Kisa cha Prof. Khigoma Malima na Sheikh Mavumbi, Uchaguzi wa 1995

Kisa cha Prof. Khigoma Malima na Sheikh Mavumbi, Uchaguzi wa 1995

Ok kumbe wewe ndio mkewe
Bujibuji,
Hapana haja ya lugha kali tufanyeni mjadala wa kiungwana.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Alishukuru kisha akafariki na siku ya mazishi yake hapakuwa na msikiti wowote uliokuwa na nafasi ya kumsalia sala ya jeneza ikaamuliwa jeneza lake likasaliwe Viwanja Vya Mnazi Mmoja.

Hii ilikuwa haijapata kutokea.

Baada ya sala mwanae Adam Malima alipanda jukwaani na akaeleza jinsi baba yake alivyofariki.

Maziko ya Prof. Malima hayajapata kutokea hadi hii leo.
 
bujibuji kama una chuk na mtu sema ila usimsem mayti vibaya.watu wengin kama wa kheri shaur yako utaj kufa kifo kibaya weweulimi ufike mpaka magoti.nini chuki yako kwa almarhum.?
 
Mzee MS
Hadithi yako haijakaa Vizuri hata kidogo
Naamini uliandika ukiwana haraka
Tafadhali fanya hima uhariri kazi yako
Uzalendo,
Hapana huwa sina haraka katika kuandika na sababu ni kuwa mengi yamo katika Maktaba yangu hivyo huwa suala la kutalii napata ninachotafuta.

Juu ya haya kazi yoyote ya mikono ya binadamu lazima itakuwa na kasoro.

Kama umeliona kosa nifahamishe nisahihishe kwani siwezi kujihariri mwenyewe.
 
KUMBUKUMBU ZA PROF. KIGHOMA MALIMA NA SHEIKH IBRAHIM MAVUMBI WA TABORA UCHAGUZI WA 1995

Radio ya gari yangu siku zote wakati wote ninapokuwa naendesha kituo changu ninachosikiliza ni TBC Taifa.

Leo ile kuwasha gari tu namsikia mtangazaji TBC Taifa anatangaza mkutano wa Kampeni ya CCM Tabora Viwanja Vya Ali Hassan Mwinyi na anasema kuwa Sheikh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi atapanda jukwaani kusoma dua.

Mashaallah kama kuna kitu masheikh wetu wanakiweza kwa ufanisi wa hali ya juu ni kusoma dua katika shughuli za kitaifa.

Kwa hakika katika eneo hili wanastahili pongezi kutoka kwetu sote.

Mtangazaji anamtaja Sheikh Ibrahim Mavumbi Sheikh wa Mkoa wa Tabora kuwa anapanda jukwaani kusoma dua kabla ya mkutano wa kampeni ya CCM.

Jina hili la Sheikh Mavumbi kwangu ni maarufu.

Ghafla na kwa kasi kubwa jina la Sheikh Ibraim Mavumbi likanirudisha miaka 25 nyuma wakati kama huu wa uchaguzi mkuu wa vyama vingi mwaka wa 1995 ndani ya msikiti mkuu wa Ijumaa Tabora magazeti yalipoandika kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya msikiti wa Tabora baada ya sala ya Ijumaa.

Wahariri wa magazeti takriban yote ukilitoa Annuur gazeti la Waislam, walikuwa wanachuki kubwa na Prof. Malima na kila wakinyanyua kalamu zao ilikuwa ni kumwandika vibaya Prof. Malima.

Magazeti ya siku hiyo yote yalikuwa yametawaliwa na habari za Prof. Malima kujitoa CCM Msikiti wa Ijumaa Tabora.

Waingereza wanamsemo wanasema, ‘’They had a field day,’’ hii maana yake ni kunufaika bila kutoa jasho na kuhangaika.

Magazeti walikuwa wamekipata walichokuwa wanakitafuta tena wamekipata kwa bei hafifu sana.

Kufika saa tano msikiti umejaa pomoni na nje watu wametandika misala Waislam wameitika taarifa za magazeti wamejitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Prof. Malima akijitoa CCM ndani ya msikiti wao wa Gongoni.

Haukupita muda gari ya polisi ikasimama mbele ya msikiti akashuka Sheikh Ibrahim Mavumbi na kuingia ndani ya msikiti.

Sheikh Ibrahim Mavumbi alikuwa Sheikh wa BAKWATA.

Siku ile nje ya msikiti askari wenye unifomu na wengine makachero walikuwa wametanda kuzunguka msikiti na wengine wakiranda mitaa ya jirani achilia mbali makachero waliokuwa ndani ya msikiti wenyewe.

Sheikh Mavumbi akaenda mbele kibla akachukua kipaza sauti akawatangazia Waislam kuwa Prof. Malima asiruhusiwe kuzungumza siasa ndani ya msikiti.

Waswahili tuna msemo, ‘’Hukuweko lakini malaika wako alikuwako.’’

Sheikh Mavumbi ile kulitaja tu jina la Prof. Malima msikiti wote ulilipuka kwa hamaki.

Kila mtu akisema lake.

Kwa kipindi kifupi pakawa na fujo na vurugu kubwa Waislam wameghadhibika pasi na kiasi.

Katikati ya kelele zile ikasikika sauti ya upole na sauti maarufu kwa wengi na hakuna asiyeijua sauti ile.

Ilikuwa sauti ya wito ikisema kwa upole, ‘’Salaa Nabi,’’ ‘’Msalieni Mtume.’’

Hakuna Muislama asiyejua maana ya wito huu kila aliyesikia maneno yale aliitika kwa Sala ya Mtume wakijibu, ‘’Allahu Maswali Wasalimaale.’’

Ghafla utulivu ukarejea msikitini ikawa ukiangisha pini utasikia kishindo cha kuanguka kwake.

Sauti ile ilikuwa sauti ya Mzee Bilal Rehani Waikela.

Muasisiwa TANU, mpigania uhuru wa Tanganyika na mtumishi wa Waislam toka ujana wake hadi pale sasa kawa mtu mzima.

Mzee Waikela akachukua kipaza sauti kutoka mikononi mwa Sheikh Mavumbi huku kamwelekea Sheikh Mavumbi akamuuliza, ’’Sheikh Mavumbi wewe nani kakuambia kuwa Prof. Malima atakuja hapa msikitini kufanya siasa?

Hebu angalia hapa.

Unamuona Prof. Malima humu msikitini?’’

Sheikh Ibrahim Mavumbi kinywa kikawa kimemjaa mate.

Anaangaza kote hamuoni Prof. Malima.

Hana la kusema.

Hakuweza kumtaja aliyemtuma kuja msikitini wala hakumuona Prof. Malima ndani ya msikiti.

Taratibu kwa unyonge akageuka kuelekea mlango wa msikiti na kutoka nje kwenda kupanda gari ya polisi iliyomleta pale msikitini kwa vishindo vya kumwaga vumbi.

Nimefurahi sana kuona kuwa Sheikh Ibrahim Mavumbi baada ya robo karne bado kashikilia nafasi yake ile ya Sheikh wa BAKWATA Tabora.

Hakika hii inaonyesha na ushahidi wa kuaminiwa kwake katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa kweli Sheikh Ibrahim Mavumbi ni kiongozi wa kuigwa katika kuweza kuwatumikia Waislam wa Tabora kwa miaka yote hii na bila shaka kwa ufanisi mkubwa.
Kisa nakikumbuka na nilikuwepo nilikua bado mvulana wa makamo ya elimu ya juu ya sekondari katika shule ya Uyui

Bahati mbaya Mavumbi ulimtaja alikwisha fariki aliyepo sasa ni mwanae

Ni kweli Mzee Bilali waikela aliongea na moja ya kauli aliyoitoa ambayo ilikaririwa katika ndimi za waislamu waliokua wapinzani wakubwa wa BAKWATA

Ni pale aliposema :

" ... sio tu kuchanganya dini na siasa bali tutaikoroga dini na siasa ..."

Nakumbuka ulikua mzozo mkubwa sana wakati huo, miongoni mwa watu maaru ninao wakumbuka kwa upande wa polisi operation hiyo ilikua chini OC CID Ndg. Chaka na rafikie mkubwa Kamanda Mohamed Chiko

Tabora iliwaka moto, na chama alichokua ikihamia Mareham Kighoma Malima kilikuwa kinaitwa NRA au NAREA nimesahau kirefu chake, wakati huo chama hicho pamoja na CUF vilihusishwa sana na udini

Ahsante kwa history hiyo!!!
 
Jina maarufu sana hili! Lakini kama ni Imamu inakuwaje anatajwatajwa kama mganga? Ni maarufu kwa hili la ulozi pia!
Alikuwa Mganga wa kiislam. Huo uganga wake aliokuwa akiufanya kwa kweli hakufaa kuwa na Kiongozi wa kidini. Alikuwa kama mchawi fulani.
 
Back
Top Bottom