Kuna kipindi nilikuwa ninahisi maumivu kwenye jino la mwisho, nikaenda hospitalini kupiga xray ikaonekana nina jino chini ya fizi, inabidi litolewe.
Nikaweka appointment ili niende kesho yake kulitoa.
Asubuhi na mapema nikawahi hospitalini, Daktari nilekutana nae ni kijana mdogo mwenye rika la 24 hadi 25 na nilijua ni mwanafunzi, mwalimu wake ambae ni daktari tulieonana jana yake alikuwa anampa maelekezo fanya hii fanya vile.
Kosa la kwanza kabisa alilokosea ni kuweka kiwango kidogo cha dawa ya ganzi, kwakweli nilikuwa napata maumivu makali sana, ilibidi mwalimu wake aweke tena.
Zoezi likafika la kung'oa jino anavuta vuta bila mpangilio ikabidi mwalimu wake aje kutoa jino lakini mpaka leo jino linalofuatia ni kama limechimbika, nikitafuna kitu kigumu kama mfupa ukifikia hapo huwa kuna maumivu, nyama huwa najitahidi kutafuna isifike huko.
Shughuli ilivyokamilika mwalimu wake akamwambia aniandikiea dawa za kutuliza maumivu bila kumuelekeza labda alimuamini ataweza bila kusimamiwa, nilienda kununua dawa hizo lakini hazikuwa za kutuliza maumivu.
Nililia chumbani na utu uzima wangu kwa maumivu niliyokuwa napata, niliongeza dozi lakini wapi
Maumivu yalikuwa makali uvumilivu ulinishinda, Nikaenda duka la dawa kuulizia kama dawa nazotumia ni za maumivu, wakaniambia ni vidonge vya tonsils sio maumivu, ilibidi ninunue vya kutuliza maumivu ndio niliweza kupata nafuu.