Kisa cha Mkuu wa Mkoa Rwegasira kuondoa makahaba Dar es Salaam

Kisa cha Mkuu wa Mkoa Rwegasira kuondoa makahaba Dar es Salaam

issue sio isifanyike bali ifanyike kwa utaratibu maalum usioleta bughudha kwa jamii nyingine hasa watoto..
 
Ndo tujiulize kwa ukamilifu wake, je umalaya tunawezaje kuuderive hadi ukawa dhambi.

Mimi kigezo changu cha kitu kuwa dhambi ni mtu mwingine aumizwe na matendo ya mtu mwingine. Yaani dhambi ni kitendo cha kimakusudi kumuumiza mtu mwingine, tena haswaa yule aliyekuamini na kutegemea mema toka kwako.

Saaa hapaa, malaya amedai pesa na amelipwa. Mteja amedai ngono na amepewa tujiulize ni nani kamtenda mwenzie!!?
Dhambi ni kutenda kinyume na maagizo ya Mungu, ni kutenda mambo yasiyompendeza Mungu, ni kutenda mambo yasiyo mema.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nchi ikichafuka rais anaweza kwenda kujificha sehemu za makahaba, na akatoboa.
 
Dhambi ni kutenda kinyume na maagizo ya Mungu, ni kutenda mambo yasiyompendeza Mungu, ni kutenda mambo yasiyo mema.
Hakika, nami nakubaliana na hilo.

Agizo la Mungu ni upendo. Sie majirani tutendeane kwa wema kama tuu ambavyo tungependa kutendewa. Kwa hiyo kufanya jambo limuumizalo mtu mwingine ni dhambi maana ni kinyume na upendo.

Malaya na mteja wake wametenda kipi ambacho hawangependa watendwe? Nani kaumia? Nani kaumizwa? Nani kamuumiza mwenzake?

Tumeambiwa leo kuwa sheria za mungu zimegawanyika sehemu mbili tu;
1,2,3 Mpende Mungu
4-10 mpende jirani kama nafsi yako.
ILa masadukayo walizifafanua hadi zikafika 613. Na ndio maana yezu alipokuja akaweka sawa kwa kusema kimsingi kuna kanuni moja tu, akaigawa vipande viwili. Tafakari
 
Wanavunja amri ya sita ya Mungu - usizini.
 
Wanavunja amri ya sita ya Mungu - usizini.
Usizini nakubali usizini.

Lakini sio kila tendo la mume na mke kukutana ni kuzini ndio maana kuna wanaokutana na wanazaa katika ndoa yao safi kabisa.

Mke akimdanganya mumewe akatoka nje ya ndoa. Anazini na anamuumiza mumewe waliyeahidiana kiapo cha uaminifu.
Vivyo hivyo mume
Vivyo hivyo mpenzi wa mtu. Usimdanganye mwenzio yupo peke ake halafu ukaenda kulala na mtu mwingine ni dhambi.

Je watu wawili (malaya na mteja wake) wasio na mikataba wala maagano kwingine wanapokutana wamemuumiza nani? Wamevunja ahadi kwa nani?
 
Uzinzi ni nini?
 
Uzinzi ni nini?
Kwa taratibu na sheria? ... au ki roho?

Kwa sheria za kisadukayo kuna mengi na yanaweza kuwa dhambi kweli au yasiwe dhambi bali makubaliano tu ya kibinadamu.

Lakini ki roho ni kuweka nadhiri sehemu moja kuwa nitafanya hivi halafu kwenda kufanya kinyume na nadhiri hiyo sehemu nyingine. Huo ni uzinzi.

Mfano 1. Mke kusema nitamtii mwanaume huyu katika haya. Halafu akaenda kumtii mwanaume mwingine katika yaleyale.
Mfano 2. Muumini kuahidi atamtumikia Mungu halafu akaenda kuitumikia miungu mingine etc etc
 
MWALIMU NYERERE ALIMZUIA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA KUWAONDOA MAKAHABA JIJINI DAR
Tanzania imepitia simulizi nyingi zenye kusisismua lakini nyingi zikiwa hazisemwi sana kwenye vyombo vya habari na hivyo kupelekea vizazi vya sasa na vijavyo kutokujua mengi yaliyowahi kutokea na kuleta changamoto kubwa kwa baadhi ya viongozi serikalini, sambamba na kutekeleza mambo yao mbalimbali.

Mnamo mwaka 1980, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar wakati huo, Balozi Joseph Rwegasira alianzisha Operesheni maalum ya kuhakikisha Makahaba wote waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza miili ndani ya Jiji hilo kuondoka haraka, sambamba na kutumia nguvu kuwaondoa wale wote ambao wangekaidi amri hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa imelenga kuwarudisha Makahaba waliopo Dar makwao, ili wakaendeleze kazi ya kulijenga taifa kupitia shughuli zao nyingine kama kilimo, ufugaji nk, na hivyo kuweza kusaidia kuimarisha vijiji vya ujamaa wakati wa Mpango wa Taifa wa kuiimarisha na kuendeleza Vijiji vya Ujamaa maarufu kama "Operesheni Vijiji".

Kufuatia uamuzi huo wa Balozi Rwegasira, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu Balozi Rwegasira, akitaka aende akamfafanulie kuhusu utaratibu na madhumuni ya Operesheni ile.

Alipofika Ikulu, kauli ya kwanza ya Mwalimu ilimtumainisha kuwa huenda Operesheni yake iliungwa mkono pale alipohoji, “Nasikia umeamua kuwahamisha mama zangu warudi makwao wakalime maharagwe!” Rwegasira alijibu haraka kwa kusema, “Unajua Mwalimu, hatua yangu hii ni kutekeleza kaulimbiu yetu ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa Letu", na Operesheni ya "Kilimo cha Kufa na Kupona" pengine hata kaulimbiu ya awali tuliyoiita, "Siasa ni Kilimo", ndipo nikaiona ni muafaka kabisa.

Hapo ndipo hoja ya Mwalimu iliyofuatia ilimshtua Rwegasira, pale aliposema, “Nimekuita unieleweshe ni watu wa aina gani ulioteua warudishwe makwao kwa utekelezaji huo, pia nataka kujua utaratibu unaotumika”.

Ndipo Baba wa Taifa aliishia kuhoji, “Kwa hiyo umewahukumu kwa ukahaba wao, au kuna sababu nyingine?” Hapo, Rwegasira alikaa kimya kwa kutokuwa na jibu muafaka! Hata hivyo, Baba wa Taifa aliendelea kudadisi kwa kuhoji, “Ikiwa umeamua kuwatimua makahaba, je, mazingira ya kule utakakowahamisha, umeyaandaaje?”

Kwa kuwa hoja ya Baba wa Taifa ilikuja kinyume na matarajio ya Rwegasira, isitoshe hakuelewa mwelekeo wa hoja ile, alibaki kimya, ndipo Mwalimu alimuamuru kwa kusema, “Ukiweza kutimiza hilo, njoo unieleze nibariki Operesheni yako!”

Aliongeza kwa kusema, “Kama usingekuwa mtani wangu wito wangu ungeishia hapa, lakini hebu nikufafanulie chanzo cha ukahaba, ndipo aliuliza iwapo Rwegasira anafahamu wateja wa makahaba ni kina nani, akawa amejibu kuwa ni wanaume! Mwalimu alicheka akamuuliza, “Wewe si mwanaume, je, huko waliko makahaba unakwenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana!”

Mwalimu akahoji tena, “Mimi si mwanaume, je, huko naenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana Mwalimu!” Ndipo alianza kumchambulia kuanzia wanaume wasiojua kumtaka mapenzi mwanamke, wasiotaka bughudha ya kutunza familia hivyo hawaoi, hata waliobarikiwa nguvu nyingi za mwili wakienda huko kuzipunguza ili wasisumbue wake zao.

Na hapo ndipo Mwalimu alifafanua hoja yake kwa Rwegasira akisema, “Nilipotaka nijue mazingira ya huko utakakowaondoa umeyaandaje, nilijua hao wateja wao wasipowakuta, matokeo ni kubakwa mama zetu, wake zetu, wanafunzi wetu, vilema wetu, hata vichaa wetu! Ndiyo maana katika miji yote duniani makahaba wapo!“

Mwalimu alimalizia kwa kumwambia Rwegasira ya kuwa, hata mataifa yaliyojigamba kuwa na utawala bora na wa sheria, yalishindwa kubuni sheria ya kutawala miili ya watu hususani wanawake hivyo kudhibiti ukahaba, pia michezo hatari kama ndondi na kareti, ikaishia kuhalalisha biashara zinazohusisha ukahaba kwa namna moja au nyingine, tena zikitozwa kodi ya mapato kwa Serikali.

Hatimaye Mwalimu alitaja kuhusishwa kwa ukahaba katika Maandiko Matakatifu, ambapo makahaba hawakuhukumiwa kwa ukahaba wao, isipokuwa walihimizwa wawe na matendo mema, sawa na walivyohimizwa watu wengine.

Alitoa mfano wa kahaba aliyemkimbilia Yesu alipokimbizwa na umati uliotaka wamponde mawe mpaka afe kama mila yao inavyoruhusu. Yesu aliuambia ule umati akisema, “Ikiwa miongoni mwenu kuna asiyepata kutenda mnalomtuhumu nalo, na awe wa kwanza kumtupia jiwe.

”Yesu alishusha macho kuendelea kuchora kielelezo chake, na alipoinua macho sekunde kadhaa baadaye, hakuona mtu hata mmoja! Ndipo alimuamuru yule kahaba akisema, “Inuka uende zako, kawe na matendo mema.“

Mwalimu alimhoji Rwegasira akisema, “Kwani Yesu alishindwa kumtamkia kahaba aache ukahaba?” Hapo ndipo Mwalimu alimtaja kahaba mwingine aliyemkuta Yesu mahali akifanyiwa karamu akamuangukia akilia, mpaka alimlowesha miguu na kumpangusa kwa nywele zake, akampaka manukato! Yesu alimuambia mwenyeji wake akisema: “Huyu mwanamke amekuzidi, kwa kuniosha miguu kama ilivyo desturi yetu, ambapo wewe hukufanya vile.“

Kwa msingi huu, Mwalimu alimtamkia Balozi Joseph Rwegasira akisema: “Kwa kupewa akili na Mwenyezi Mungu, mwanadamu hatahukumiwa kwa dhambi ya mwenziwe, ndipo kwa hali hiyo, litatimilika agizo la Mwenyezi Mungu kuwa, "Usihukumu mwenzio, ndipo nawe hutahukumiwa."

Credit to JamiiForums:
Kule nilikoipata
we ulikuwepo hapo ofisini kwa mwl. Nyerere wakati hayo yanatendeka? Upumbavu mwingine uwe unaona haya. Ni zuzu gani ataelewa huu upupu wako?
 
Kwa taratibu na sheria? ... au ki roho?

Kwa sheria za kisadukayo kuna mengi na yanaweza kuwa dhambi kweli au yasiwe dhambi bali makubaliano tu ya kibinadamu.

Lakini ki roho ni kuweka nadhiri sehemu moja kuwa nitafanya hivi halafu kwenda kufanya kinyume na nadhiri hiyo sehemu nyingine. Huo ni uzinzi.

Mfano 1. Mke kusema nitamtii mwanaume huyu katika haya. Halafu akaenda kumtii mwanaume mwingine katika yaleyale.
Mfano 2. Muumini kuahidi atamtumikia Mungu halafu akaenda kuitumikia miungu mingine etc etc
Hebu kajifunze kwanza maana ya dhambi na ujielimishe maana, mfanano na tofauti ya ngono, uasherati, ukahaba na uzinzi ndiposa uje tujadiliane. Kila la kheri.
 
we ulikuwepo hapo ofisini kwa mwl. Nyerere wakati hayo yanatendeka? Upumbavu mwingine uwe unaona haya. Ni zuzu gani ataelewa huu upupu wako?
Ulivyonitukana, imekusaidia Nini?
 
Sijawahi kuona mtu aliyefanikiwa kuondoa hiyo biashara.

Viongozi wetu ni wavivu tu kufikiri.

Wanaacha mambo ya msingi na kurukia vitu visivyokua ni matatizo katika jamii zetu.

Watu wanahitaji afya elimu bora ajira na uchumi wa kueleweka.

Maji yenyewe ya uhakika hatuna

Waache usanii bwana.
 
Hakika, nami nakubaliana na hilo.

Agizo la Mungu ni upendo. Sie majirani tutendeane kwa wema kama tuu ambavyo tungependa kutendewa. Kwa hiyo kufanya jambo limuumizalo mtu mwingine ni dhambi maana ni kinyume na upendo.

Malaya na mteja wake wametenda kipi ambacho hawangependa watendwe? Nani kaumia? Nani kaumizwa? Nani kamuumiza mwenzake?

Tumeambiwa leo kuwa sheria za mungu zimegawanyika sehemu mbili tu;
1,2,3 Mpende Mungu
4-10 mpende jirani kama nafsi yako.
ILa masadukayo walizifafanua hadi zikafika 613. Na ndio maana yezu alipokuja akaweka sawa kwa kusema kimsingi kuna kanuni moja tu, akaigawa vipande viwili. Tafakari
Vp mashoga au wasagaji wakiridhiana ...nayo sio zambi?
 
Makahaba wapo kitambo sana na wana wateja wao wanaowezana nao. Wengine mikriti ya makahaba hatuiwezi kwa kuwa ni watu wa slow motion
 
Back
Top Bottom