Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Well kuna kisa kingine tena yani issue moja hadi leo inanichoma sana pia na kutokujua pia ilinicost sana sana.

Basi mwaka flani nyuma kidogo nilipokua nimemaliza form 6, nikapata kazi moja ya muda somewhere hapa Dsm na nikasema nitaenda chuo mwaka mwingine wacha nifanye hii job kwanza sababu ilikua inalipa poa sana so sikutaka kuiacha tu na pesa zote hizo, basi that time nikawa naishi kwa brother angu mmoja around banana na ni sababu ilikua karibu na job nikasema nitakaa kwa muda, brother alikua anaishi na mwanamke wake mzuri sana, ila walikua hawajazaa but huyo mwanamke ako na mtoto wake, basi hiyo nyumba wamepanga ziko nyumba 3 ndani ya fensi moja, sasa hizo nyumba mbili wamepanga hao single mother nyumba moja, ingine ni mmama tu ako na mtoto wake.mmoja na house girl ila mwanaume wake huwa anakuja mala moja moja na anapesa (ni mume wa mtu so ye ni mchepuko tu ulipangishiwa nyumba nzima).

Hao wamama walikua wambea vibaya sana yani wao hata ukikaa nao like 2 minutes utajua mtaa mzima nini kinaendelea, so walikua mala nyingi wako tu nyumbani , sku moja wakaniambia unajua huyo shemeji yako hampendi huyo unaemwita kaka ako, hampendi na ndio maana hamzalii mtoto, kila mala amapata mimba anatoa, wakanipa hadi ushuuda kua wao.ndo humsaidia hata kumsafisha akinywa madawa yake ya kutoa mimba ikitoka, waliongea sana na mimi maneno yakaniingia. Basi hakuna kitu nachukia kama watu wanaotoa mimba, nikaanza kumchukia kidogo kidogo yule shemeji wakati nilikua nampenda sana hata alihisi kuna kitu i think, pia alikua na roho nzuri sana yule dada ila nikamchukia na nikiona wanagombana hata siwi upande wake tena like before, basi one day kweli kumbe alikua na mimba ila wao wawili tu na mumewe ndio wanajua, basi kumbe mimba tena ilitoka akiwa ndani, akapigia simu friends wake na shangazi yake wakaja kumsaidia, me nimetoka job hapo nakuta hali ndo hivo analia kwa uchungu, nakumbuka niliongea maneno mengi sana that day, nae alikua na hasira mbaya hiyo tukagombana hivo hivo akiwa mgonjwa namtuhumu anatoa mimba makusudi kama hamtaki si amuache, tuligombana sana hadi akanifukuza home, wale wamama wambea walikua nnje wanaskiza nilipotoka wananipongeza , mpaka wakanipa room kwao nikalala sababu ilikua usiku ila yule bro alikua hajarudi, nikaona kwenye dirisha shemeji katoa vitu vyangu vilivyobaki akavichoma moto hapo analia kwa uchungu na hasira, kumbe bwana anamatatizo tu ya kiafya na mimi nilikua sijui thats why mimba hua zinatoka pia.

Tukaachana me nikaenda kwa my friend mwingine alikua ashaanza chuo IFM alikua amepanga nyumba somewhere. Basi after like 1 year ushapita yule bro akanicall shemeji yako amejifungua mtoto wa kiume, nikampongeza hapo bado hatuongei na yule shemeji hata sikumpigia hata simu.

One day kama after 3 month yule bro tena usiku akanipigia akiwa na hudhuni kuu , akaniambia aisee shemeji yako hatunae tena, niliogopa sana nikamuuliza what happened akasema miaka yote shemeji yako ana kisukari, tena kikali sana na anaishi kwa hayo ma insulin, akasema jana yake waliendesha gari hadi morogoro kulikua na msiba wa babu wa huyo mwanamke so wakawachukua na ndugu baadhi wakaenda nao, walipofika shemeji akakumbuka amesahau kubeba insulin, na akamwambia please ninunulie insulin huku tafadhari manake nina stress ila bro akasema haina shida tutawahi kurudi (ubahili japo anasema aliona.mbona huwa anaweza kukaa hata 4 days au wiki nzima bila kuchoma so akaona kawaida tu hakuna kitu kitatokea in 24 hours) wakasema kesho yake wawahi kurudi (alikua muslim family so walizika siku hiyo hiyo) basi akasema asubuhi yake wameamka fresh tu akiwa mzima ila huyo bro kumbe alimgombeza sana wakafokezana na according tu doctor kumbe alikua haruhusiwi hata kua na stress sababu hiyo inapandisha sukari yake kwa haraka sana anaweza kufa, kumbe sukari ilipanda na alikua hana insulin, wakawasha gari kurudi Dar na kwenye gari wanasema alikua fresh tu, wamefika wanaita maili moja akasema wacha nilale, akalala, hadi wanafika ubungo bado amelala , sasa wanawashusha watu wengine walikua kwenye gari wanamuamsha haamki, kumbe ashakufa kitambo ni wa baridi na kaacha katoto kachanga ka 3 month, nikakumbuka lile tukio nilomfanyia na kumbe halikua kosa lake mimba kutoka ila ni sababu ya kisukari, nikaja kujua kumbe yeye ndio alikua hata anataka mtoto sana sana ila anashindwa na hicho kitu kimemuuma miaka mingi, hadi leo najiskia vibaya sana, nikaja kuangalia account yangu ya facebook nikakuta kumbe alinitafutaga kunijulia hali few days ago na akanipigia pia ila number ikawa haipatikani as nilimblock, aisee shemeji.nisamehe sana , hii kitu hadi leo inaniuma sana, sikupata nafasi ya kumuomba samahani eeeh Mungu i hope umenisamehe kwa hili. Alikua anakisukari thats why hata nilipomuapset wale wamama walinipia simu after two days amelazwa hospital. God forgive me kwa kile nilifanya[emoji20].

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
Ooh pole sana mkuu. Na hongera kwa kupata mke anayewalea vizuri watoto wako.

Btw huyo mke wako wa sasa hivi; umesema kuwa marehemu mkeo alikuwa akimchukia. Alikuwa mchepuko wako au alichukiwa kwa sababu gani?
 
Duuh pole sana nkamu. Aisee tujitahidi kutafuta amani na watu wote; kama inawezekana. Hivi vinyongo na uchungu huwa vinatumaliza wenyewe tu tunaovibeba
 
Umesomeka na kuekeweka vyema lakini je huoni kwamba uki entertain hizo regrets utaambulia maumivu???

Pamoja na uliyosema regrets zitumike Kama kumbukumbu tu vinginevyo zitakuletea madhara

Solution ya regrets ni kupambana na wakati uliopo maana hizo regrets zilifanywa na akili ya kipindi hicho usiidharau hiyo akili, sasa una akili nyingine unaweza kufanya makubwa zaidi.

The only time is right now
 
kipindi Iko keko hukatizi kimama....Kuna wahuni wa kuitwa wasumbufu ao noma....!nashangaa hao Wana eti kiwanja Chao cha kutambia kilikuwa king palace dah....umeacha inferno au uku JJ amani ya kutosha
Shida totoz that time zinasomeka sana king , nigga huko kwingine ni mbilingembilinge za washua.
 
Ooh pole sana mkuu. Na hongera kwa kupata mke anayewalea vizuri watoto wako.

Btw huyo mke wako wa sasa hivi; umesema kuwa marehemu mkeo alikuwa akimchukia. Alikuwa mchepuko wako au alichukiwa kwa sababu gani?
Alikuwa mchepuko hii ndo faida ya kuwa na mchepuko pindi inapotokea km hivi huwa wanasaidia sn huyu mchepuko alikuwa anajua wanangu kitambo hata watoto nilikuwa nawatuma kwake
 
Alikuwa mchepuko hii ndo faida ya kuwa na mchepuko pindi inapotokea km hivi huwa wanasaidia sn huyu mchepuko alikuwa anajua wanangu kitambo hata watoto nilikuwa nawatuma kwake
Aaah kwa hiyo ulitegemea mkeo aupende mchepuko wako? Yaani ni kama unamsimanga marehemu mkeo kwamba mwanamke aliyemchukia ndiyo amekuwa mwema kwa watoto wake leo; una-justify kila ujinga na unyama ulioufanya kwa marehemu mkeo na ndoa yenu. Yaani ulikuwa na mkeo wa ndoa; ila hadi watoto ulikuwa unawatuma kwa mchepuko??? Huyo mkeo wa sasa hivi; hata awe mwema kiasi gani haibadili ukweli kwamba wakati mkeo yupo hai; wewe na huyo mchepuko wako ndiyo mlivunja ndoa yenu kwa uzinzi, na mlimsababishia marehemu mkeo mateso, maumivu na stress. Na usikute yeye ndiyo alichangia hata kumrudisha marehemu mkeo kwao. Mtubu, yasije yakawarudi na ninyi

So na sasa hivi una faida nyingine pembeni (mchepuko?). UMENISHANGAZA, UMENISIKITISHA....... Anyway, to each his own.
 
Sitahau Tuliuza mbuzi wa headmastress .iAlisema kama mnatak shule tulimpe mbuzi wake bila ivyo nyumbani bila hadhabu shule huna. bahat nzur nilikuwa na kadem kiongozi wa chakula Ili nisfukuzwe shule aliniambia ataniibia mahidi nikauze nipate hela ya kulipa mbuzi.Yule dem alikuwa ananielewa balaa .Akaniambia siku ya kwenda kusaga atazidisha hesabu ya kilo za kupeleka mashineni akazidisha loba mbili debe kumi kila roba pale ilitakiwa 140,000/= coz walikuwa mbuzi wawili kweli Tulanikikwa kulipa wale mbuzi kesi ikaisha lakin yule dem alikuwa ana wivu sana alikuwa akion nipo na msichana ana nimaindi sana.mim nikaona isiwe kesi bhna ngoja niachane nae la kuwa liwepo kunasiku nikaamzaba vibao kwnye michezo alikuwa ananitukana baadae mambo yakaisha nashangaa nimeitwa kw mwlim wa nidham anasema nilienda kwenye bwen la wasichana kumfata msichana mwingine tofauti na uyu aliekuwa dem wangu kumbe yule demu alienda kunichongea kwa walimu kwmba mm nalala bweni la wasichana daah niliumia sana kusingiziwa vile na yule dem baadae akaletwa dem mwingn at sijawai kumtokea nikaaambiwa ulikuw unamfata uyu bas pale tukalimwa adhabu wote mim na yule dem kufatua tofali elf tatu kila.mmoja. Sitahau .
 
MMH huyu amenisikitisha sana na kunishangaza sana, ila Mungu wa haki yupo
 
Kisa kama hiki kilimgharimu shemeji yangu akawa amefukuzwa chuo mwaka wa mwisho, Ili bidi aende jeshi kwa mayokeo ya six

Nilikunywa sana bia zake bila kujua anapata wapi hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…