Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

w
we jamaaa tema mate chini🤣🤣🤣
 
Unaongea fact kabisa...
Hizi mambo niliwahi ongea mbele ya wazee wangu,wakasikitika wakaona nimechanganyikiwa,nishapotoshwa na dunia.
 
Ukristo kiukweli hasaa hauendani na maumbile ya m.damu

tukatae tukubali lkn ukweli ndo huo
 
[emoji23][emoji23]
 
Nami ngoja nishushe kisa changu hapa.
Mimi nilianza kidato cha kwanza nikiwa na miaka 24 nikasoma mpaka Namaliza kidato cha nne, wakati nasoma shule hiyo walimu walinielewa, hata ikitokea kuna jambo nimekosea naomba msamaha yanaisha siadhibiwi japo makosa Yale ya wanafunzi wote nilikuwa naadhibiwa, nikahitimu kidato cha nne, baada ya matokeo kutoka nikaenda shule nyingine ya kulipia, nikaanza kidato cha tano kabla sijalimaliza kidato cha tano nikahamia shule nyingine, kwenye hiyo shule kulikuwa na utaratibu wa kuvaa t-shirt kwa siku maalumu bila shati la shule mimi nikiwa bado mgeni nikavaa, muda wa mapumziko nikatoka nje kuna mwalimu alinikamata akasema kwa nini sijachomekea t-shirt nikamuomba msamaha hakukubali akataka kuniadhibu nikambembeleza lakini ikashindikana akanichukua mpaka ofisini kufika ofisini wakaitwa viongozi wa wanafunzi yakafanyika mazungumzo kwa muda mrefu baadae nikakubali kuadhibiwa akasema kama umekubali tunagonga kengele Kisha unaadhibiwa mbele ya wanafunzi wote wakishuhudia nikawaza sasa hapa nitachakaa kwa kipigo nikamwambia hapana kama naadhibiwa hapa ofisini Sawa ila kama ni assembly hapana na yeye akakataa kuniadhibu ofisini basi baada ya hapo akasema atalifikisha kwa headmaster akasema moja Kati ya mawili lazima litokee ni yeye kuacha kazi au mimi kufukuzwa shule wakati huo headmaster alikuwa amesafiri tangu nihamie nilikuwa sijamuona, nikaona mambo yamekuwa magumu upande wangu nikatoka ofisini nikaenda bwenini nikawaza kuwa sina namna nyingine zaidi ya kuondoka, siku ya pili nikapanda basi narudi nyumbani, baada ya hapo nikachukua cheti changu cha kidato cha nne na kwenda kusomea taaluma fulani kwa level ya certificate na nikaajiriwa yasingenikuta hayo ningeajiriwa nikiwa na diploma au degree.
Ni hayo tu kwa Leo.
 
Pole sana kiongozi. Shukuru kwa yote. Yawezekana ungesoma mpaka digrii then ukaishia mtaani. Shukuru kwa ulichonacho
 
Umeshamshughulikia huyo mbaya wako au bado?
 
Wewe jamaa utakuwa na tabia ya kutusi watu usiowajua...

Ushawahi nitolea lugha chafu hapa jukwaa, vile mimi ni mtu wa kupuuzia tu...

Nimesoma visa vyako viwili humu, nimepata picha...

[emoji1787][emoji1787] unammind
 
Hiyo inayofuata sasa[emoji1787][emoji1787]
 
We jamaa bhn[emoji28][emoji28]
 
Nikiwa chuo mwaka wa kwanza,nilikua nakaa hosteli Basi Kuna mdada tukawa tumezoeana Sana ingawa tulikua tunasoma course tofauti na Mara nyingi alikua anakuja chumbani kwetu,tunapiga stori na roommates wengine au kuangalia movie,alikua ana boyfriend wake Ila yeye anasoma chuo kingine,Sasa sikumoja akaja room tukawa tunaangalia movie tupo Kama wanne hivi Ila yeye alikua busy Sana na simu,baadae anatuambia eti Fulani( huyo boyfriend Sasa) kanitumia message anataka kujiua hivi mtu anayetaka kujiua anasema kweli?, Sisi tukamwambia bwana mtu akitaka kujiua hasemi,utasikia tu amekufa,tukatania pale kila mtu akaendelea na movie,kesho yake natoka darasani mchana nikakutana na bajaji inatoka hosteli kwa nyuma amekaa mdada mwingine halafu yule rafiki yangu kamlalia yaani Kama vile mgonjwa nikawa najiuliza huyu kaugua saa ngapi mbona asubuhi nimemuacha mzima,baadae Sasa wakarudi hosteli analia nikaenda kumuona namuuliza vipi, ananiambia yule boyfriend wake kajiua kweli na hapo ndio ametoka kumuona alipigiwa simu na dada wa marehemu, yaani nilifreeze kwanza kwa muda ,nikatamani masaa yarudi nyuma aniulize Tena lile swali halafu nimpe jibu tofauti dah mpaka leo nikikumbuka huwa naumia Sana.Mpaka leo mtu akianza kuniambia masuala ya kujiua Nampa counseling ya nguvu haijalishi ananitania au vipi maana wengine inakua Ni cry for help.
 
Ndio mm huyo nipo zangu peponi huku... walah ukija lazma nikusukumie kwenye tanuru la moto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…