Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakumbuka kama sijasahau, kuna mtu alishawahi leta simulizi inafanania na hii ya kwako hata mazingira yana fanana. Yeye alikwenda kusoma sekondari kwa Baba yake mdogo ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule huko Kanda ya Ziwa. Ila Kuna sehemu uliandika Veronica badala ya Vumilia ndio ikanistua kwani moja ya Muhusika wa hiyo simulizi alikuwa ni Veronica ambaye alimpenda huyo jamaa na Veronica naye alikuwa na uhusika wa Uchawi. Sikumbuki vyema ile simulizi ilikuwa inaitwaje labda Kuna wanayo Ikumbuka.Tunaendelea sehemu ya kumi.
Baada ya kumaliza kumwaga maji na kumuacha bibi akilalamika, niliondoka zangu. Siku hiyo kila kitu kilifanyika ilivyotakiwa, baada ya hapo nikarudi nyumbani kwetu, nikaachana na mzee Masele. Lakini wakati tunaagana kuna kitu aliniambia ndio kilichokuwa kinanifikirisha kwa wakati huo.Nakumbuka wakati tunaachana aliniuliza
"Mwanangu hii kazi imefanyika vyema sana, lakini imekuwa nyepesi haswa kwa sababu tumesaidiwa na Yame"
"Kumbe" niliishia kujibu hivyo tu kwa sababu sikujua niseme kitu gani
Mzee Masele aliniangalia kidogo halafu akaniambia
"Unajua mwanangu kule kwenye mkuyu tulikochukua damu ni sehemu hatari na ngumu sana. Sio rahisi kufanikisha jambo kama lile la kuchukua damu kiurahisi kiasi kile sehemu kama ile. Yule Yame muone vile tu, yule mtu ana dawa sio mchezo. Mimi ni mganga ninayeogopeka sana lakini kwa Yule ninanyoosha mikono"
Alitulia kidogo kana kwamba anafikiria jambo, halafu akaendelea...
"Unajua mimi na Yame huwa tunashirikiana kwenye mambo mengi. Nikiwa nampa tiba mtu na nikahitaji msaada wake huwa ananisaidia. Japo hata mimi huwa namsaidia kwenye mambo fulani fulani. Lakini mara nyingi hunisaidia pindi wachawi wakiwa ni wa mbali. Yame huwa mgumu sana kunipa ushirikiano wachawi wakiwa ni wa kijiji hiki. Lakini kwako imekuwa tofauti, ametoa ushirikiano wa haraka sana. Sijajua sababu ila tambua tu una bahati sana mwanangu"
Kauli hii ilikuwa inanifikirisha, na niliwaza ili nipate majibu kwa nini Yame aliamua kunisaidia. Majibu yaliyokuwa kichwani mwangu ni mawili tu.
Kwanza, niliwaza labda ni Kwa sababu ya urafiki kati ya mdogo wake wa kiume na baba yangu. Kama alivyoniambia yeye siku ile tunatafuta damu.
Pili, niliwaza labda anashirikiana na mjukuu wake kuhakikisha naangukia katika mahusiano nae.
Jibu la pili kwangu ndio lilikuwa na mashiko zaidi kwangu. Ndio lilikuwa na mashiko zaidi, kwa sababu kama mchawi anaweza kuua mtoto wa kumzaa mwenyewe kitu gani mtoto wa rafiki wa mdogo wake.
Tuachane na hilo.
Nilipanga kupumzika nyumbani kwa siku tatu, ndio nirudi shule lakini siku tatu hazikuisha. Siku ya pili yake Yule bibi mchawi alikuwa ameshaaga dunia na mtoto wake wa kike, yaani mama mdogo alikuwa yuko mahututi. Watu walishangazwa na kifo kile cha ghafla lakini mimi nilikuwa nacheka kimoyomoyo nikijiona mshindi wa vita. Miezi kama mitatu michache mbele mama mdogo naye alifariki dunia.
Nikawa nimesharudi shule sasa, naendelea na masomo kama kawaida. Nilikuwa nakutana na Vumilia na tulikuwa tunapiga story. Lakini cha ajabu hatukuwahi kuongelea kabisa kilichotokea siku ile usiku, Kuna kipindi nilijaribu kuleta zile story lakini alionekana hayupo interested kabisa kuongelea mambo yale. na tokea niliporudi darasani hakuwahi kuniambia kama ananipenda. Ingawa ilinipa maswali kichwani, lakini moyoni nilifurahi nikiamini labda ameshampenda mwingine ameamua kuniacha. Kiukweli sikutaka kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye viashiria vya uchawi.
Sasa pale darasani kulikuwa na binti mmoja aliyekuwa anaitwa Sara. Huyu binti mimi nilikuwa nafahamiana naye muda mrefu tokea tukiwa wadogo. Japo tulitokea vijiji tofauti na shule ya msingi tulisoma shule tofauti lakini tulikuwa tunafahamiana. Huyu binti alitokea kijiji jirani na chetu, au niseme kijiji ambacho huwa tunakivuka katikati ili ufike kijiji shule yetu ya sekondari iliko. lakini tulikuwa tunasali kanisa moja. Hivyo tulifahamiana kanisani hasa kwenye mambo ya Pathfinder (wasabato wanaelewa). Huyu binti ni mtu ambaye nilikuwa najua ananipenda japo ile kitototo toto tokea enzi hizo. Na mimi najua nilikuwa nampenda, nakumbuka nilikuwa nikienda kanisani nisipomuona nilikuwa nakoswa raha kabisa natamani niende hata kwao nikamuone tu basi. Baba yake alikuwa ni mwalimu na alikuwa ni tajiri kwa level za kijijini, kwa hiyo alikuwa wa kishua fulani. Tulipofika sekondari ni bahati iliyoje tukakutana tena, na tulikuwa marafiki wa kawaida. Moyoni nilimpenda japo sikuwahi kumwambia, labda ni kwa sababu ya udomozege tu.
Moyo wangu ulikuwa umekufa ukaoza kwa huyo binti Sara.
Sasa siku moja nikasema liwalo na liwe lazima nimchane makavu. Sikumuwaza tena Vumilia maana ishapita muda kidogo hatujaongea chochote zaidi ya kuzungumza mambo ya kawaida tu. Niwe mkweli tu mpaka nafika hicho kidato cha tatu nilikuwa sijawahi tongoza mwanamke wala kuwa na mpenzi. Kwa hiyo siku hiyo ndiyo nilipanga kwenda kuandika historia mpya.
Mwalimu wa English alipomaliza tu kupiga porojo zake za " three suitors one husband" mwanaume nikaingia kazini. Nilimfata hadi kwenye dawati lake yule binti nikamnong'oneza
"kuna kitu nataka nikwambie wakati wa break naomba tuonane"
"Alitikisa kichwa kuashiria amekubali"
Wakati wa break uliwadia, sikutaka kulaza damu nilimfuata na kumwambia twende sehemu tukakae tuongee.
"Tukaongee nini mr the dragon tena, si uniambie hapahapa" binti alitaka kukaza
Baada ya kumshawishi sana hatimae alikubali tukaenda kukaa kwenye jiwe fulani palepale shuleni. Sehemu ilipokuwepo shule yetu ilikuwa karibu na vimilima na kulikuwa na miamba au mawe mengi sana yaliyozagaa kila sehemu. Tulifika tukakaa nikaanza kujieleza!
Sikutumia nguvu nyingi mtoto alieleweka, ukizingatia nilikuwa najua mtoto ananipenda toka muda sana.
Baada ya hapo mapenzi kati yangu na yule binti yalianza rasmi, japo ilikuwa kwa siri haikuwa wazi sana.
Siku moja Vumilia alinipa ujumbe wa maandishi darasani wakati ilipogongwa kengele ya kutawanyishwa saa nane na nusu mchana. Ulikuwa na maneno machache tu
"Tutaona na huyo Sara wako, labda sio mimi Vumilia"
Itaendelea
hiyo ni simulizi ya mwamba mmoja huyu ndani anaitwa UMUGHAKA ....hafu kama umenifumbua macho....huyu jamaa kama anatunga kupitia mule mule alopitia umughakaNakumbuka kama sijasahau, kuna mtu alishawahi leta simulizi inafanania na hii ya kwako hata mazingira yana fanana. Yeye alikwenda kusoma sekondari kwa Baba yake mdogo ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule huko Kanda ya Ziwa. Ila Kuna sehemu uliandika Veronica badala ya Vumilia ndio ikanistua kwani moja ya Muhusika wa hiyo simulizi alikuwa ni Veronica ambaye alimpenda huyo jamaa na Veronica naye alikuwa na uhusika wa Uchawi. Sikumbuki vyema ile simulizi ilikuwa inaitwaje labda Kuna wanayo Ikumbuka.
Hiyo simulizi inaitwa "tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe", ni ya UMUGHAKA hiyo na yule mwanamke wa Umughaka alikuwa anaitwa Monica, siyo VeronicaNakumbuka kama sijasahau, kuna mtu alishawahi leta simulizi inafanania na hii ya kwako hata mazingira yana fanana. Yeye alikwenda kusoma sekondari kwa Baba yake mdogo ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule huko Kanda ya Ziwa. Ila Kuna sehemu uliandika Veronica badala ya Vumilia ndio ikanistua kwani moja ya Muhusika wa hiyo simulizi alikuwa ni Veronica ambaye alimpenda huyo jamaa na Veronica naye alikuwa na uhusika wa Uchawi. Sikumbuki vyema ile simulizi ilikuwa inaitwaje labda Kuna wanayo Ikumbuka.
Mine story is very genuine.Nakumbuka kama sijasahau, kuna mtu alishawahi leta simulizi inafanania na hii ya kwako hata mazingira yana fanana. Yeye alikwenda kusoma sekondari kwa Baba yake mdogo ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule huko Kanda ya Ziwa. Ila Kuna sehemu uliandika Veronica badala ya Vumilia ndio ikanistua kwani moja ya Muhusika wa hiyo simulizi alikuwa ni Veronica ambaye alimpenda huyo jamaa na Veronica naye alikuwa na uhusika wa Uchawi. Sikumbuki vyema ile simulizi ilikuwa inaitwaje labda Kuna wanayo Ikumbuka.
uchunguzi wako wa kipuuzipuuzi uutoe hapa,usitake kutuharibia radha,,wengi wetu hiyo story tunaijua hakuna sehemu iliyokopiwa,,, halafu eti unajikuta kumtag umughaka ili aje kushuhudia anavyoibiwa mafaili, u*b*** wewe...Nakumbuka kama sijasahau, kuna mtu alishawahi leta simulizi inafanania na hii ya kwako hata mazingira yana fanana. Yeye alikwenda kusoma sekondari kwa Baba yake mdogo ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule huko Kanda ya Ziwa. Ila Kuna sehemu uliandika Veronica badala ya Vumilia ndio ikanistua kwani moja ya Muhusika wa hiyo simulizi alikuwa ni Veronica ambaye alimpenda huyo jamaa na Veronica naye alikuwa na uhusika wa Uchawi. Sikumbuki vyema ile simulizi ilikuwa inaitwaje labda Kuna wanayo Ikumbuka.
Mulemule wapi?hiyo ni simulizi ya mwamba mmoja huyu ndani anaitwa UMUGHAKA ....hafu kama umenifumbua macho....huyu jamaa kama anatunga kupitia mule mule alopitia umughaka
Achana na Monica, hata kama kwenye hiyo story mnayoisema angekuwa Veronika vile vile, bado isingekuwa proof ya kusema ninamkopi mtu. Onyesha sehemu gani nimecopy?Hiyo simulizi inaitwa "tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe", ni ya UMUGHAKA hiyo na yule mwanamke wa Umughaka alikuwa anaitwa Monica, siyo Veronica
Hazifanani. Leta hapa huo mfanano tuoneShukrani sana! Zinafanana kwa kiasi fulani
mkuu achana na hawa wapuuzi..hawa ni wale ambao hawasomagi stories humu, kama wangekua wafuatiliaji kweli wasingekuja na shombo zao hizo,, kwamaana kila kitu kiko wazi...Achana na Monica, hata kama kwenye hiyo story mnayoisema angekuwa Veronika vile vile, bado isingekuwa proof ya kusema ninamkopi mtu. Onyesha sehemu gani nimecopy?
Kwani majina ya watu siku hizi hayafanani?
yani limtu limo humu kitambo,lakini linashindwa kutofautisha story...umekazana tu imekopiwa sijui zinafanana,,zinafanana nyoko....Shukrani sana! Zinafanana kwa kiasi fulani
Enyi wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga.Mimi nimeishtukia tokea mwanzo Veronica,Yunge na Tatu[emoji23]
Poa mkuu.mkuu achana na hawa wapuuzi..hawa ni wale ambao hawasomagi stories humu, kama wangekua wafuatiliaji kweli wasingekuja na shombo zao hizo,, kwamaana kila kitu kiko wazi...
Inavutia sanaNimeamua kushare hapa hiki kisa cha kweli kilichonitokea kwenye maisha yangu. Nikiamini wengi mtajifunza na kuburudika pia.
NB: Majina ya watu na baadhi ya Majina ya sehemu yatakuwa sio halisi ili kuficha indetity yangu. Pia sio mwandishi mzuri Ila nitajitahidi kuandika kwa mtiririko mzuri.
Naitwa Mr the dragon ni mzaliwa wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara. Nilizaliwa katika hospitali ya Bunda district designated hospital (DDH) katikati ya miaka ya tisini, yaani miezi sita kabla ya kifo cha 2pac na miezi miwili kabla ya kuzama kwa Mv Bukoba. Ukiwa pale ilipo Crdb bank kwa sasa ndio maeneo niliyozaliwa.
Nikiwa ndio kwanza nina umri wa miaka mitano. Baba yangu mzazi aliugua kichaa, namaanisha alianza kupata uwendawazimu ikabidi apelekwe kwa waganga wa kienyeji. Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara aliyejulikana vizuri mitaa hiyo. Japo baadae alikuja kupona, lakini mpaka sasa imebaki ni kitendawili juu ya chanzo cha ugonjwa ule wa akili. Inasemekana ni mkakati maalumu ulioandaliwa na baadhi ya wafanyabiashara wenzake ukitaka wafanyabiashara wote waliovuka rubana warudi kwao. Mkakati huu ulihusisha imani za kishirikina, wafanyabiashara baadhi waliovuka mto rubana kuja bunda walipoteza maisha. INASEMEKANA LAKINI!!!
Mhenga aliyesema mwanaume ni kichwa cha familia hakukosea. Baada ya baba kuugua mambo yote yaliharibika maisha yalituchapa kwelikweli. Ikabidi mama achukue familia kurudisha nyumbani kwao, yaani kwa Babu yetu mzaa mama. Nyumbani kwao na mama ni mkoa wa Simiyu wilaya ya Busega kijiji cha Mwanono (Sio jina halisi). Mimi na kaka zangu na dada zangu tukaanza kuishi kwa Babu, kipindi hicho nina miaka minane nikiwa darasa la pili.
Babu yangu aliitwa mzee Manumbu alikuwa very prominent pale kijijini. Kijana wake wa kiume yaani mjomba wetu (kaka mama mmoja na mama yangu) alikuwa na cheo kikubwa serikalini. Alimjengea babu nyumba nzuri kijiji kizima, alimnunulia ng'ombe wengi na trekta jambo lililomfanya kuwa miongoni mwa matajiri wa kile Kijiji. Babu yangu alikuwa na wake sita walioishi sehemu moja, jambo lililofanya awe na familia kubwa sana. Watoto wake na wajukuu tulikuwa wengi sana tulioishi pale.Mabinti wa Kijiji kile na vijiji jirani walitamani kuolewa kwa mzee Manumbu.
Nakumbuka mwaka uliofuata 2005 nikiwa darasa la tatu siku moja mama yangu alialika kikundi cha watu wa kulima. Kwa jina maarufu kwa kisukuma huitwa "Luganda". Alialika hicho kikundi wakamlimie palizi ya pamba. Kikundi hiki kilitumia zeze na ngoma pindi wakiwa wanalima ili kupandisha mzuka watu wasichoke wakiwa wanalima. Muda wa usiku nikiwa nimelala nilisikia sauti ya ngoma na vifijo nje ya nyumba. Nilifikiri ni wale wa kikundi wamekuja kuwapitia watu wa nyumbani waende shamba. Nilikurupuka kutoka nje ili nikawaone wanavyocheza.
Nilifungua mlango nikiwa na shauku kubwa. Nilipofungua niliona kundi kubwa la wanawake na wanaume wanaimba na kucheza katikati ya uwanja wa pale nyumbani wengine wakiwa uchi, wengine wamevaa nguo nyeusi. Kwanza nilipigwa na butwaa na kujikuta nikikaza jicho langu kuangalia wanavyocheza. Baadae ndipo wazo la kwamba wale ni wachawi ndio lilikuja akilini, nikatimua mbio kurudi ndani nikajifunika shuka gubigubi. Cha ajabu niliporudi ndani tu zile ngoma zilikoma, niliogopa sana japo sikufanikiwa kumtambua yeyote katika kundi lile.
Kesho niliamka mapema ili niwahi kuhesabu namba shuleni, lakini nilisikia maumivu kwa mbali kwenye mguu. Kuangalia nikaona nilikuwa na kidonda mguuni japo sio kikubwa Sana. Nilijiuliza nimepata wapi hicho kidonda lakini sikupata jibu. Nikikumbuka hata jana yake usiku sikujigonga wala kujikwaa popote wakati nakimbia. Niliogopa sana lakini sikuwa na jinsi niliendelea na kunawa miguu na uso niende shule. Wakati tukiwa tunatoka kwenda shule mimi na ndugu wengine tulisikia taarifa mbaya. Mjomba wetu (kaka wa mama tofauti na mama yangu) aliyekuwa anakaa pale nyumbani alikuwa amechanjwa Chale mgongo mzima. Niliogopa sana nikawa natamani kusimulia nilichokiona usiku, ila kila nikijaribu napata uoga sana... Sikuzungumza chochote
Baadae tulienda shule, siku hiyo sikuwa na raha kabisa ukizingatia matukio yaliyotokea nyumbani. Kikubwa zaidi kilichoniogopesha ni hiki kidonda ambacho sikujua kimetokea wapi. Wakati nikiwa darasani binti mmoja tuliyekuwa tunasoma nae darasa moja alinifata, binti huyu bibi yake alikuwa ni mchawi aliyeogopeka zaidi pale kijijini. Ujio wake haukunishangaza kwa sababu nilimchukulia kama ndugu yangu, na mara nyingi tulikuwa tunapiga story. Nilimchukulia kama ndugu kwa sababu kaka wa huyo bibi yake alikuwa ni rafiki mkubwa wa baba yangu mzazi. Hata bibi yake yaani mchawi aliyeogopeka nilikuwa nikimuita shangazi. Alipofika aliniambia
" Mr the dragon kumbe ni muoga vile, nilikuona usiku ulivyokimbia kurudi ndani. Sisi tulienda kwenye mkwaju wa kwa lugota kula nyama"
Mkwaju wa kwa Lugota ulikuwa ni mti wa ukwaju mkubwa na mnene sana uliokuwepo pale kijijini.
Nilimuangalia tu nikakaa kimya, sikuzipendelea story zake kwa sababu nilikuwa naogopa sana.
Itaendea kesho...