Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Nakazia

NIDA waboreshe taarifa za Watanzania kwenye Vitambulisho wangeScan kidole cha mhanga pale pale taarifa za DADA, KAKA, WATOTO, BABA nk zingeonekana na wajulishwe. Hizi habari za mgonjwa kakosa ndugu karne ya 21 ni upuuzi.

Hii itasaidia CITY kutozika ndugu zetu ambao tunawatafuta bila mafanikio. Hili nalo wakaliangalieee
 
Huenda Osman aliaga anaenda Mtwara atakaa wiki 2 ndipo arudi Dsm.
Vinginevyo familia yake hawako siriazi.
 
Hizi kiki tunazitafuta kwa maumivu ni kukosa utu. May be ndio nini?
Haya hujafa hujaumbika
 
Ajali ya mwendokasi ilyotokea wiki moja iliyopita maeneo ya kisutu ina shangaza mengi!

Ajali ile ilitokea majira ya asubuhi na kuhusisha gari dogo kugongana na mwendokasi ulikochangia majeruhi kadhaa akiwemo bwana mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu (Osman)

Taarifa za vyombo vya habari, report za hospital na report za kipolisi zilieleza wazi kila kitu kilichojili (sitarudia)

Takribani karibu siku saba baadae zimepita hadi Jana 27 February 2023! Taarifa za hospital ziliendelea kueleza HAKUNA MTU aliyejitokeza kwenda kumtambua mhanga wa ajali (bwana OSMAN)

Baada ya taarifa ya hospital kutaja kwamba yule mtu kazinduka! Ufahamu umerejea! Leo tarehe 28 ndipo Tunamshuhudia mke wa Osman pamoja na ndugu akijitokeza kumtambua (Yote ni kheri ya Mungu).

Tunashukuru ndugu wamepatikana, lakini kupatikana kwao kwa vyovyote vile kunaibua maswali mengine ingawa tunashukuru wamepatikana!

Simulizi za mke wa Osman!

Mama huyu kwa mara kwanza kasikika akisimulia kwamba hakuwa na taarifa Yoyote hadi pale shemeji yake jana alipomtaarifu kwamba, Taarifa za hospital zinazomtaja OSMAN (wanahisi Osman anayetajwa kupata nafuu hospital ni ndugu yao)!

Mke wa OSMAN Anaendelea kusimulia kwamba, Siku ya tukio, mmewe alimuaga kama kawaida yake kwamba anakwenda kibaruani (kwamba OSMAN anajishughulisha na kubeba mizigo hapo Ferry) kwamba alimuaga kuwa huenda anatarajia kusafili na chombo siku hiyo kwa siku kadhaa!

Haya ni maelezo ya mkewe OSMANI!

Maelezo hayo yanaukweli mwingi kwamba huenda ni kweli kwamba alijua mme wake kasafili ndiyo maana hakuwa na wasiwasi kwamba atarudi!

Lakini maelezo hayo hayawezi kuwa kweli pasipo kusindikizwa na style yao ya maisha, history, uhusiano wao kama familia!

Ni kweli alisafili kama alivyoaga, je baada ya siku ya kwanza, ya pili ya tatu mke na ukoo wao wote na majilani hawakuona ya mtandaoni kiasi cha kushituka?
Sawa mke hana simu je majilani na ndugu hawakuona angalau kufananisha fananisha?

Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA!
Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia yakutojali!

  • YAMKINI KWASABABU YA UMASKINI huenda ndugu na jamaa waliamini yule jamaa kakata moto hivyo wakaamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwakuogopa bili ya hospitali (gharama za matibabu) mke,ndugu na jamaa waliamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwa tabia za maisha yao ni kama UMEME WETU, kwamba mme akiondoka haagi na akirudi tunashangilia huooo! (May be)
  • YAMKINI SASA BAADA YA KUSIKIA KAZINDUKA (OSMAN) Familia na ndugu wameogopa kwamba atawaumbua kwa kuwataja! Hivyo sasa wamejitokeza chapu! (May be)
  • YAMKINI huyu wameona huyu mtu kapona sasa huenda kuna matunda mbele ya misaada (may be)

Tunashukuru ndugu wamepatikana lakini YAMKINI ...na may be ....Havitaacha kugonga vichwani mwa watu wengi.

Yote kwa yote mipango ya Mungu haina makosa , Na kila uzao hauwezi kupatikana pasipo kutungwa mimba!

Ajali ya mwendokasi ilikuwa mimba ya kumuumba OSMAN MPYA!
Mimba ile ilutungwa kwa mwenye gari dogo! Taarifa za kipelelezi zinaonesha yule mwenye gari dogo alikuwa na mgogoro na mkewe uliomjaza stress!
Stress za mapenzi kwa dreva wa gari dogo zilimfanya apoteze umakini barabarani (uzembe)

Hadi pale alipokatiza hovyo na kugonjwa na mwendokasi! Kulikopelekea gari la mwendokasi kwenda kumgonga bwana OSMAN!

MBIO ZA YULE MLINZI HAZIKUWA NA FAIDA, BALI MIMBA Ile ilikuwa kwa ajili ya kumzaa OSMAN MPYA!

Tumuombee apone mapema!

USHAURI!
1. HOSPITALI ZINAPOTANGAZA KUTAFTA NDUGU wasiache kutamka wazi kwamba HAKUNA DENI WALA BILI KWA NDUGU! Ikiwezekana anayejitokeza waseme watamsaidia kumsafilishia mgonjwa hadi nyumbani! (Hili litasaidia watu wasiwe wanauchuna na kutelekeza ndugu na jamaa)
2. NIDA wapoleshe taarifa za vidole na database! Kwamba alama za vidole ziwekwe kwenye kanzudata ya taifa ili hospital wakiskani vidole taarifa za mtu na ndugu zijazwe huko

Heri maskini wa roho kuliko maskini wa mali maana ni rahisi sana kukosa ufalme duniani na mbiguni!

Tubuni na kuiamini injili
 
Majilani wasingekausha pangetokea minong'ono tu.
Hisia hizi ni zako na hazina msingi wowote....unawasingizia MAJILANI BULE
 
Mimba ya Osman mpya una maana gani?
Kwamba kupitia tukio hili kumezaliwa tabia mpya kuanzia kwa mhanga hadi jamii yote kwa ujumla mfano kama bwana Osman alikuwa na tabia ya kutoka na hata kama atachelewa anakuwa hapigi simu kutoa taarifa atabadilika, kama mke wa Osman hana tabia yakumpigia simu mumewe mara kwa mara, atabadilika, kama wana jamii hawajaliana kwa kuulizana hali kila baada ya muda mfupi, watabadilika, hilo ndio somo nilivyolielewa, imekuwa wamezaliwa upya au wamefunzwa tabia mpya
 
Ni uzembe tu wangetaka mjua wangemjua kupitia NIDA, NEC finger prints
Ndugu je ni kila mwana jamii anavyo hivyo? Kuna watu wana changamoto na ukimwambia hivyo vitu sijui anaviona kama unamwambia nini? Nina mwanangu mmoja nikikwambia hana NIDA wala cha kura hauwezi kuamini😂😂😂😂😂
 
Ni uzembe tu wangetaka mjua wangemjua kupitia NIDA, NEC finger prints
Nani ana muda huo? Nchi hii tena kwa masikini!! Angekuwa ni mzungu asiwe hata na kitambulisho chochote kile ,siku ile ile angetambulika!! Wao kama hutambuliki na umekufa wanazika tu.
 
Kwamba kupitia tukio hili kumezaliwa tabia mpya kuanzia kwa mhanga hadi jamii yote kwa ujumla mfano kama bwana Osman alikuwa na tabia ya kutoka na hata kama atachelewa anakuwa hapigi simu kutoa taarifa atabadilika,kama mke wa Osman hana tabia yakumpigia simu mumewe mara kwa mara,atabadilika,kama wana jamii hawajaliana kwa kuulizana hali kila baada ya muda mfupi,watabadilika,hilo ndio somo nilivyolielewa,imekuwa wamezaliwa upya au wamefunzwa tabia mpya
Hayo ndio maisha ya jamii masikini!!sio rahisi kusema eti tukio hili litabadirisha kitu kwani ndio tukio la kwanza?baba anenda kutafuta kazi hata siku tatu,na hajui hali ya nyumbani kwani anajua alichowaachia kitaisha baada ya siku hizo!!
 
Ile footage ya CCTV siyo rahisi kumfahamu huyo bwana tena jirani tu, ukizingatia alikuwa ameipa mgongo camera.

Hivyo vyombo si vina bima? Bill ya hospital ina wenyewe tena hospital itamsaidia ku-process ili wadake chao mapema!

Ingekuwa magari yaliyohusika hayajulikani ingekuwa mziki.

Nachojiuliza: Ina maana wafanyakazi wenzie huko ferry walipoona kimya hakuna hata mmoja wa kumtafuta nyumbani kwake?

Hana hata rafiki wa kumuulizia kwa mkewe baada ya kumkosa kijiweni?

Ni lifestyle ya hovyo mno hii.
 
Ile footage ya CCTV siyo rahisi kumfahamu huyo bwana tena jirani tu, ukizingatia alikuwa ameipa mgongo camera.

Hivyo vyombo si vina bima? Bill ya hospital ina wenyewe tena hospital itamsaidia ku-process ili wadake chao mapema!

Ingekuwa magari yaliyohusika hayajulikani ingekuwa mziki.

Nachojiuliza: Ina maana wafanyakazi wenzie huko ferry walipoona kimya hakuna hata mmoja wa kumtafuta nyumbani kwake?

Hana hata rafiki wa kumuulizia kwa mkewe baada ya kumkosa kijiweni?

Ni lifestyle ya hovyo mno hii.
YAMKINI
 
Uswahilini kwetu simu ya kupyatila ni ishu kubwa na aliyenayo basi anatumia Facebook na YouTube kucheki mastaa wamefanya nini.
 
Back
Top Bottom