaka ilipoenda kusimama kwenye kituo cha mafuta pale Kisutu palipo pia na kituo cha basi cha mwendo kasi. Ni kwa vile hakuna footage ya matukio ya kule gari ndogo ilipoelekea. Kwa ule mzinga aliopigwa hiyo akili ya kuendesha gari akikimbia angeipata wapi!?
 
Maelezo ya mke wa Osman yana mashiko sana wavuvi wakiondoka na chombo hukaa Hadi wiki na zaidi na bahati mbaya baharini ama baadhi ya visiwa network sio nzuri ama hamna kabisa.

Kuhusu taarifa mpaka Osman anatoka ICU kulikua hamna picha yake halisi hata wewe sasa hujaona picha ya Osman na cctv haijatoa muonekano vizuri wa Osman

Baada ya kutoka ICU alivyotaja jina na anapotokea ilikua ni rahisi kWa ndugu kuhisi yawezekana ni ndugu Yao.
 
Umeandika vyema. UMASIKINI NI MBAYA SANAA!Tupambane wakuu tusiache pia kuwashika ndugu mikono angalau ukoo uwe na ahueni. Fikiria tu mimi niliyepo Kijijini huku KITEFU -Meru nimeona taarifa yake na kuifuatilia ila ndugu wa hapo tu wamekausha mpk jana, ingekuwa family inayojiweza lazima tu siku ile ile ingejua kutoweka kwa ndugu yao.UMASIKINI UNAFANYA UWEPO WAKO USITAMBULIKE.
 
Pia wanawake wengi wana viswaswadu, hawana vishkwambi kama angeona footage,,
Nyumba zingine hazina tv,, miaka hii sio kama ya zamani miaka ya 90,watu walikua wanawahi saa mbili hata baa za jirani kuangalia taarifa ya habari ya ITV,, Wakati wanasubiri kuangalia tamrhilia za kina Seki😁
 
Ni uzembe tu wangetaka mjua wangemjua kupitia NIDA, NEC finger prints
Nduu yangu wapo watu umri wa 35+ hawana kitambulisho chochote iwe NIDA (Uraia) , NEC (Kura) au leseni ya udereva au NHIF.
Wapo wengi tu nawafahamu na wengine hawana simu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…