Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Ina maana mume na mke huwa hawapeani taarifa mmoja anaposafiri kama amefika salama!?
Nomekwambia YAMKINI anatoweka kama UMEME na anarudi kama UMEME huoooooo
 
Osman apate mwanasheria wakuhahakikisha analipwa kila tone la stahiki zake (afidiwe)
*ulemavu km utajitokeza
*muda wa kuwa nje na shughuli zake
*kadhia nyngine alizopitia na anazopitia baada ya ajali
#Osman Kwanza
 
Ni uzembe tu wangetaka mjua wangemjua kupitia NIDA, NEC finger prints
hayo ni ya kwako wewe mjuaji, hivi huko mitaani unadhani mke wake atakumbuka fingerprints? Au una uhakika gani kuwa anacho kitambulisho cha NIDA au NEC? kuna wengine mpaka leo wamepewa namba tu bado hawana vitambulisho
 
Ingekua nchi zingine Bwana Omary sasa hivi ni Tajiri kwa pesa ambayo angelipwa.

Hata hapa hapa Africa ingekua ni nchi kama South Africa asingekosa kima cha chini kabisa 150 millions.
Samahani mkuu....
Hivi 150 miluons ni utajiri??
 
Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA!
Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia yakutojali!
Hii ni kweli asilimia 💯
 
Ajali ya mwendokasi ilyotokea wiki moja iliyopita maeneo ya kisutu ina shangaza mengi!

Ajali ile ilitokea majira ya asubuhi na kuhusisha gari dogo kugongana na mwendokasi ulikochangia majeruhi kadhaa akiwemo bwana mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu (Osman)

Taarifa za vyombo vya habari, report za hospital na report za kipolisi zilieleza wazi kila kitu kilichojili (sitarudia)

Takribani karibu siku saba baadae zimepita hadi Jana 27 February 2023! Taarifa za hospital ziliendelea kueleza HAKUNA MTU aliyejitokeza kwenda kumtambua mhanga wa ajali (bwana OSMAN)

Baada ya taarifa ya hospital kutaja kwamba yule mtu kazinduka! Ufahamu umerejea! Leo tarehe 28 ndipo Tunamshuhudia mke wa Osman pamoja na ndugu akijitokeza kumtambua (Yote ni kheri ya Mungu).

Tunashukuru ndugu wamepatikana, lakini kupatikana kwao kwa vyovyote vile kunaibua maswali mengine ingawa tunashukuru wamepatikana!

Simulizi za mke wa Osman!

Mama huyu kwa mara kwanza kasikika akisimulia kwamba hakuwa na taarifa Yoyote hadi pale shemeji yake jana alipomtaarifu kwamba, Taarifa za hospital zinazomtaja OSMAN (wanahisi Osman anayetajwa kupata nafuu hospital ni ndugu yao)!

Mke wa OSMAN Anaendelea kusimulia kwamba, Siku ya tukio, mmewe alimuaga kama kawaida yake kwamba anakwenda kibaruani (kwamba OSMAN anajishughulisha na kubeba mizigo hapo Ferry) kwamba alimuaga kuwa huenda anatarajia kusafili na chombo siku hiyo kwa siku kadhaa!

Haya ni maelezo ya mkewe OSMANI!

Maelezo hayo yanaukweli mwingi kwamba huenda ni kweli kwamba alijua mme wake kasafili ndiyo maana hakuwa na wasiwasi kwamba atarudi!

Lakini maelezo hayo hayawezi kuwa kweli pasipo kusindikizwa na style yao ya maisha, history, uhusiano wao kama familia!

Ni kweli alisafili kama alivyoaga, je baada ya siku ya kwanza, ya pili ya tatu mke na ukoo wao wote na majilani hawakuona ya mtandaoni kiasi cha kushituka?
Sawa mke hana simu je majilani na ndugu hawakuona angalau kufananisha fananisha?

Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA!
Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia yakutojali!

  • YAMKINI KWASABABU YA UMASKINI huenda ndugu na jamaa waliamini yule jamaa kakata moto hivyo wakaamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwakuogopa bili ya hospitali (gharama za matibabu) mke,ndugu na jamaa waliamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwa tabia za maisha yao ni kama UMEME WETU, kwamba mme akiondoka haagi na akirudi tunashangilia huooo! (May be)
  • YAMKINI SASA BAADA YA KUSIKIA KAZINDUKA (OSMAN) Familia na ndugu wameogopa kwamba atawaumbua kwa kuwataja! Hivyo sasa wamejitokeza chapu! (May be)
  • YAMKINI huyu wameona huyu mtu kapona sasa huenda kuna matunda mbele ya misaada (may be)

Tunashukuru ndugu wamepatikana lakini YAMKINI ...na may be ....Havitaacha kugonga vichwani mwa watu wengi.

Yote kwa yote mipango ya Mungu haina makosa , Na kila uzao hauwezi kupatikana pasipo kutungwa mimba!

Ajali ya mwendokasi ilikuwa mimba ya kumuumba OSMAN MPYA!
Mimba ile ilutungwa kwa mwenye gari dogo! Taarifa za kipelelezi zinaonesha yule mwenye gari dogo alikuwa na mgogoro na mkewe uliomjaza stress!
Stress za mapenzi kwa dreva wa gari dogo zilimfanya apoteze umakini barabarani (uzembe)

Hadi pale alipokatiza hovyo na kugonjwa na mwendokasi! Kulikopelekea gari la mwendokasi kwenda kumgonga bwana OSMAN!

MBIO ZA YULE MLINZI HAZIKUWA NA FAIDA, BALI MIMBA Ile ilikuwa kwa ajili ya kumzaa OSMAN MPYA!

Tumuombee apone mapema!

USHAURI!
1. HOSPITALI ZINAPOTANGAZA KUTAFTA NDUGU wasiache kutamka wazi kwamba HAKUNA DENI WALA BILI KWA NDUGU! Ikiwezekana anayejitokeza waseme watamsaidia kumsafilishia mgonjwa hadi nyumbani! (Hili litasaidia watu wasiwe wanauchuna na kutelekeza ndugu na jamaa)
2. NIDA wapoleshe taarifa za vidole na database! Kwamba alama za vidole ziwekwe kwenye kanzudata ya taifa ili hospital wakiskani vidole taarifa za mtu na ndugu zijazwe huko

Heri maskini wa roho kuliko maskini wa mali maana ni rahisi sana kukosa ufalme duniani na mbiguni!

Tubuni na kuiamini injili
Mke wa Osman anaitwa nani na je ni mke mdogo au mkubwa? Ili nitoe ushauri
 
Samahani mkuu....
Hivi 150 miluons ni utajiri??
Utajiri ni relative term. Yaani inategemea na hali yako ya kiuchumi wakati unaipata hiyo fedha. Kwangu ambaye sijawahi kuishika 5,000,000 ya pamoja, kuishika millioni 150 nahesabu huo ni utajiri. Ila kwa yule mwenye bilioni na zaidi inawezekana ni pesa ndogo tu kwake.
 
Huna ukichoandika, ile CCTav haikuonyesha sura na si rahisi kumjua. Na mtu alishaaga anaweza kusafiri na chonbo, sasa wasiwasi utoke wapi
Zipo clip 2 nyingine huenda hujaiona mkuu, ipo wananchi wanamrekod badala ya kumsaidia amelowa damu kalala chini na alikua anapumua iyo alionekana vzr tu ipo humu humu Jamii forums.
 
Utajiri ni relative term. Yaani inategemea na hali yako ya kiuchumi wakati unaipata hiyo fedha. Kwangu ambaye sijawahi kuishika 5,000,000 ya pamoja, kuishika millioni 150 nahesabu huo ni utajiri. Ila kwa yule mwenye bilioni na zaidi inawezekana ni pesa ndogo tu kwake.
Basi sawa mkuu, mie niliuliza swali tu ili nipate ufahamu
 
Umeandika mambo mengi yaliyojaa hisia tupu.
Kwani wewe kwanini huamini kwamba mke wake aliagwa kama hatorudi nyumbani atasafiri?
Kwani amepata ajali feri kwenye kivuko hadi apatwe na taharuki?

Inawezekana akisafiri hawafanyi mawasiliano ya marakwamara hivyo kukitokea tatizo inakua ngumu kutambua.
Kwani wewe tukikuambia utupe hiyo video iliyoonekana mtandaoni unaweza ukagundua kama yule mtu ninani?
Unafikiri kama familia walijua wakaamua kunyamaza(jambo ambalo nihisiatu) je majirani walisema wakaambiwa tulieniiiii?
Video ile sidhani kama unaweza ukamtambua yule ninani
 
Back
Top Bottom