Kisa cha Jaji na profesa katika uchaguzi wa 1995

Kisa cha Jaji na profesa katika uchaguzi wa 1995

Mzee mohamed wewe na udini,udini na wewe,hutufai wewe,kila jambo ni kulalamika tu,
kuna sehemu kasema waislamu hawa jawai kuingia ikulu na mnukuu pale kwenye gazeti lake.alafu mwinyi enzi hizo sijui alikuwa mkristo na kikwete mda huo alikuwa wapi na rafiki yake lowasa
 
1614495518392.png
 
Kamati kuu ndio zao

2015 Ngoyai alikuwa na watu kadhaa ndani ya Kamati kuu akiwemo Nchimbi, Sadifa, Sofia Simba, Kimbisa na wengineo wengi aliowapanga kuwa yakiletwa majina ya Wagombea wakomae mwanzo mwisho hadi Washindwe kumkata Ngoyai

Cha Kushangaza Jk akaja kishakata majina kabisa wao wakabaki na kazi ya kubariki yaliyoletwa

Walipofika kwny NEC wapambe wa Lowassa wakajipanga kujibu hoja za Richmond, Jk akaja na hoja alizotumia Nyerere kumkataa Lowassa 1995

Ngoma ikaanuliwa kabla ya kukauka
 
Jaji Mark Bomani alikuwa kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, kitendo cha yeye kuchukua fomu na huku akiwajua kuwa alikuwa kwenye nafasi hiyo nyeti kilitosha kabisa kumwengua ni kama aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, msajili wa vyama vya siasa Christopher Liundi wote walipotaka kugombea uongozi kupitia CCM walitoswa .
Hata kama Mark Bomani asingekuwa kwenye tume, bado CCM wasingempitisha hata kama angekuwa na sifa kwa 101%! Ni bahati mbaya sana watu tunasoma uzi kwa mihemuko lakini hoja ya MS inaeleweka sana. Bomani hakuwa kwenye circle ya CCM. Usipokuwa kwenye circle ya CCM hata ufanye vipi kuteuliwa utasikia kwenye bomba unless uwe na watu wenye influence wa kuweza kukusimamia kama ilivyokuwa kwa Mkapa na JPM.
 
Hata kama Mark Bomani asingekuwa kwenye tume, bado CCM wasingempitisha hata kama angekuwa na sifa kwa 101%! Ni bahati mbaya sana watu tunasoma uzi kwa mihemuko lakini hoja ya MS inaeleweka sana. Bomani hakuwa kwenye circle ya CCM. Usipokuwa kwenye circle ya CCM hata ufanye vipi kuteuliwa utasikia kwenye bomba unless uwe na watu wenye influence wa kuweza kukusimamia kama ilivyokuwa kwa Mkapa na JPM.
Labda umezaliwa juzi kina bomani wameanza kuwa na influence kwenye nchi kabla ya kupata uhuru, ccm kama chama ilikuwa na vigezo vyake kama angekidhi vigezo wangempitisha.
Kumbukabhuu mchakato ulisimamiwa na mwasisi wa ccm ambaye pia ni rais wa kwanza na mafaili yote alikuwa nayo kama kuwa kwenye circle ya ccm hakuna aliyekuwa na nguvu kama Malecela na alikatwa hata 2015 lowassa alikuwa na nguvu kubwa lakini alikatwa
 
NEC,NA CC ZOOTE KAZI YAO NI KUTIA MHULI KWA ANAETAKIWA KUWA RAIS,RAIS NDANI YA CCM NA TANZANIA HUTENGENWZWA,NA HATA YEYE HUWA HAJUI KAMA KATENGENEZWA NA ANATAKIWA,RAIS WA NCHI HII HAZUKI TU KAMA NCHI ZINGINE ZINACYOFANYA,ANAANDALIWA KBS
 
JAJI MARK BOMANI KATIKA KUMBUKUMBU ZA PROF. KIGHOMA MALIMA UCHAGUZI WA RAIS DODOMA 1995

Nimesoma makala ambayo imezunguka sana katika mitandao ya kijamii kuhusu Mark Bomani katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM mwaka wa 1995.

Makala hii kila nikiisoma inanirudisha nyuma miaka 25 iliyopita wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi baada ya kurejeshwa mwaka wa 1992 na kwa hakika huishia kwa kucheka napomkumbuka Prof. Malima kwani ni kama vile namuona anavyonihadithia kwa staili yake ya hata jambo likiwa zito kiasi gani yeye atakuhadithia katika njia ya kukufanya wewe ucheke na nyie wasikilizaji wake mcheke pia.

Siku moja katika mazungumzo yetu alinihadithia jinsi siasa za Tanzania zinavyochezwa kwa ustadi wa hali ya juu kiasi ni watu wajanja sana ndiyo wanaweza kutambua na kutegua kitendawili pindi kinapomkabili.

Prof. Malima akanipa mfano wa Jaji Mark Bomani pamoja na yeye wa wanachama wengine wa CCM walipoomba uteuzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais na majina yao yafikishwe Halmashauri Kuu ya CCM ili waingizwe kwenye mchakato.

Prof. Malima anasema yeye aliomba uteuzi ule kwa kughadhibishwa na gazeti moja lililoandika mbele kwa wino mweusi wa kukoza, ‘’Waislam Waiogopa Ikulu.’’

‘’Hivi hawa jamaa wanatudharau sana sisi,’’ Prof. Alisema huku anacheka.

Lakini gazeti lile lilikuwa limeandika ukweli.
Hapakuwa na Muislam yeyote aliyechukua fomu kuutaka urais.

Prof. Malima anasema, ‘’Pale pale nikamwambia dereva wangu akaiangalie gari ajaze mafuta safari Dodoma kwenda kuomba nafasi ya kugombea urais.’’

Prof. Malima mwenyewe alikuwa na historia ya kutukuka katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwani akiwa kijana mdogo na bingwa wa hesabu aliacha shule Mzumbe mwaka wa 1957 kurudi kijijini kwao Kisarawe kujiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi wa Julius Nyerere.

Sasa ikiwa Malima hakuiogopa Government House ya Governor Edward Francis Twining na Special Branch yake vipi atishike na Ikulu ambayo anaijua ndani nje?

Wakati ule lile gazeti lilipotoka na maneno yale ya kuwabeza Waislam katika ukurasa wake wa mbele hapakuwa na hata Muislam mmoja aliyeomba nafasi ya kutaka achaguliwe kugombea urais.

Prof. Malima akaendelea kusema kuwa ‘’Mimi nikijua fika siwezi kuchaguliwa lakini nilitaka nitoe jibu kwa lile gazeti kuwa Waislam hatuiogopi Ikulu.’’

Ndani ya Bunge la Tanzania kulikuwa na kikundi cha Wabunge wamejichagua na kutengeneza genge ambalo kazi lililojipa ilikuwa ni kumzomea Prof. Malima ndani ya Bunge kwa kila atakalofanya.

Pamoja na Wabunge hawa walikuwapo pia na wahariri wa magazeti ambao wao kazi yao kuu ilikuwa ni kumuandika Prof. Malima kwa ubaya.

Katika hali hii Prof. Malima alikuwa anaijua hali vizuri sana.

Sasa tuje kwa Jaji Mark Bomani.

Baadhi ya wananchi na marafiki wa Mark Bomani walimwendea na kumuomba agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na inasemekama walimshinikiza sana aombe nafasi hiyo na yeye hakutaka kuwavunja akiamini kuwa anaweza akatoa mchango katika ujenzi wa taifa la Tanzania akawakubalia.

Jaji Bomani hakuwa anafahamika sana katika duru za siasa lakini aliongoza kwa idadi ya wadhamini kwa nafasi ile akifuatiwa na John Malecela.

Prof. Malima akawa anasema, ‘’Wengi katika sisi tuliokwenda Dodoma kufanyiwa usaili ukinitoa mimi wakidhani kuwa zoezi lile lilikuwa linaendeshwa kwa umakini mkubwa na kuwa wagombea watakuwa na nafasi ya kujieleza na yule ambae ataonekana ana sifa zinazohitajika ndiyo atakuwa mshindi.’’

Baada ya kuingia Prof. Malima katika kinyang’anyiro kile cha urais akaongezeka Muislam mwingine – Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikwete katika maziko ya Benjamin Mkapa alisema alisukumwa kuingia kwenye kinyang’anyiro kile na iko siku ataeleza kisa hicho.

Leo baada ya zaidi ya miaka 25 ndiyo nami nimejifunza vipi siasa za Tanzania zinavyoendeshwa.

Prof. Malima amekuwa ndani ya chama kile toka enzi za TANU na nikisoma kumbukumbu zake na kufanya rejea katika mazungumzo yetu natembea katikati ya mistari ya maneno yake.

Kwa hakika nimejifunza mengi.

Nimeoona pia Prof. Malima na yeye kama binadamu amefunzwa mengi mengi ndani ya CCM.

Nimeweza kubaini kuwa kuna sifa za ziada mtu anatakiwa awe nazo ndipo achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ikiwa mimi nimezitambua sifa hizi zisizoonekana kwa macho Prof. Malima yeye bila shaka alikuwa anazijua vizuri na alikuwa na uwezo wa kuziona kwa macho yake mawili.

Kuwa Jaji au Profesa si moja ya sifa za Urais.

Prof. Malima anasema alipofika chumba cha mapumziko kabla ya kuingia ndani kuhojiwa na Central Committeee alimkuta Jaji Mark Bomani keshafika zamani na mkononi ana makaratasi mengi anatalii.

Mkononi Jaji ana kalamu anapiga mstari hapa na pale anahangaika kuweka kila jambo mahali pake.

Wasukuma na Wazaramo ni watani.

Prof. akamuuliza Jaji katika njia ya utani, ‘’Jaji hiyo nini?’’

Jaji Bomani akamjibu, ‘’Hii hotuba yangu mbele ya Kamati.’’

Prof. akacheka sana.

Hapa nilipo ni kama vile namuona Prof. na kicheko chake nakisikia.

Prof. akamwambia Jaji kuwa hawana muda wa kusikiliza hotuba yake na atakuwa na bahati kubwa ikiwa atapewa dakika tatu.

Jaji Bomani alishtuka na Profesa alimuona kwa hakika kabisa Jaji alikuwa kashtuka kwani hakulitegemea hilo.

Iweje jambo muhimu na kubwa kama hili Kamati iwe haina muda wa kuwasikiliza?

Prof. Malima hakuwa na la zaidi la kuongeza alitulia tuli anamwangalia Jaji lakini ndani ya nafsi yake akimuhurumia sana na huruma yake Prof. Malima ilitokana na kuwa Jaji Bomani atavunjika moyo atakapotambua kuwa yeye hakuwa anajua siasa za Tanzania ngoma zinaporindima ni mtindo upi wa ngoma wachezaji hucheza.

Prof. Malima alikuwa anajua fika kuwa si yeye wala Mark Bomani watapitishwa, alikuwa anajua kuwa palitakiwa wawepo watu mfano wa wao ili ngoma inoge.

Prof. Malima aliingia kuhojiwa na kutoka muda mfupi.

Hapa kwenye mahojiano machozi yalinitoka kwa kucheka.

Prof. Malima alijaaliwa kipaji cha kuchekesha.

Hakukaa akiwa wima alimuaga mtani wake Jaji.

Jaji akamuuliza Prof, ‘’Husubiri matokeo?’’

Prof. Malima aliniambia alipigwa na mshangao mkubwa.

Central Committee iliwapitisha - Kikwete, Mkapa na Msuya kuwa majina yatakayokwenda mbele kwa uchaguzi wa jina moja la mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Taarifa zinasema Jaji Mark Bomani aliumia sana kwa kukatwa jina lake.

Prof. Malima yeye njia nzima wakati anarudi Dar es Salaam ni kuwa kila akikumbuka aliyoyaona Dodoma yeye ilikuwa ni kucheka tu kwani yale yalimkumbusha yaliyomfika Chimwaga mwaka wa 1992 pale alipofanyiwa njama asichaguliwe NEC iliyokuwa na viti 20.

Huwezi kuchoka kumsikiliza Prof. Malima kwani alikuwa anajua mengi sana na akiyaeleza kwa namna ambayo ingawa mengi ni ya kusikitisha atakuacha taaban kwa kucheka.
mbona hujaelezea akaamua kuanzisha chama chake cha NRA baada ya kutoswa?
 
mbona hujaelezea akaamua kuanzisha chama chake cha NRA baada ya kutoswa?
Geza Ulole,
Ungeuliza swali hili kwa heshima na adabu ningekuwekea hapa historia nzima ya Prof. Malima katika nyakati zile.

Naamini wengi wangenufaika na tungekuwa na mjadala mzuri.

Mimi hutaabika kumjibu mtu anaeonyesha fedhuli katika maandishi yake.
 
Palikuwa na stori za mitaani mwaka 1995 kuhusu mada hii. Palikuwa na katuni, kama sikosei ya Masudi Kipanya, ikirandana na stori zile.

Oh! How time flies!
 
Labda umezaliwa juzi kina bomani wameanza kuwa na influence kwenye nchi kabla ya kupata uhuru, ccm kama chama ilikuwa na vigezo vyake kama angekidhi vigezo wangempitisha.
Kumbukabhuu mchakato ulisimamiwa na mwasisi wa ccm ambaye pia ni rais wa kwanza na mafaili yote alikuwa nayo kama kuwa kwenye circle ya ccm hakuna aliyekuwa na nguvu kama Malecela na alikatwa hata 2015 lowassa alikuwa na nguvu kubwa lakini alikatwa
Nimezungumzia suala la nchi au suala la CCM? Au unadhani ukishakuwa na influence ndani ya nchi ndo tayari umeshakuwa na influence ndani ya CCM? Na nimeshasema usipokuwa CCM Insider ni LAZIMA awepo wa kukupigania kama ambavyo Mwalimu alimpigania Mkapa kiasi cha kuwashinda akina Malecela!!
 
Back
Top Bottom