Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Wakati tunasoma shule alikuwepo mtoto mmoja baba yake alikuwa Shehe.
Mtoto yule Kuna siku aligombana na sisi wanafunzi wenzake wote bwenini.
Kwa bahati mbaya Sana alitutishia kwamba baba yake ni Shehe na anafuga majini hivyo usiku atakuja kwa njia ya paka akiwa Kama jini.
Basi sisi tulilala kwa kujihami sana tukijua leo kazi ipo.
Kwabahati mbaya sana usiku ule akaja paka bwenini na kama mjuavyo shule nyingi za bording mapaka ni mengi kwa sababu kuna misosi ya bwerere.
Hakika tulitaka kumuua yule mtoto wa Shehe pona yake ilikuwa ni walinzi waliwahi kuja bwenini vinginevyo angekufa siku hiyo na maafa yangekuwa makubwa.
Maskini ya Mungu mtoto wawatu Wala familia yao haina Mambo yoyote ya kishirikina na baba yake ni Shehe kweli ila mwislam Safi mzee yule rafiki yake na mzee Benjamin William Mkapa.
Mdomo ulitaka kumponza mtoto yule kwa kututishia kwamba atakuja usiku bwenini kama jini kwa sura ya paka ili tukione cha mtema kuni.
Sasa kitendo cha mzee Bulembo Mama Rwakatare Ndugai na wabunge wa CCM kutaka Zitto auwawe ni kucheza na Moto kama ule wa mtoto wa Shehe.
Mdomo huumba muombeeni sana Zitto abaki kuwa salama vinginevyo mnaweza kuta jumba bovu linawaangukia nyie in case ZITTO akidhurika. (Kuna Mambo yanatokea coincidentally) mfano unamtishia mtu ajali kwa utani na kweli anapata ajali ujue Hilo linakuhusu huchomoki lakini pia Kuna maadui wanaweza kutembelea kauli zenu kweli watamdhuru victim ili tu jumba bovu liwaangukie kumbe maskini mliongea kimuhemko.
Jitafakarini sana hasa Mama Rwakatare mchungaji.