Kisa cha Zakayo mtoza ushuru na Mwigulu Nchemba kwa ufupi

Kisa cha Zakayo mtoza ushuru na Mwigulu Nchemba kwa ufupi

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Zakayo kwa Kiebrania Zakai(msafi,mnyoofu) alikua mkuu wa watoza ushuru na tajiri, alipata kibali cha kutoza kodi na mapato na kiasi kilichozidi alikiingiza mifukoni mwake. Aliishi maisha ya kifahari na kuponda mali. Zakayo alimsaliti Mungu na taifa lake .

Wakati Yesu anaingia Yeriko, Zakayo alipanda kwenye mti ili aweze kumwona kutokana na wingi wa watu, ila Yesu alimfuata na kumuamuru ashuke. Zakayo hakua na amani na maisha aliyokua anaishi.

Zakayo anasema, "tazama bwana, nusu ya mali zangu nawapa maskini na kumrudia Mungu." Hivyo hivyo kwa Mwigulu Nchemba, umetusaliti wananchi kwa tamaa za kodi na mapato, ni muda sahihi wa kuwarudia wananchii.
 

Attachments

  • 01.jpg
    01.jpg
    55.8 KB · Views: 4
  • 1-3.jpg
    1-3.jpg
    14.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom