Kisa cha wezi walioiba benki

Kisa cha wezi walioiba benki

Kwekitui

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
1,070
Reaction score
1,083
Wakati wa Uvamizi wa Benkii nchini fulaniii majambazi waliwaambia kwa sauti watu waliopo Mule benki "Musisogeee hata kidogo maana Pesa ni mali za serikali ila uhai wako ni ni mali yako "

Basi kila mtu alilala chini kwa haraka na kila mmoja alikaaa kimya Hii inaitwa " KUMBADILISHA MTU AKILI " badili fikra za watu ili Ufanikiwe.

Wakati wamelala kuna mwanamke mmoja alilala kwa mitego yaan Nguo yake Aliipandisha Juu Jambazi akafoka kwa sautii " Lala vizuri hatujaja Kubaka Tumekuja Kuiba "

Hii inaitwa " KUWA PROFESSIONAL" yaani Focus kazi iliokuleta sio unaangaika na mambo mengne.

Wakati wamerudii nyumbani Kulikuwa na jambazi Mdogo akamwambia Jambazi mkubwa kuwa "Tuhesabu pesa Tujue ni kiasi gani Tumepata "

Yule Mkubwa akasema " Acha ujinga Wewe Tumeiba pesa nyingi mnoo tukihesabu hapa tutachukua mda mrefu wewe tulia Tuangalie taarifa ya habari watasema n kiasi gani kimeibiwa "

Hii inaitwa "EXPERIENCE " siku izi kuwa na experience ni muhimu Sana kuliko Vyeti vyako vyenye A nyingiiii

wakati wezi wameondoka meneja wa benki alimwambia Supervisor " Tupige simu polisi haraka lkn yule Supervisor akasema " Tulia Ngoja tuibe na sie million 800 Alafu ndo tupige simu polisi "

Hii inaitwa " HOGEREA KWENYE MAWIMBI " yaani badili hali usioipenda kuwa Faida kwako

Supervisor akasema " n vizuri wezi wakawa wanakuja kutuvamia kila mwezi "

Hii inaitwa " KUUA UCHOVU " Furaha yako n muhimu kuliko kazi unayoifanya

Siku inayofata Taarifa ya habari ilitangaza kuwa Bilioni 1 zimeibiwa na wezi kwenye benki wale wezi walienda kuhesabu pesa walizoiba zaidi ya Mara 10 wakakuta Million 200 Tu kila wakihesabu inakuja milioni 200

Wale wezi wakafoka kwa hasira " yaani tumehatarisha maisha yetu Tumeiba million 200 tu wao wameiba million 800 tena bila ya kuvuja jasho kwa kweli Elimu ya kitu unachokifanya bora kuliko kufanya kazi bila elimu yeyote "

Hii inaitwa " THAMANI YA ELIMU NI SAWA NA THAMANI YA DHAHABU "
KUMBUKA ELIMU HAIPATIKANII SHULENI TU ...


Mwisho
FB_IMG_1612675472000~2.jpg
 
Back
Top Bottom