Kisa cha Tabora kuwa nyuma kielimu

Nicotompa

Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
66
Reaction score
13
Habari zenu wanajukwaa,

Naomba kwa ufupi sana nibainishe sababu kadhaa zinazochangia kushukaa kwa kiwango cha elimu katika mkoa wa Tabora,kwanza mazingira magumu kutokana na jiografia ya mkoa ulivyo,pili uhaba wa walimu na vifaa vya kufundishia kutokana na idadi kubwa ya walimu kuhama mkoa kwa kukimbia mazingira magumu,tatu tafiti zinaonesha 70% ya watumishi {walimu} wanaishi na mishahara chini ya 50000/=kutokana na madeni kuwa mengi,lakini wapo wengine hawana mishahara hata kidogo na wapo kazini...nne mwamko mdogo wa kielimu mkoani humo maana yasemekana wapo wazazi ambao huwajenga watoto kutofanya vizuri kwenye masomo....itaendelea.
 
Ni kwa sababu ya kuwa na shule nyingi then wanaosoma shule hizo ni wageni kutoka nje ya mkoa wa Tabora
 
Ukitakaa majibu ya maswahali haya kichwani kisha fanya utafiti kuhusu elimu ya tabora

1.profesa ibrahim lipumba amesoma wapi na mtu wa wapi....
2.profesa juma kapuya ni mtu wa wapi na elimu yake allipata wapi
3.dkt.kitila nkumbo wa udsm mtu wa wapi na alisomea wapi
4.dkt.saanane john from d.i.t.....mtu wapi na elimu yake aliipata wapi
5.dkt.kigwangala from
6.dkt kafumu from
7.dkt.harrison mwakiembe
8.ismail aden rage...
9.profesa erick masesa from udsm
10.samweli sita minister
11.magreth sitta
12.jaji joseph sinde warioba
13.jaji mkuu othumani chandee

na wengine wote elimu yao wallipata wapi,na wazawa wa wapi ndo uje na majibu na wadhifa gani nchini halafu ndo post....
 

Huna hata sababu moja ya msingi,na pengine nikuombe usipende kuelezea kitu usichokijua. Hii itakupelekea kuwapotosha watu na kuupoteza ukweli.
Kumbuka mara baada ya mwalimu Julius Nyerere kumaliza elimu ya msingi huko Musoma aliletwa Tabora kuendelea na elimu ya sekondari. Inamaanisha wazi kuwa kipindi hicho elimu ilikuwa ikipatikana sehemu chache tu katika Afrika ya Mashariki,Tabora ikiwemo. Sina imani kama mkoa wako ulikuwemo kwenye orodha hiyo.
Pili,juhudi za kudai uhuru zilifanikisha Tabora,baada ya mikoa mingine kusita kuunga mkono. Ni wazi kuwa kudai haki hakuji tu kama mvua,bali ni juhudi zinazotokana na uelewa.
Tatu, shule za vipaji maalum zilizopo Tabora ni ishara tosha kuwa mkoa una historia ya elimu.
Nakushauri kusoma historia sahihi ili uache ubabaishaji.
 
aisee akili yako bado changa sana umemwelewa mtoa mada kweli
 
Ni kwa sababu ya kuwa na shule nyingi then wanaosoma shule hizo ni wageni kutoka nje ya mkoa wa Tabora

Hnja hii ina ukweli usiopingika. Shule zilizopo Tabora hazina manufaa kwa wana-Tabora bali kwa watu wanaotoka nje. Na hili halipo kwa bahati mbaya bali limewekwa kwa makusudi.
 
Kinachowasumbua ni zao la tumbaku tuuuu.hivyo.vingine ni vijisababu tu.

Utakuwa umesemea uchumi. Any way,tuseme uchumi mbovu ndiyo kisababishi kikubwa cha elimu kukosekana. Nakubali,lakini huu utakuwa ni mpango maalumu wa maadui wa mkoa huu.
Mimi nasema maadui hawa waliondoa kwanza elimu ndipo uchumi ukaharibika kabisa.
Hapo nyuma Tabora palikuwa na uzalishaji wa karanga na mpunga na sasa hakuna. Wakulima sasa wanaamini kuwa tumbaku peke yake ndi njia ya uchumi,bila kujali hata hiyo tumbaku hawana mamlaka nayo.
Zingatia:leo tabora iku nyuma kwa kila kitu. Elimu,uchumi,miundombinu na hata maadili,vyote ni vibovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…