Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Kisa cha aliyegongwa na mwendokasi (Osman): Kinahuzunisha, kinafundisha na kushangaza

Sitashangaaa bill na gharama za matibabu zikimuangukia jamaa bila kupewa hata mia. Nchi hiii iiiii
 
Samahani mkuu umeshawahi kukaa uswahilini na maanisha uswazi kweli mke hana simu mume hana simu mume anaondoka kwenda, kutafuta kibarua akipata sawa akikosa sawa na ndo mtindo wao wa maisha akiondoka atarudi tuu kwa sababu Niko uswazi familia kama hizo nyingi mwingine alizikwa mpka na manispaa mke hajui
Kuna mazingira ni hatari, ukitoka kama hujatoka na usipotoka kama hujatoka tu! Yaani uko full viduku, la 4 kama chuo, watoto wana watoto, unasonga ugali mboga maharage ya kupimiwa na mwiko, mwiko 300, wenye kunywa supu ya mapupu au ngozi ya ng'ombe baki! MAE! Wake kwa waume wanabet tu hakuna uzingativu wa 18+ hadi watoto ktk Dubu😂 hapo mke hamjui mume wala mume hamjui mke na ikitokea mmojawapo kakutwa na la kukutwa Mungu jaalia mwanajamii amgumie kinyume na hvyo mwenzako anapiga hesabu kuwa umeenda kupiga show ya ndondo nae anatafuta wake😂
 
Up to all yule jamaa wa gari ndogo alikamatwa?, maana kwenye sinema hapo anaonekana alimenya mbuga kwa speed kubwa sana.
Na yeye yupo ICU hapo hapo MNH somebody Jumbe Mohammed ,ile gari ukiiangalia ile video vizuri utaona baada ya kupigwa ilielekea uelekeo wa kushoto sasa kule ilienda kujipiga ukutani airbags zikafunguka na driver alibanwa na steering,ameumia sana kwa ndani hakuna alipovunjika hali yake ilikuwa mbaya ila toka juzi jumamosi ilikuwa imetengamaa kidogo.

Ktk biashara yangu nina mteja wangu tunafahamiana sana jana nilikuwa na ahadi nae sasa akawa amekuja nje ya wakati ktk kujitetea tetea ndo kuniambia ktk hii ajali dereva alikuwa mjomba'ake muajiriwa wa Rwandan Air (hata gari aliyopata nayo ajali ni ya shirika hilo na pale alikuwa na safari ya airport)so walikuwa na process za kumfanyia dhamana pale kituo cha kati kutokana na pale hospital pana askari kila saa mgonjwa wao akipata nafuu akiona mazingira yale anazidiwa upya wakaomba wamdhamini askari waondolewe ili kila siku wawe wanaenda wao ku-report central.
 
Ajali ya mwendokasi ilyotokea wiki moja iliyopita maeneo ya kisutu ina shangaza mengi!

Ajali ile ilitokea majira ya asubuhi na kuhusisha gari dogo kugongana na mwendokasi ulikochangia majeruhi kadhaa akiwemo bwana mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu (Osman)

Taarifa za vyombo vya habari, report za hospital na report za kipolisi zilieleza wazi kila kitu kilichojili (sitarudia)

Takribani karibu siku saba baadae zimepita hadi Jana 27 February 2023! Taarifa za hospital ziliendelea kueleza HAKUNA MTU aliyejitokeza kwenda kumtambua mhanga wa ajali (bwana OSMAN)

Baada ya taarifa ya hospital kutaja kwamba yule mtu kazinduka! Ufahamu umerejea! Leo tarehe 28 ndipo Tunamshuhudia mke wa Osman pamoja na ndugu akijitokeza kumtambua (Yote ni kheri ya Mungu).

Tunashukuru ndugu wamepatikana, lakini kupatikana kwao kwa vyovyote vile kunaibua maswali mengine ingawa tunashukuru wamepatikana!

Simulizi za mke wa Osman!

Mama huyu kwa mara kwanza kasikika akisimulia kwamba hakuwa na taarifa Yoyote hadi pale shemeji yake jana alipomtaarifu kwamba, Taarifa za hospital zinazomtaja OSMAN (wanahisi Osman anayetajwa kupata nafuu hospital ni ndugu yao)!

Mke wa OSMAN Anaendelea kusimulia kwamba, Siku ya tukio, mmewe alimuaga kama kawaida yake kwamba anakwenda kibaruani (kwamba OSMAN anajishughulisha na kubeba mizigo hapo Ferry) kwamba alimuaga kuwa huenda anatarajia kusafili na chombo siku hiyo kwa siku kadhaa!

Haya ni maelezo ya mkewe OSMANI!

Maelezo hayo yanaukweli mwingi kwamba huenda ni kweli kwamba alijua mme wake kasafili ndiyo maana hakuwa na wasiwasi kwamba atarudi!

Lakini maelezo hayo hayawezi kuwa kweli pasipo kusindikizwa na style yao ya maisha, history, uhusiano wao kama familia!

Ni kweli alisafili kama alivyoaga, je baada ya siku ya kwanza, ya pili ya tatu mke na ukoo wao wote na majilani hawakuona ya mtandaoni kiasi cha kushituka?
Sawa mke hana simu je majilani na ndugu hawakuona angalau kufananisha fananisha?

Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA!
Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia yakutojali!

  • YAMKINI KWASABABU YA UMASKINI huenda ndugu na jamaa waliamini yule jamaa kakata moto hivyo wakaamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwakuogopa bili ya hospitali (gharama za matibabu) mke,ndugu na jamaa waliamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwa tabia za maisha yao ni kama UMEME WETU, kwamba mme akiondoka haagi na akirudi tunashangilia huooo! (May be)
  • YAMKINI SASA BAADA YA KUSIKIA KAZINDUKA (OSMAN) Familia na ndugu wameogopa kwamba atawaumbua kwa kuwataja! Hivyo sasa wamejitokeza chapu! (May be)
  • YAMKINI huyu wameona huyu mtu kapona sasa huenda kuna matunda mbele ya misaada (may be)

Tunashukuru ndugu wamepatikana lakini YAMKINI ...na may be ....Havitaacha kugonga vichwani mwa watu wengi.

Yote kwa yote mipango ya Mungu haina makosa , Na kila uzao hauwezi kupatikana pasipo kutungwa mimba!

Ajali ya mwendokasi ilikuwa mimba ya kumuumba OSMAN MPYA!
Mimba ile ilutungwa kwa mwenye gari dogo! Taarifa za kipelelezi zinaonesha yule mwenye gari dogo alikuwa na mgogoro na mkewe uliomjaza stress!
Stress za mapenzi kwa dreva wa gari dogo zilimfanya apoteze umakini barabarani (uzembe)

Hadi pale alipokatiza hovyo na kugonjwa na mwendokasi! Kulikopelekea gari la mwendokasi kwenda kumgonga bwana OSMAN!

MBIO ZA YULE MLINZI HAZIKUWA NA FAIDA, BALI MIMBA Ile ilikuwa kwa ajili ya kumzaa OSMAN MPYA!

Tumuombee apone mapema!

USHAURI!
1. HOSPITALI ZINAPOTANGAZA KUTAFTA NDUGU wasiache kutamka wazi kwamba HAKUNA DENI WALA BILI KWA NDUGU! Ikiwezekana anayejitokeza waseme watamsaidia kumsafilishia mgonjwa hadi nyumbani! (Hili litasaidia watu wasiwe wanauchuna na kutelekeza ndugu na jamaa)
2. NIDA wapoleshe taarifa za vidole na database! Kwamba alama za vidole ziwekwe kwenye kanzudata ya taifa ili hospital wakiskani vidole taarifa za mtu na ndugu zijazwe huko

Heri maskini wa roho kuliko maskini wa mali maana ni rahisi sana kukosa ufalme duniani na mbiguni!

Tubuni na kuiamini injili
..."Kanzu data"...huu ni msamiati mpya umetupa na like nimekupa.
 
KATAA NDOA.
Uje ubebe viumbwa
FB_IMG_1677635454000.jpg
 
Ajali ya mwendokasi ilyotokea wiki moja iliyopita maeneo ya Kisutu ina shangaza mengi!

Ajali ile ilitokea majira ya asubuhi na kuhusisha gari dogo kugongana na mwendokasi ulikochangia majeruhi kadhaa akiwemo bwana mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu (Osman)

Taarifa za vyombo vya habari, report za hospital na report za kipolisi zilieleza wazi kila kitu kilichojiri (sitarudia)

Takribani karibu siku saba baadae zimepita hadi Jana 27 February 2023! Taarifa za hospital ziliendelea kueleza HAKUNA MTU aliyejitokeza kwenda kumtambua mhanga wa ajali (bwana OSMAN)

Baada ya taarifa ya hospital kutaja kwamba yule mtu kazinduka! Ufahamu umerejea! Leo tarehe 28 ndipo Tunamshuhudia mke wa Osman pamoja na ndugu akijitokeza kumtambua (Yote ni kheri ya Mungu).

Tunashukuru ndugu wamepatikana, lakini kupatikana kwao kwa vyovyote vile kunaibua maswali mengine ingawa tunashukuru wamepatikana!

Simulizi za mke wa Osman!

Mama huyu kwa mara kwanza kasikika akisimulia kwamba hakuwa na taarifa Yoyote hadi pale shemeji yake jana alipomtaarifu kwamba, Taarifa za hospital zinazomtaja OSMAN (wanahisi Osman anayetajwa kupata nafuu hospital ni ndugu yao)!

Mke wa OSMAN Anaendelea kusimulia kwamba, Siku ya tukio, mmewe alimuaga kama kawaida yake kwamba anakwenda kibaruani (kwamba OSMAN anajishughulisha na kubeba mizigo hapo Ferry) kwamba alimuaga kuwa huenda anatarajia kusafiri na chombo siku hiyo kwa siku kadhaa!

Haya ni maelezo ya mkewe OSMANI!

Maelezo hayo yana ukweli mwingi kwamba huenda ni kweli kwamba alijua mme wake kasafiri ndiyo maana hakuwa na wasiwasi kwamba atarudi!

Lakini maelezo hayo hayawezi kuwa kweli pasipo kusindikizwa na style yao ya maisha, history, uhusiano wao kama familia!

Ni kweli alisafiri kama alivyoaga, je baada ya siku ya kwanza, ya pili ya tatu mke na ukoo wao wote na majirani hawakuona ya mtandaoni kiasi cha kushtuka?

Sawa mke hana simu, je majirani na ndugu hawakuona angalau kufananisha fananisha?

Majibu ya hayo yote ni mepesi tu kwamba UMASKINI HULETA TABIA YA KINYAMA! Ninaposema tabia ya kinyama sina maana tabia ya kikatili bali namaanisha Umasikini huzalisha tabia ya kutojali!

  • YAMKINI KWASABABU YA UMASKINI huenda ndugu na jamaa waliamini yule jamaa kakata moto hivyo wakaamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwakuogopa bili ya hospitali (gharama za matibabu) mke, ndugu na jamaa waliamua kukausha! (May be)
  • YAMKINI kwa tabia za maisha yao ni kama UMEME WETU, kwamba mme akiondoka haagi na akirudi tunashangilia huooo! (May be)
  • YAMKINI SASA BAADA YA KUSIKIA KAZINDUKA (OSMAN) Familia na ndugu wameogopa kwamba atawaumbua kwa kuwataja! Hivyo sasa wamejitokeza chapu! (May be)
  • YAMKINI huyu wameona huyu mtu kapona sasa huenda kuna matunda mbele ya misaada (may be)

Tunashukuru ndugu wamepatikana lakini YAMKINI ...na may be ....Havitaacha kugonga vichwani mwa watu wengi.

Yote kwa yote mipango ya Mungu haina makosa, Na kila uzao hauwezi kupatikana pasipo kutungwa mimba!

Ajali ya mwendokasi ilikuwa mimba ya kumuumba OSMAN MPYA!
Mimba ile ilutungwa kwa mwenye gari dogo! Taarifa za kipelelezi zinaonesha yule mwenye gari dogo alikuwa na mgogoro na mkewe uliomjaza stress!
Stress za mapenzi kwa dreva wa gari dogo zilimfanya apoteze umakini barabarani (uzembe)

Hadi pale alipokatiza hovyo na kugonjwa na mwendokasi! Kulikopelekea gari la mwendokasi kwenda kumgonga bwana OSMAN!

MBIO ZA YULE MLINZI HAZIKUWA NA FAIDA, BALI MIMBA Ile ilikuwa kwa ajili ya kumzaa OSMAN MPYA!

Tumuombee apone mapema!

USHAURI!
1. HOSPITALI ZINAPOTANGAZA KUTAFTA NDUGU wasiache kutamka wazi kwamba HAKUNA DENI WALA BILI KWA NDUGU! Ikiwezekana anayejitokeza waseme watamsaidia kumsafirishia mgonjwa hadi nyumbani! (Hili litasaidia watu wasiwe wanauchuna na kutelekeza ndugu na jamaa)

2. NIDA waboreshe taarifa za vidole na database! Kwamba alama za vidole ziwekwe kwenye kanzidata ya taifa ili hospitali wakiskani vidole taarifa za mtu na ndugu zijazwe huko.

Heri maskini wa roho kuliko maskini wa mali maana ni rahisi sana kukosa ufalme duniani na mbiguni!

Tubuni na kuiamini injili
Bonge la article, magazeti yangechukua article kama hizi pia na kuziweka kwao
 
Kuna mazingira ni hatari, ukitoka kama hujatoka na usipotoka kama hujatoka tu! Yaani uko full viduku, la 4 kama chuo, watoto wana watoto, unasonga ugali mboga maharage ya kupimiwa na mwiko, mwiko 300, wenye kunywa supu ya mapupu au ngozi ya ng'ombe baki! MAE! Wake kwa waume wanabet tu hakuna uzingativu wa 18+ hadi watoto ktk Dubu😂 hapo mke hamjui mume wala mume hamjui mke na ikitokea mmojawapo kakutwa na la kukutwa Mungu jaalia mwanajamii amgumie kinyume na hvyo mwenzako anapiga hesabu kuwa umeenda kupiga show ya ndondo nae anatafuta wake😂
Hayo ndo maisha ya uswazi ndo maana sikushangaa mke wake kutokujua
 
Back
Top Bottom