Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Watu wote pale hamna aliyekuwa anajua kwann tunaitwa na tulivokusanyika tukambiwa tukae chini ndo maafande wakaja na majina ya waliochana magodoro na sisi tuliochana uniform ndo tukajumuishwa na pia hamna aliyekuwa anajua kwamba tungeenda kusulubiwa na mijeledi siku kama ile ya kumaliza shule[emoji23][emoji23]Oya sasa kwanini hukutimua mlivyoitwa na maafande?
Ulihofia nini tena kama mitihani ulishamaliza?
Sisi tulikuwa tunaogopa kufukuzwa shule tu lakini baada ya mitihani walimu ndio walikuwa wanatembea watatu watatu kuepuka kichapo cha revenge katika miaka minne yote waliyotutesa
At my early 20's, siku moja nilikuwa na ugwadu sana so nikaenda pale Manzese kwa malaya.
Kwa mbali nikamuona mmoja amenona sanaaa, kutokana na zile taa zao sikuweza muona vizuri.
So nikaingia moja kwa moja ndani, hapo ndipo nilipoduwaa.
Aisee ni mama mtu mzima sana rika hata la mama yangu mzazi. Kwa kweli nilifanya ile sex hata utamu sikuusikia, mawazo yalikuwa mbali sana.
Nikajua njaa mbaya sana. Niliumia mno kwa bibi yule kufanya biashara ya namna ile.
Huwa naumia sana mpaka leo hii nikikumbuka ga hili suala.
Aiseeh haichoshi kujifunza. Elimu Dunia!Wakati bado nipo chuo kabla ya msala wa Receipt fake.. ilikua ni mwaka wa pili kama sikosei sem ya pili..
Hii story kama mhusika yuko humu JF atanijua rasmi mimi ni nani. Ila hakuna shida, cha kuogopa ni kifo pekee na bado kidgo kingenikuta!
Jamaa yangu mmoja nilikua naishi naye hostel nje kidgo ya chuo. Yeye kama ilivyo mimi hatukuwa na mkopo, na kwao hawakua vizuri kama ilivyo kwetu. Sema yeye alikua mtoto wa mjini kushinda mimi na alikua ameniacha parefu ki umri. Sema kuna vitabia flani hivi huwa vinafanya watu wanakua marafiki. Kwa namna yeye na mimi tulivyokua, ungeweza kutuita wazee wa michongo katika rejesta za kileo.
Kwa vile tulikua tunakaa room moja, vitu vingi kuhusu mimi vilikua wazi. Sina hela. Nimefulia. Sikua hata na confidence ya kusimamisha mwanamke nimtongoze. Akitaka tutoke out nitampeleka wapi? Kwa hela ipi? Kwaiyo nikawa ni mtu wa kutulia sana ndani na kuishi kikamilifu ndani ya ratiba za chuo na hostel. So unaweza ku imagine vile maisha yangu yalikua Boring!
Siku moja wakati tunapiga story za hapa na pale na jamaa akaniambia kuna mchongo wa siri anataka kunishirikisha. Nikatega sikio vizuri. Akaniambia kuna jamaa anamjua tukimpa kiasi fulani halali anaweza kututumia hadi mara nne yake ya bandia. Kwaiyo sisi kazi yetu ni kutafuta changes tu ili tupate za halali.
Duh, wakati ananiambia mimi natetemeka. Nikamwambia mwanangu hii issue si inaweza ikatufanya tufungwe kabisa? Akaniambia "Ufungwe na nani?" .. "Tulia nikuoneshe", na mimi nikatulia.
Jamaa akaagiza mzigo, ukafika. Ilikua kama Mil 1 hivi ya Bandia. Nikamuona kwenye zile pande mbili za kuwekea hela kwenye Wallets; upande mmoja kaweka pesa halali kama 30K, na upande mwingine kaweka bandia kama 100K (Laki). Kaoga kamaliza, huyoooo kasepa!
Alikua ni mtu wa viwanja sana, sikumsikia wakati anarudi usiku. Kwaiyo kesho yake ahsubui namuona kakaa kwenye angle ya kitanda anahesabu hela, Duh. Ni kaki na buku be za kutosha. Mshenzi kashikisha watu zaidi ya elf 90 za bandia. Kabaki na 10 tu. Mimi tamaa ikawa imeanza kugonga mlango, nikawa sitaki kuifungulia. Unajua ukiwa umefulia sana vishawishi ni rahisi sana kukuzidi nguvu. Nikaendelea kujikaza huku jamaa yangu anazidi kuagiza mizigo na anapiga hela vibaya mno.
Mimi nampiga tu vi mizinga vya hapa na pale mwisho wa siku nikajikuta na mimi kanigawia fungu la kuchekecha. Ilikua kama laki 5. Laki 4 bandia, laki 1 halali.
Kama uko viwanja pesa za kwanza unatoa halali, halafu unatafuta mhudum mmoja mwenye tamaa unampiga vi ofa vya Beer huku ukiandaa mazingira ya yeye kukuhudumia tu. Akianza kuchangamka unamsukumia hizo noti mdogo mdogo kama hatasanuka ndio imeisha hiyo. Kazi inakua imebaki kuhesabu changes nikifika hostel.
Shetani ni mjanja sana. Huwa anakulinda ukiwa unaanza halafu baadae anakutelekeza ukisha kolea. Ndio kilichonikuta mimi, sikumaliza hata mwezi kwenye huo mchongo. Mungu huyu ni wa kumshukuru sana! Nisingekua naandika huu uzi hapa saivi.
Kuna mahali nilikuja kusoma kuwa "Katika magendo yoyote yale, daima epuka kuwafanyia watu wenye hali za chini kwa sababu ina create a very bad luck". Na ndio kilichoniponza, kwa sababu nilikua desperate sana kupata hela haraka haraka nikaanza kuwafanyia hako ka mchezo mpaka boda boda na dereva taxi. Eh bhana eeh. Kumbe walikua wakifika sheli wanakataliwa pesa zao, wengine mpaka wanaitiwa polisi mimi sijui.
Wakawa wamejipanga siku wakimkamata huyo anayetoa pesa za bandia wanamuua. Mimi sikua nafahamu, nilikuja kugundua baadae huko. Sasa kuna boda wawili ambao nilikua napenda sana kuwatumia katika mishe zangu ambao nilikua nawapa pesa halali, hao ndio walikuja kuniokoa siku nimebananishwa nataka kumalizwa.
Siku yenyewe ilikua hivi. Mida ya jioni nimetoka zangu misele nikapita kijiwe kimoja kipya cha toyo nika scan sura za wajomba nikamuona mmoja kama boya boya hivi nikamchagua anipeleke maeneo karibu na Hostel (Huwa napenda kushukia kwa nyuma kidgo). Sasa kosa la kwanza, sikuwa na pesa ya halali hata moja kwenye wallet.
Sijui ilikuaje nikatumia zote huko nilipotoka halafu sikukagua kabla sijapanda boda. Ile nimeshuka si nikampa jamaa ten. Akaanza kuikagua akakuta ni bandia, akanikwida shati faster. Akasema wewe ndio tulikua tunakutafuta. Nikawa nabishana naye pale kwani vipi, kama ni bandia huenda hata mimi nimeshikishwa nikatoa wallet nikachomoa ten nyingine kumpatia alivyoicheck nayo ni bandia. Mama yangu!
Akapigia simu washkaji wa kijiweni na wao wakapigiana simu na wengine wakajaa pale. Mimi najifanys sielewi nimepanick najisachi kila mahali. Akaja jamaa mmoja akasema huyu mnamuhoji wa nini nikapigwa kofi moja la maana mpka nikajikuta niko chini. Nikaanza kulia kwa huruma. Wahuni wengine wanasema litafutwe tairi nichomwe. Ghafla mmoja kati ya wale jamaa naowatumiaga mara nyingi akawa na yeye amefika eneo la tukio. Hapo nimesha shikwa shikwa sana mpaka shati limechanika. Sura yangu imeanza kufanana kabisa na ya mwizi. Moyoni mwangu nimeshakubali kuwa leo ndio mwisho wangu!
Jamaa kuniona si ndio akawambia mbona huyu ni mwanafunzi wa chuo namchukuaga sana. Boda wengine wakakataa kata kata kuwa hakuna huyu ni jambazi hakuna kutetea. Wengine wakataka ninyang'anywe pochi waangalie ID. Ndio wakaona kweli mimi ni mwanafunzi. Hapo nimeshalia nimechoka, nawambia mimi sio mwizi jamani, mtaniua bure tu, nawaelewesha kuwa nilikua na shida nikaamua kuuza simu yangu ya kupangusa nahisi wale jamaa niliyowauzia ndio wamenifanyia huo mchezo hata mimi sielewi kama ni bandia.
Wakanichukua wakanipeleka kituo kidgo cha polisi hakikua sana mbali na pale. Nikaandika maelezo yangu na wao wakaandika maelezo yao. Sikumaliza hata siku tatu jamaa yangu akaja na wenzake wawili kuniwekea dhamana. Mambo yalikuja kuisha lakini baada ya hilo tukio na jamaa yangu akaachana na hayo mambo kabisa.
Bado nakumbuka vile nilikua najuta na kusali kule kituoni. Kumbe kufa ni kitu kidogo sana. Nikasema nikitoka hapa naenda nyumba za ibada kutoa sadaka ya shukrani. Washkaji walivyoisikia issue yangu, waliniambia nina bahati sana. Lazima kuna kusudi la Mungu katika maisha yangu ndio maana nimeponea tundu la sindano.
Lol .poleMengi mengi mengi ....mengi mnooo....ila kubwa kuliko ni kumwamini mwanaume....na sitokoma kujuta coz bado ni mwepesi sana kumwamini mtu mapema
Duuh mkuu funguka kidogo [emoji30][emoji30]INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] what went wrong nigga !?Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,
Wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,
Weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
Pole Sana tupe full package mkuuMi najuta kuwa na huyu niliye naye nilijua naondoa upweke kumbe naongeza maumivu
Ngoja nilee tu Hawa watotoView attachment 2166015
[emoji16][emoji849][emoji849][emoji849]Bora ungekua mtungo[emoji1787][emoji1787]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119]Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six
Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa
Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa, tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza
Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)
Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)
Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea
Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani
Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana
Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform
Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika
Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)
Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa
Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji24][emoji24][emoji20]Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja hivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja.
Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....
I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako.
Kifo ni fumbo kubwa.
Tuwajali Sana wanaotupenda, life is too short.
Story za kweli mwisho page ya 10..Uzi ulianza vizuri saivi naona chai zinaanza
Aiseee [emoji849][emoji20][emoji20][emoji20][emoji16]Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.
Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.
Speak it out hata kwa I'd nyingine tupo hapa kwaajili ya kujifunza jamani msitunyime elimukiukweli kuna mtu najuta mno kumfanya rafiki, sina wa kumsimulia kisa changu maana hii siri nitakufa nayo mwenyewe, lakini najuta mno kumfanya rafiki na sina namna ya kumuacha na kumuweka mbali lakini pia sina namna ya kumkimbia..
Mola wangu wa mbinguni nisamehe mimi siyapendi haya na yananigharimu mno kwenye maisha yangu..
AiseeSio amenipeleka mpaka sasa niko kwenye majanga na sijui yataisha lini kuna namna ya kumkimbia mtu ambaye ana maslahi na wewe!?..
Usinitoneshe kidonda naumia sanausingefanya Mkuu ungeghairi ukampa hela ukaondoka
Acha uoga mkuu kula mbususu wewe maana hata hao wazee wanatuelewa vijana...Usinitoneshe kidonda naumia sana
Aiseee [emoji16][emoji119]Mimi naenda direct najua hata nikitaja shule wengi wamesoma pale, hii ni story ya kwanza.
Nilisoma shule moja inaitwa Shybush au Shinyanga sec, niliingia kidato cha pili msala ukatokea wananzengo wameiba bomba, Hp akakusanya wanafunzi nakwenda sehem inaitwa maganzo ambapo hapohapo na mimi nilikuwa sijui kama wameenda huko maana walikusanyana baadhi wengine tulikuwa hatujui basi sikuiyo namimi nikasema acha niende huko maganzo eeeebwanawee sinikakutana nao alafu huyo Hp alikuwa na misuli balaa si akanilazimisha nijiunge nao.
Basi baada yakujiunga nao na kusaka bomba tukalikosa maana hapo shuleni hatukuoga almost wiki hivi, basi Hp akaanza kupiga sim shule nzima ije ikichafue maganzo maana si unajua wanafunzi walivyo wakorofi? Duh! Hao wanafunzi wakagoma kwenda maganzo aisee Hp alikasirika wakati tunarudi tukaambiwa tuvae kininja tuchume bakora tukawachape waliobaki shuleni [emoji24][emoji24], masikini wengine walikiwa ni walemavu, aisee walichezea kichapo si cha polepole.
Kesho yake ukawa ni msala maana wengine walilazwa, wengine walivunjika vidole vya miguu, tukaitwa parade nakuambiwa tupige kura walioshiriki aisee nilianza kutetemeka huku nikijisemea si nimo kwenye huu msala? Dah! Bahati nzuri sikuwemo aisee niliponea tundu la sindano na walio gundulika wamefanya hivyo walifukuzwa shule aisee.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji2]
Ulitokea mgomo shuleni na umeme ulikuwa umekata wana wameenda kumtia adabu headmaster mimi nikaamua kujificha bwenini nkalala deka la juu, maana mshua aliniasa mambo ya migomo nisishiriki sisi ni masikini.
Ebwana eeh majamaa wameenda wakakuta headmaster kakimbia wakaona waje kuzimalizia hasira kwa waliolala bwemi waliokataa kugoma aisee
Bwemi la mbele kuna wanawakadakwa wakaanza kushambuliwa kwa bakora huku wengine wakivunja vioo,
Nilijikuta tuu nipo sakafuni natimua mbio kuelekea kwenye shamba la mahindi, kumbe kuna mmasai na wenzake walikuwa mle ndani nao nilishangaa wameibuka kama mizimu tunaongozana kwenye mahindi
Nimecheka Sana kmmk [emoji91][emoji16] [emoji16][emoji16][emoji119][emoji2]
Ulitokea mgomo shuleni na umeme ulikuwa umekata wana wameenda kumtia adabu headmaster mimi nikaamua kujificha bwenini nkalala deka la juu, maana mshua aliniasa mambo ya migomo nisishiriki sisi ni masikini.
Ebwana eeh majamaa wameenda wakakuta headmaster kakimbia wakaona waje kuzimalizia hasira kwa waliolala bwemi waliokataa kugoma aisee
Bwemi la mbele kuna wanawakadakwa wakaanza kushambuliwa kwa bakora huku wengine wakivunja vioo,
Nilijikuta tuu nipo sakafuni natimua mbio kuelekea kwenye shamba la mahindi, kumbe kuna mmasai na wenzake walikuwa mle ndani nao nilishangaa wameibuka kama mizimu tunaongozana kwenye mahindi