Kisa cha "Trojan Nuclear Plant" na elimu ya Usimamizi wa Miradi (Project Management)

Kisa cha "Trojan Nuclear Plant" na elimu ya Usimamizi wa Miradi (Project Management)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
1545227866426.png

Ilikuwa ni mwaka 2000 mbele ya umati wa watu nchini Marekani; Ndugu John Lackey akishangiliwa baada ya kupewa TUZO (Reward for Best Project Management of a Utility Plant in the United State), hakuwa akiamini kama juhudi zake siku moja zingekuja kumjengea heshima kubwa kiasi hiki nchini Marekani.

John Lackey alipewa "task" ya kuondosha kinu cha nuclear (Trojan Nuclear Plant Decommission), ambacho kilikuwa karibu na makazi ya watu, na matumizi yake yalikuwa yamefika ukomo, hivyo kupelekea kuleta hatari kwa afya na ustawi wa jamii ya maeneo ya jirani. Kijuujuu ilionekana kama kazi rahisi, ila kiuhalisia si kazi rahisi hata kidogo. Trojan Nuclear Plant, ilichukua ukubwa sawa na uwanja wa mpira, na namna ya kuiharibu ilibidi kutoa "component" moja baada ya nyingine tena kwa uangalifu mkubwa ili kuepusha "leakage" ya sumu ambayo ingeleta madhara kwa binadamu.

Ili kufanikisha kazi hii, Mr John ali-consider the assignment as a project, hivyo akaanza mchakato kwa ku-design PROJECT MANAGEMENT TRAINING kwa watendaji wa kampuni. Mafunzo haya yaliweza kugusa maeneo mbalimbali katika Usimamizi wa Miradi, kama vile; Cost Management, Scope Management, Time Management, Risk Management n.k

Changamoto kubwa aliyokutana nayo Mr John, ni katika kubadili fikra (Mind-Set) ya watu katika kampuni kutoka kuwa OPERATIONS BASED COMPANY, na kwenda kwenye PROJECT BASED COMPANY. Kwa msaada wa mafunzo, hatimaye watendaji katika kampuni waliweza kubadili fikra zao, na kuanza kufanya kazi katika utaratibu wa ki-miradi, na hatimaye MRADI ukaisha kwa mafanikio makubwa ambayo yalimpatia Mr John heshima kubwa.

KAMPUNI YA KI-MRADI (PROJECT-BASED ORGANIZATION)
Hii ni aina ya kampuni ambayo hufanya shughuli zake kwa kufuata misingi ya miradi; kwa maana ya kwamba, shughuli yoyote (ya kutengeneza bidhaa/kutoa huduma)huchukuliwa kama ni mradi, hivyo inapaswa kuwa na muda maalum wa kuanza na kumaliza, kuwa na malengo na kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa, kuwa na bajeti maalum, pia kuwa na timu ya watendaji maalum (timu hii hujumuisha wawakilishi kutoka kila idara ya kampuni) ambao wataongozwa na mtu mmoja tu (Project Manager), na si wakuu wa idara walizotoka.

Miaka ya 1960, kampuni nyingi ulimwenguni zilijikita kwenye uzalishaji zaidi (Mass Production),miaka ya 1970, kampuni hizi zilihama muelekeo na kujikita katika ubora (striving for quality).Miaka ya 1980, uelekeo ukahama tena kutokana na mahitaji ya wateja, kipindi hiki kampuni zikajikita katika aina/upekee wa bidaa dhidi ya washindani wao (variety), miaka ya 1990, muelekeo ukahama kwa mara nyingine na kwenda kwenye upya wa bidhaa (novelty), mteja hakutaka tena kuuziwa bidhaa (same product) inayofanana na ile aliyonunua miaka ya nyuma. NA SASA muelekeo umebadilika na kuhamia katika utendaji wa bidhaa (functionality), leo hii mteja haihitaji simu kwa ajili ya kupiga na kupokea simu tu (Make a Call), bali anahitaji simu kwa ajili ya kusikiliza muziki, kuangalia video, ku-surf internet, kusoma na kutuma barua pepe, kuandaa nyaraka, kusoma vitabu n.k. Hivyo kampuni nyingi sasa hazina budi kubadilika na kuendanda na mahitaji ya soko. Ni kupitia misingi ya "Project Management" kampuni itaweza kuja na bidhaa/huduma bora yenye kiwango kinachokidhi mahitaji ya mteja wa leo. Katika kulitekeleza hili, kampuni nyingi sasa katika nyanja mbalimbali kama vile "Telecommunication, Engineering, Construction etc" zinatumia kanuni za Miradi katika uzalishaji.

FAIDA YA KUENDESHA KAMPUNI KATIKA UTARATIBU WAKI-MIRADI
  • Huwezesha kujenga timu ya kiutendaji iliyo madhubuti
  • Husaidia kumaliza/kufanya uzalishaji wa bidhaa au huduma kwa wakati na kwa ubora stahili
  • Inachochea ubunifu kutokana na mchanganyiko wa watu kutoka idara mbalimbali za kampuni
  • Hupunguza gharama za uzalishaji, kwa sababu kabla ya kufanyika kwa mradi, makisio ya ghrama hufanyika kwanza.
  • Huisaidia kampuni hususani katika kipindi cha mtikisiko (turbulance),

The Consult; +255 719 518 367
E-mail ; [email protected]
Dar es Salaam

Tanzania
 
Makala nzuri ingawa hakukua hâta na umuhimu wa kusimulia hicho kisa
 
Back
Top Bottom