Katika harakati za kusaka maisha Mganda, Mkenya na Mtanzania wakajikuta mikononi mwa dola huko Uchina, kosa likiwa kukutwa na madawa ya kulevya.
Kama mnavyojua Uchina ukishatiwa mbaroni wewe ni KIFO tu hakuna adhabu nyingine.
Basi wote watatu wakaambiwa kuchagua MOJA kupigwa risasi papo hapo ya kichwa au kupatiwa adhabu nyingine ambayo nayo inaendana na ya kifo ila unaweza ukaponyoka ukiwa na bahati.
Wote watatu wakachagua ile ya pili - Basi wakapelekwa kwenye msitu wakaambiwa kila mmoja kwa njia yake aende na akirudi awe na matunda 10 anayoyaona kayapenda, yoyote yale.
Wakaenda bwana, wa kwanza kurudi alikuwa Mganda, karudi na machungwa 10, adhabu yake akaambiwa ameze yote bila kutafuna akimaliza atakuwa huru - akameza la kwanza, la pili akashindwa - akapigwa risasi akafa.
Wa Pii akaja Mkenya, yeye alikuja na vitunda 10 kama amri ilivyosema vilikuwa mfano wa pilipili hivi...akaambiwa ameze vyote bila kutafuna na akimaliza yupo huru.. Kwa sababu ni vidogo akameza cha kwanza hadi nane ile anameza cha tisa tu akaanza kucheka sana sana kiasi cha kushindwa kumeza kile cha mwisho - kwa kosa hilo akapigwa risasi akafa hapo hapo.
KUZIMU:
Walipofika kuzimu Mganda na Mkenya, yule Mganda akaamuuliza kulikoni wewe, umeshindwa kumeza cha mwisho wakati vyako vilikuwa vidogo vidogo...
Mkenya akasita kidogo kisha akasema, si kwamba nilishindwa kumeza ila nilishindwa kujizuia kicheko....
Mganda akamuuza kwa nini ukashindwa kujizuia kicheko?
Mkenya akamjibu: NILIMWONA MTANZANIA AKIJA NA MATIKITI MAJI.