Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kule kwetu siku za nyuma, nyumba ilijengwa nyuma ikiwa na pori dogo. pori hili lilikuwa mahsusi kwa kujisaidia wanawake, wagonjwa, wazee na watoto.
pia mbali ya nyumba, umbali kama kilometa nne kulikuwa na pori kubwa sana, hili lilitumika na vijana pamoja na kina baba wenye nguvu kujisaidia.
Vijana walikuwa wakishindana mbio, wanajikusanya wengi kama wako kwenye marathon, kisha inahesabiwa mpaka tatu, mbio zinaanza kuelekea porini.
Wale waliokuwa wanakuwa wa mwisho kila siku kwnye mashimbano, walipewa ruhusa maalum ya kujisaidia kwenye pori dogo la nyuma ya nyumba.
Timu ya Yanga ni timu imara na kubwa sana hapa nyumbani, lakini kamwe haitakuja kufanya vyema kwenye michuano mikubwa ya kimataifa kwasababu ya roho ambayo Yanga inayo. (Falsafa).
Ukiangalia logo yao imejaa ghiriba tupu. Kuna bondia, Yanga haina timu ya masumbwi, kuna mcheza netiboli, Yanga haina timu ya netiboli. Pia kuna mwenge. Huu ndio kiashiria kikubwa cha roho inayoimaliza Yanga, mwenge hauvuki nje ya mipaka yetu. Mwenge ni wa humuhumu tu, ukitoka kijiji hiki, utaenda kijiji cha pili, tarafa na wilaya kisha mkoa mmoja baada ya mwingine.
Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Yanga, ila kwa kweli bila Yanga kubadili logo, na kubadili mipango yake ya maendeleo, maono na mbinu za mpira wa kisasa, kamwe haitakuja kufanikiwa.
Pia Yanga iache kujiona yenyewe ni sehemu ya jumuiya za CCM, iachane kabisa na mambo ya mwenge.