Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Batuli na Ashura walisoma pamoja mikoani, kufika darasa la sita Batuli alihamia jijjni na kukaa na shangazi yake. Alisoma mpaka chuo na kuajiriwa na bank moja mjini. Alipata a mume na kuolewa harusi kubwa tu. Yeye na mume wake walipata nyumba ya NHC mjini maisha yakaendelea.
Batuli alipata watoto watatu wote wa kiume, nyumba yake ni ya vyumba viwili, alipata dada wa kazi wa kutwa anaanza kazi saa moja mpaka saa kumi jioni. Watoto wanasoma English Medium na dada asubuhi anawahi kuwapandisha basi la shule. Mume wa Batuli ni shift manager huko kazini anafanya kazi usiku, mke akiwa kazini yeye ndiyo anakua amepumzika. Haya ndiyo maisha yetu ya mjini. Mkitakka mapenzi ya Kihindi mkashike jembe huko vijijini.
Ashura aliolewa na mwana diplomasia, maisha yake yote alikua nje ya nchi. Ndoa ilipoingiliwa na jini mkata kamba, alirudi kwao. Kufika kijijini kuanza kupikia jiko la mkaa na kuni, aliona namba hazisomeki. Alimuomba mama Batuli namba ya Batuli. Alivyokua ninja baada ya simu ya kwanza ya salamu simu ya pili anapigia Batuli kuwa yuko Mbezi stand ya Magufuli ameishaingia mjini.
Batuli aliona si shida, huyu ni kama ndugu yangu. Alimchukua na kumkaribisha nyumbani. Ashura alianza kupika na dada wa kazi alishukuru kuwa anasaidiwa shughuli, yeye alisafisha nyumba na kufua.
Yule mume wetu shft manager, akiamka anakuta chuzi shata shata. Vilianzia hapo mpaka Ashura akawa anapumzika na mume kabla watoto hawajarudi. Ni hiki kichwa cha migraine kilichomrudisha Batuli nyumbani na kuku mali yake inaliwa.
Matusi yalianza na cha kushangaza, shift manager alichukua maamuzi magumu ya kuondoka na Ashura na kwenda kuanza maisha mapya.