Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kumbe ndio alikuwa anajaza wese....dah inaelekea jamaa alikuwa anadatisha na ubooo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sitasahau hiki kisa kwa mshkaj wangu..baada ya kumaliza A level nikapata tempo ya kuandikisha sensa..sasa nilikua na mshkaj wangu mmoja ikawa nikija kutoka ma bush natoka nae tunakula gambe sana kisha tunaenda zetu disco kipimd hicho..tulikua na utaratibu wetu kuwa we party with no bitchez kwahyo ilikua ni kivyetu vyetu ..siku moja nimerud na mpunga wa maana tukaenda na mwana kama kawaida kula gambe..kdgo ikaja pisi kali sana..jamaa yangu akaielewa nikamwambia kama vp sema nayo..pisi ilikua inasoma chuo cha uhazil
Tbr bas baada ya jamaa kusema na mtoto kumbe mtoto alikua anajiandaa walikua wefunga chuo na kesho yake alikua anapanda treni kwenda dar..so wakakubaliana aende chuo kuchukua begi lake then waende guest then gambe na mambo mengine then kesho amuwahishe stesheni awah tren..jama akaniambia mtoto kaeleweka nikaona mshkaj nisimbanie..nikampa mpunga wanku spendi daah hapo ndo ilikua mistake..basi kwel jamaa akaenda nae chuo wakachukua mizgo then wakapanga guest na wakaja sehem nilipokuwepo tukaendeleza gambe kama kawa..mida mida jamaa akasema ngoja aende akale mzgo basi tukaagana..next day mshkaj akaniambia alikamua kama kawa na demu kesha sepa kwenda dar..basi ikapita hyo sasa siku moja tumekaa sehem mshkaj mmoja akatuona wkt yule mshkaj wangu ametoka basi yule jamaa akaniambia huyu ni jamaa yako nikamwabia yes akaniambia anakumbuka alimuona sehem flan na dem wa chuo ila dem
Mwenyewe kaungua na miwaya nikashtuka kinyama..nikapotezea ila ile kitu ilikua inasumbua sana kichwa siku moja nikamwambia mwana eebwana twende tukachek afya maana maisha mafup haya..aisee sitasahau ile siku baada ya mshkaj wangu kukutwa na ngoma na nikajiona nahusika kwa 80% na issue ile..kpndi hicho hakuna ARV wala nn..mshkaj alipata shock akaanza kuumwa kwa hofu ikawa ndo kuumwa mpk kifo..SITASAHAU AISEE
 
Niko form one muhula wa kwanza na niko likizo , kuna tajiri na kijana mmoja walikuja kijiji kwetu kununua mpunga.
Nikawa nimejenga urafiki na yule kijana.

Wakawa wamekodi godown kwa hiyo mpunga ulikuwa unahifadhiwa humo. Yule tajiri yeye alikuwa anarudi mjini akimuacha yule kijana pale kijijini na alikuwa analala humo humo kwenye godown.
Baadae tajiri aliniomba(bila malipo yoyote) niwe nampa kampani yule kijana kwa kulala wote kwenye godown, nilikubali bila kujua nilikuwa nahatarisha maisha yangu.

Tajiri siku zingine alikuwa haji na anamuachia yule kijana fedha za kununulia huo mpunga kwa siku ambazo hatakuja. Kuna siku ambayo aliacha fedha na mpunga haukununuliwa kwa kiasi kikubwa kwa hiyo kijana akabaki na salio.

Kitendo cha kubaki na salio kumbe wahuni washajua. Hawa wahuni ni jamaa waliowahi kukaaa mjini wakawa wamerudi kijijini kutokana na changamoto ya maisha kwa wazazi wao.Walijulikana kutokana na baada ya tukio kutoonekana.

Imefika usiku baada ya story za hapa na pale tukalala. Baadae katikati ya usingizi nilishtushwa na kitu kikitua kwenye kichwa changu , nikawa nimepigwa panga kwenye paji la uso. Tukaambiwa tuwape hela la sivyo watatuua.

Walipoona nimeloa damu na siwaangalii usoni wakawa wako na kijana wakimpiga mapanga ya ubapa. Kijana akawa anagoma kwamba hana hela lakini baadae walipata kiasi kilichokuwa kimebaki alikokuwa ameficha kwenye magunia.

Baada ya kuondoka nilijikongoja mpaka nyumbani maana ilikuwa karibu, wazazi walinipeleka fasta hospitalini na kushonwa nyuzi.

Tajiri hakuamini kama tulivamiwa, hii ndio inanifanya nijute mpaka leo.
Baada ya mimi kutolewa hospitalini tajiri akatuita mimi na kijana wake akituambia tuseme ukweli kama tumejiumiza au la maana anaenda kwa mganga.
Tulimwambia aende tu kwa mganga.

Mpaka leo kovu lipo kwenye paji na nilirudi shule nikiwa na nyuzi. Nikikumbuka tukio hili najiona mjinga kukubali ombi la yule tajiri bila malipo huku nikihatarisha maisha yangu. Nawaza angeshusha kidogo angeweza kunikata shingo.
 
Lomnyaki ni koumer....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
🥺🥺🥺🥺😭😭Hamna jinsi ungefanyaje sasa
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji24][emoji23]dah
 
So sad
 
Udomo zege ndo ulikukosesha tunda
 
Sad
 
Pole.Cha ajabu baada ya hayo kutokea,ukute tajiri hakukupa hata mshiko kidogo tu wakufutia machozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…