Kisa cha ''magaidi'' wawili: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege

Abuu Dharr,
Nashukuru.

Jina lako ni la Kiislam kwa hiyo nakuchukulia hivyo.
Umeninasihi mimi niusome Uislam.

Maana yake ni kuwa umenipima na umeniona mimi ni mjinga wa dini yangu.
Nakuchukulia kuwa wewe una elimu kubwa ya dini ya kuweza kuwapima Waislam wenzako.

Sawa.
Lakini nakusoma naona umetumia lugha ya ''Sheikh Ponda na genge lake.''

Sheikh Ponda Issa Ponda kiongoziwa Shura ya Maimam kwako anaongoza ''genge.''

Subhanallah.
Haya si mafunzo ya Uislam.

Lakini wewe umejiaminisha kuwa una elimu kubwa ya Uislam kiasi cha kutoa nasaha kwangu.

Umewasema vibaya Ikhwan.

Unaijua vyema historia ya Hassan Banna?

Haya si mafunzo ya Uislam kushambuliana.

Mashambulizi yako mbona umeyaelekeza sipo?

Mtazame Sheikh Chambuso vyema katika picha hii ya mwaka wa 2006 yuko ndani ya darasa anagawa mashafu kwa wanafunzi wake wengine aliwasomesha udogoni alif kwa kijiti.

Unajua wakati anafanya haya alikuwa na umri gani?

Muangalie vizuri katika hii picha:



Huu kwako ndiyo ushabiki?

Kafungua shule ya chekechea anasomesha watoto wadogo Qur'an na lugha ya Kiarabu.

Kafungua shule ya ushoni kwa watoto wa kike wajifunze kushona wajiajiri.

Haya kwako ni ushabiki?

Ahmada anapita katika majumba ya Waislam anawahamasisha wachangie fedha wajenge hosptali.

Hospitali inajengwa na Waislam wamehamasika wanatoa michango kazi inafanyika.

Haya kweli ni ya kumuudhi Muislam?

Umejinasibu kwa Uislam nami sina sababu ya kukutilia shaka.

Allah ndiye mjuzi na yeye ndiye Hakimu Muadilifu.
 
Kambi ya mafunzo ya ugaidi, kama ile ya Mtwara na Lindi.
Lihakanga,
Ikiwa kweli hizo kambi zipo hilo ni jambo ovu sana.

Kwa nini hawa watu hawakamatwi na kushitakiwa mahakamani kesi zikasemwa na wakaadhibiwa kwa mujibu wa sheria?
 
nimwalimu wangu wadini akat nasoma mkwakwani secondary.
tulikua nasomo ladini lakin shule haikua namwalimu hata mmoja kwamiaka yote 4 niliosoma hapo.
hao mabwana walikua wakihangaika karbia shule zote kubwa zatanga mjin kwakufundisha vipind vi 4 kwawiki kwakila shule. kwetu ilikua nijumatatu na alhamis

waliweza kututengenezea umoja nakwaushauri wao tukapata tuition nyingi zilizoanzishwa kwenye madrasa namisikitini zikawazinafundisha masomo ya sayansi nabiashara tukifundishwa nawanafunzi ambao wako advance. tuliweza kuchagua ma amir tukaweza kusimamia mambo yetu yakiimani tukiwa shule mpaka tukafikia kupewa jengo tufanyie mskiti nakupewa break yadakika 20 kilaikifika saa 7 ili kufanya ibada.

waliweza kutulea nakutupa msingi mkubwa sana kiiman ambao nimsaada mpaka Leo kwetu. tumepata ndugu wazuri mabrother waliojengwa kiimani haswa ambao hatashida zakifamilia zikitupata leo tunaelekea kwao.
 
Find...
Allah akujaze kheri.
 
Shekau (kwa kiingereza)
Shekau was born in Shekau town, in Tarmuwa local government, Yobe State;[citation needed] his exact date of birth is unknown but is said to be between 1965 and 1975. Shekau was an ethnic Kanuri, and also spoke Hausa, Fulani, Arabic, and English.[12] In 1990 he moved to the Mafoni area in Maiduguri and studied under a traditional cleric before entering the Borno College of Legal and Islamic Studies (now called Mohammed Goni College of Legal and Islamic Studies). Shekau left the college for ideological reasons and without earning a degree.[13] He later met Mohammed Yusuf, the founder of Jamaat Ahlus Sunnah li Dawah wal Jihad, and became one of his deputies. Shekau was appointed the leader of the group in July 2009, after the death of Yusuf in the 2009 Boko Haram uprising. Shekau survived being shot in the leg during the 2009 attempt on his life by Nigerian security forces.[3] He was married to one of Muhammad Yusuf's four widows.[14] His nickname was “Darul Tawheed”, which translates as "specialist in tawheed", the Islamic concept of oneness of Allah.[14]

Mwanzo wa Sheau(kwa kiswahili)
Shekau alizaliwa katika mji wa Shekau, mtaa wa Tarmuwa, Jimbo la Yobe, tarehe yake halisi ya kuzaliwa haijulikani lakini inasemekana ni kati ya 1965 na 1975. Shekau alikuwa kabila la Kanuri, na pia alizungumza Kihausa, Kifulani, Kiarabu na Kiingereza. Mnamo 1990 alihamia eneo la Mafoni huko Maiduguri na akasoma chini ya mkufunzi wa jadi kabla ya kuingia Chuo cha Mafunzo ya Sheria za Kiislamu cha Borno (sasa kinaitwa Chuo cha Mafunzo ya Sheria na Uislamu cha Mohammed Goni). Shekau aliondoka chuo kikuu kwa sababu za kiitikadi na bila kupata digrii. [13] Baadaye alikutana na Mohammed Yusuf, mwanzilishi wa Jamaat Ahlus Sunnah li Dawah wal Jihad, na kuwa mmoja wa manaibu wake. Shekau aliteuliwa kuwa kiongozi wa kikundi hicho mnamo Julai 2009, baada ya kifo cha Yusuf katika ghasia za Boko Haram za 2009. Shekau alinusurika na kupigwa risasi ya mguu wakati wa jaribio la 2009 la kumuua na vikosi vya usalama vya Nigeria. [3] Alimuoa mmoja wa wajane wanne wa Muhammad Yusuf. [14] Jina lake la utani lilikuwa "Darul Tawheed", ambalo linatafsiriwa kama "mtaalamu wa tawheed", dhana ya Kiislam ya umoja wa Allah. [14]

Nimetanguliza habari fupi ya huyo bwana ili walau kupata picha fupi.

Kama inavyotarajiwa mara zote Mzee Saidi ni utatetea kwa kuchagua upande kwa jambo lolote linalohusishwa na imani yako ya kiislamu.

Sidhani kama hilo litakuacha kwenye heshima ya kutambulika kama Mchambuzi makini wa mambo.

Ni bahati mbaya kwamba kuna mstari mwembamba sana kati ya kuwa Mwanaharakati wa imani ya Kiislamu na kuwa Mfuasi wa itikadi kali za Kiislamu. Na sioni yeyote wa kumtupia lawama hapa zaidi ya Wahusika wenyewe kujitizama upya namna ya kuendesha shughuli zenu za kiimani na mafundisho.

Hivi ni ushauri gani uliwahi kuutoa kwa Serikali ili kupambana na "Majambazi" waliokuwa wanaua Watu hovyo pale Tanga au Kibiti?. Au yaliyokuwa yanatokea kule sio matukio halisi ni stori tu?. na je hujaridhika na kilichofanyika kurejesha usalama wa Wananchi wa kule?.

Juzi nimemsikia Mtangazaji mmoja akilalama kwamba Ugaidi unashereheshwa na Uislamu...hivi ni nani wa kumlaumu kwa hilo?. kina Shekau au Jamii ya kitaifa na kimataifa? . Hata wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela aliitwa Gaidi, Waasi wa Msumbiji wa wakati ule 1970's tuliwaita "Magaidi wa Msumbiji" na wala halikuwa suala la kidini.

Hebu muanze kupitia aina ya Mafunzo mnayoyatoa kwa Wana imani wenu, maana kwa sehemu kubwa mafunzo yenu yanahimiza kutowajali wale wasio na imani kama yenu. Hivi utategemea matokeo gani kwa kuandaa kizazi cha aina hiyo kwenye Jamii yenye Watu wenye mchanganyiko wa kiimani?.

Kwa Wasifu wote uliotoa kuhusu hao Mabwana hakika inaleta maswali, haswa kwa wakati huu tulionao....ni jambo la kheri kama wanahubiri yaliyo mema na kuhimiza Jamii kupendana na kuheshimiana lakini pia itakuwa ni uzembe kwa Mamlaka kukaa tu pembeni na kuwaamini kwa 100% kwamba wanafanya kila kitu sawa.

Kwa wewe kuwa karibu nao haitoshi kuiaminisha Jamii yote ya mamilioni ya Watanzania kuwa hao Watu ni Wema na waaminiwe tu.
 
May Day,
Umeandika mambo mengi.
Kueleza ugaidi kwengineko ukaleta mifano hiyo Tanzania ni kosa kubwa sana.

Mimi naandika kama Muislam na najitahidi kueleza mambo kama niyajuavyo.

Tatizo la hili tatizo la ugaidi ni kuwa mahakama haijaweza kupelekewa ushahidi kuwezesha kuendesha kesi.

Hili lingewezekana hayo yote ya Kibiti na kwengineko yangefahamika na wahusika kutiwa hatiani.
 
Kuhusu ushahidi sitaki kuamini kama hufahamu ugumu wa kupata ushahidi kwenye mambo kama haya.....mambo yanayohusiana na vitisho, adhabu kali na hata ya kuuwawa Mtu na familia yake nzima na imani kwa upande mwingine ni ngumu Mtu kuthubutu kujitokeza kutoa ushahidi?.

kesi hizi nyingi zitaishia hewani tu ingawa matokeo yataonekana kama tunavyoona usalama ulivyorejeshwa kwa ndugu zetu wa Tanga, Kibiti n.k....Serikali ingezubaa kwa kujibweteka kwenye kivuli cha "ushahidi" leo hii tungekuwa tunaongea mengine.

Sioni tatizo kufananisha mambo ya nje na hapa kwetu maana sisi hatupo kwenye kisiwa.

Kutoa mifano ya kina Mzee Mandela ni kujaribu tu kusema kwamba kumbe sio lazima Ugaidi kufungamanishwa na Uislamu tu.
 

Haya maandishi yako mbona kama yana mambo mengine ya ziada? Wanaomuhoji unadhani wote walikuwa hawaitambui Quran? Umetumia kigezi gani kusema hivyo? Maana jinai ni suala moja na kuonewa ni jingine kabisa. Na sio kila anayekuhoji ana shida na kitabu kitakatifu.
Matendo yetu ndio yatatuhukumu. Hata kama ni muumini kiasi gani, kama matendo yanakinzana na mafundisho ya dini au yanaongezwa mbwembwe ili kuhalalisha mambo ambayo sio halali ni makosa makubwa sana. Lazima tutapata tabu sana. naogopa sana watu wanaotumia dini kuhalalisha uhalifu wao
 
Hitler alikuwa Muislamu?Aliyeporomosha amkombora ya nyuklia Hiroshima alikuwa Muislamu?Musolini alikuwa Muislamu?Kaburu wa Africa kusini alikuwa Muislamu?
 
Ndio nimeongea mengi lakini nimeitahidi kuzungukia kwenye hizo hizo hoja ulizozileta.

Nimezungumzia aina ya mafundisho maana unasema tu kuwa walikuwa wanatoa mafundisho ya Kiislamu kwa kujitolea waipate thawabu, sawa lakini ni nani ana hakiki kila wanachokifundisha?.

Mara nyingi Mtu Mwanaharakati awaye yote sio lazima wa kiimani, huwa ni mwepesi sana kujiongeza kwa mafunzo yake anayoyaamini yeye.
 
Naomba radhi Sheikh wangu Mohammad Said
Bahati nzuri,Mimi ni Mzawa wa Tanga na hawa kina Chambuso,nawajua vilivyo...kujenga Shule au kufundisha Cherehani..hizi zote ni kazi za Kijamii...si kazi labda ukisoma ndio umemjua Allah....Laa Hasha

Naomba samahani sana kama nimekukwaza kwa kauli yangu susuavu

Ila sisi kama Waislam,tunahitaji kusoma Dini yetu na tunahitaji Wasome wa Dini na si wana Harakati

Shukran sana
Allah akubaarik popote ulipo
 
Ni chuki ya Kanisa Katoliki pamoja Na baadhi ya wakristo dhidi ya uislamu Na waislamu

Chuki ya kanisa katoliki? Kivip? Ndugu kikulacho ki nguoni mwako. Ukaanza kuhimiza uuaji utakamatwa. Ukianza kuhimiza uvunjaji sheria utakamatwa.
Tena watakukamata watu wa dini yako, amini usiamini. Ukatoliki toka lini unaogopa uislamu? Ukatoliki unaogopa mambo mengine makubwa ambayo yanalitafuna kanisa kutokea ndani. Haliogopi mtutu wa bunduki wala siasa za chuki.
 
Hii post umeweka ilivyotakiwa . Dini sio kuwa mwanaharakati. Dini sio ya kutafutia sifa na ukubwa.
 
Kuna mambi mengi na makubwa yamejificha nyuma ya pazia...
 

Tulia na usome vizuri hii habari

Yaani watu wanamiliki AK 47 na kimya husikii kuitwa gaidi. Hivi tuambie hii kesi ilienda vipi ??


PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA
 
boss mim nimmoja kati yawaliofundishwa nahuyo jamaa. alikua yeye natimu yake wakisfundisha shule zaid ya 5 kwakujitolea bure, shule yetu pekee ilikua namkondo A-H kwakila darasa. mim bunafsi nilfanikiwa kufanya mitihani ya necta ya elimu ya dini kwakufundishwa nahao jamaa pekeake bila kufundishwa namwalimu mwengine yoyote.

jamaa katulea kama mzazi kabisa, alifanya ikawa ikifikia kipindi chalikizo wanafunzi wake aliowafundisha waliopo vyuoni wakirudi tanga tunapata tuition yabure.
niliwahi kwenda kusoma TIA ya mbeya kwamsaada wandugu yangu nilipofika hapo college sikua namwenyeji nanilikua namazingira magum sana kiuchumi bahat Nzuri nilkutana najamaa ambae alikua nimmoja wawanafunzi wake yeye Ndo alikua mwaka wamwisho. nilimfata nkajitambulisha kua nilishawai kumuona na ustadhi chambuso kwenye kipindi chadini. jamaa alinikarim nakunisaidia sana kma nnaundugu naye vile.

walikua namoyo wakutusaidia tupate miongozo mzuri wamaisha wadini naelimu ya dunia. jamaa nimfano wakuigwa hakukua nabaya lolote kwenye mafundisho yake
 
Niseme ukweli siamini kama haya mambo yanafanyika Tanzania. Kuna umuhimu wa waislamu kuunda taasisi zao nje ya hizi akina BAKWATA ambazo zitaeka mikakati ya kutetea haki za waislamu nchini.

Njia za kujihami ziko nyingi baadhi:
  1. Kutoa misaada ya kisheria kwa waislamu
  2. Kuendesha kampeni za boycot na kuwawajibisha wabunge wasirudi bungeni kwa kushiriki kupitisha sheria mbovu. Hizi zote zimepita na wabunge wako wanasinzia tuu kwenye vyombo vya sheria.
  3. Kupigania mabadiliko ya sheria kandamizi kama hizi za ugaidi (kwa nilivyofahamu sheria imependekezwa na wamarekani/waizrael).
  4. Mikakati ya kukuza vipato vya waislamu, wengi wanaweza wasifahamu lakini kipato kinasaidia kutatua mambo mengi tuliyonayo duniani.
Kitu kimoja hadi leo kinaniacha mdomo wazi, ni vipi mtu anaweza kukamatwa bila ya ushahidi ? Halafu anasota gerezani watu wakisema wanatafuta ushahidi au upelelezi haujakamilika ? Kivipi raia mnyonge au sheikh anaweza kuzuia upepelezi wapolisi wakati akiwa nje ya gereza ?

Nadhani sheria zinatakiwa zisitoe mwanya kiasi hiki, hakuna ushahidi ndani ya siku 1-2 polisi wanalazimika kisheria kumwachia mtu. Hii inaongeza pia creativity ya jeshi la polisi. Maana kwa wale wahalifu inawabidi wafanye kazi kwa bidii/weledi kuweza kufanikisha, na kwa upande mwengine inaokoa wanyonge kusota magerezani bila ya sababu ya msingi. Hawa watu wanaosota gerezani wanakula na kulala kwa fedha za walipa kodi!

Sababu za kiusalama miaka takriban 9 hatukuona mabomu wala vita ya kigaidi, badala yake DPP anasema ameshindwa kuendelea na kesi. Isitoshe kisheria pia muathirika hawezi kudai fidia!

Asante sana Sheikh Mohammed kwa makala.

Maasalaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…