Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nikiwa chuo mwaka wa kwanza,nilikua nakaa hosteli Basi Kuna mdada tukawa tumezoeana Sana ingawa tulikua tunasoma course tofauti na Mara nyingi alikua anakuja chumbani kwetu,tunapiga stori na roommates wengine au kuangalia movie,alikua ana boyfriend wake Ila yeye anasoma chuo kingine,Sasa sikumoja akaja room tukawa tunaangalia movie tupo Kama wanne hivi Ila yeye alikua busy Sana na simu,baadae anatuambia eti Fulani( huyo boyfriend Sasa) kanitumia message anataka kujiua hivi mtu anayetaka kujiua anasema kweli?, Sisi tukamwambia bwana mtu akitaka kujiua hasemi,utasikia tu amekufa,tukatania pale kila mtu akaendelea na movie,kesho yake natoka darasani mchana nikakutana na bajaji inatoka hosteli kwa nyuma amekaa mdada mwingine halafu yule rafiki yangu kamlalia yaani Kama vile mgonjwa nikawa najiuliza huyu kaugua saa ngapi mbona asubuhi nimemuacha mzima,baadae Sasa wakarudi hosteli analia nikaenda kumuona namuuliza vipi, ananiambia yule boyfriend wake kajiua kweli na hapo ndio ametoka kumuona alipigiwa simu na dada wa marehemu, yaani nilifreeze kwanza kwa muda ,nikatamani masaa yarudi nyuma aniulize Tena lile swali halafu nimpe jibu tofauti dah mpaka leo nikikumbuka huwa naumia Sana.Mpaka leo mtu akianza kuniambia masuala ya kujiua Nampa counseling ya nguvu haijalishi ananitania au vipi maana wengine inakua Ni cry for help.
Jamaa kajiua kaacha bia ilivyo tam
 
Nami ngoja nishushe kisa changu hapa.
Mimi nilianza kidato cha kwanza nikiwa na miaka 24 nikasoma mpaka Namaliza kidato cha nne, wakati nasoma shule hiyo walimu walinielewa, hata ikitokea kuna jambo nimekosea naomba msamaha yanaisha siadhibiwi japo makosa Yale ya wanafunzi wote nilikuwa naadhibiwa, nikahitimu kidato cha nne, baada ya matokeo kutoka nikaenda shule nyingine ya kulipia, nikaanza kidato cha tano kabla sijalimaliza kidato cha tano nikahamia shule nyingine, kwenye hiyo shule kulikuwa na utaratibu wa kuvaa t-shirt kwa siku maalumu bila shati la shule mimi nikiwa bado mgeni nikavaa, muda wa mapumziko nikatoka nje kuna mwalimu alinikamata akasema kwa nini sijachomekea t-shirt nikamuomba msamaha hakukubali akataka kuniadhibu nikambembeleza lakini ikashindikana akanichukua mpaka ofisini kufika ofisini wakaitwa viongozi wa wanafunzi yakafanyika mazungumzo kwa muda mrefu baadae nikakubali kuadhibiwa akasema kama umekubali tunagonga kengele Kisha unaadhibiwa mbele ya wanafunzi wote wakishuhudia nikawaza sasa hapa nitachakaa kwa kipigo nikamwambia hapana kama naadhibiwa hapa ofisini Sawa ila kama ni assembly hapana na yeye akakataa kuniadhibu ofisini basi baada ya hapo akasema atalifikisha kwa headmaster akasema moja Kati ya mawili lazima litokee ni yeye kuacha kazi au mimi kufukuzwa shule wakati huo headmaster alikuwa amesafiri tangu nihamie nilikuwa sijamuona, nikaona mambo yamekuwa magumu upande wangu nikatoka ofisini nikaenda bwenini nikawaza kuwa sina namna nyingine zaidi ya kuondoka, siku ya pili nikapanda basi narudi nyumbani, baada ya hapo nikachukua cheti changu cha kidato cha nne na kwenda kusomea taaluma fulani kwa level ya certificate na nikaajiriwa yasingenikuta hayo ningeajiriwa nikiwa na diploma au degree.
Ni hayo tu kwa Leo.
Bado una nafasi ya kujiendeleza
 
Nikiwa chuo mwaka wa kwanza,nilikua nakaa hosteli Basi Kuna mdada tukawa tumezoeana Sana ingawa tulikua tunasoma course tofauti na Mara nyingi alikua anakuja chumbani kwetu,tunapiga stori na roommates wengine au kuangalia movie,alikua ana boyfriend wake Ila yeye anasoma chuo kingine,Sasa sikumoja akaja room tukawa tunaangalia movie tupo Kama wanne hivi Ila yeye alikua busy Sana na simu,baadae anatuambia eti Fulani( huyo boyfriend Sasa) kanitumia message anataka kujiua hivi mtu anayetaka kujiua anasema kweli?, Sisi tukamwambia bwana mtu akitaka kujiua hasemi,utasikia tu amekufa,tukatania pale kila mtu akaendelea na movie,kesho yake natoka darasani mchana nikakutana na bajaji inatoka hosteli kwa nyuma amekaa mdada mwingine halafu yule rafiki yangu kamlalia yaani Kama vile mgonjwa nikawa najiuliza huyu kaugua saa ngapi mbona asubuhi nimemuacha mzima,baadae Sasa wakarudi hosteli analia nikaenda kumuona namuuliza vipi, ananiambia yule boyfriend wake kajiua kweli na hapo ndio ametoka kumuona alipigiwa simu na dada wa marehemu, yaani nilifreeze kwanza kwa muda ,nikatamani masaa yarudi nyuma aniulize Tena lile swali halafu nimpe jibu tofauti dah mpaka leo nikikumbuka huwa naumia Sana.Mpaka leo mtu akianza kuniambia masuala ya kujiua Nampa counseling ya nguvu haijalishi ananitania au vipi maana wengine inakua Ni cry for help.
Kwanini alijiua au hukufuatilia
 
Usiku mmoja nikiwa katika harakati za kutafuta elimu nipo mikoa ya watu shuleni kwetu dinning Hall ilikua pia inakodishwa kwa ajili ya shughuli nyingine za kijamii kama harusi na send off.
Hio siku prepo haikuepo kwa kua kulkua na shereh dinning mimi na wanangu wachache wahuni tukapanga tuvamie sherehe Ile ilosifika kua ya watoto wa matajiri wa mji ule.
Nikatoka general wa vita kwenda kutazama ulinzi na usalama na kuandaa plan ya kuzamia..kufika eneo la tukio nkascan haraka nkaona dress code suti nyeus na tai kwa wanaume uzur na shuleni ni maeneo ya baridi tulkua tunavaa suti pia.
Wanaume tukabadilika tukafika eneo la tukio mimi nkatokea kwenye parking kulkua na discovery imepaki nafika getini mlinzi wa getini ni jamaa wa mtaani ambae ananijuaga mm ni dent miyeyusho spend shule (huyu jamaa alkua anauza viatu raba nlkua naenda kuchukua za kwendea club usiku) wenzngu walifanikiwa kupenya mm ikashindikana
Kufika mishale ya saa 4 kwendea 5 akatoka dada mmoja mrembo tu akawa anaongea na simu (nafikiri alipigiwa na mmewe akitakiwa nyumban) nkamfata akanpa kadi akawasha gari yake akaondoka

Nkarudi getini tena yule jamaa anataka kunsukumizia mabaunsa nkatoa kadi akawa ananiangalia kwa kuntaman. Mwanaume nikazama ndani na kukuta wenzngu washapata na wachumba nkachagua angle moja nzuri ya nkatulia muda ukakatika mziki tukacheza na misosi tukala sana

Sasa kuna ule utaratb wa watu kukusanya vinywaji na makulaji na kufunga ili kwenda navyo majumban basi mwshon kabisa mwa shughul nikaona package kubwa ipo inazagaa zagaaa (sjui roho gan ikaniingia inanambia unaacha vinono ivo kesho utakinga ugal maharage nikajikuta nasogelea ule mzgo) katika malez yangu mm kitu sijawezaga ni kuchukua cha mtu basi nikachukua kile kifurushi aisee Ile nageuka nilipigwa mibanzi (yule mzee hatar anapiga mibanz kama sokwe) nkabak nimekua mdgo kusema nmuanzshie vagi yule mzee ningeweza ila ningezua soo kubwa ukizingatia nlizamia so yule mzee alinzaba mikofi kama 6 ivi na wala hakuongea na mm wala sikusema nikageuka kutazama wenzngu naona wanaparty na kina mama nkatoka nje nkaenda kulala uku nikiomba Ile mibanzi kusiwe na mtu ameiona na ndo ikawa ivo

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Duh
 
Mkuu ulituangusha wanajeshi wa mpakani.
Mimi walinibembeleza wanishikisha hizo cards, nikashinda vocha ya buku 8 wakaniambia niwape simu waniwekee nikawapa.

Badae nikashinda redio bas wakasema nichangie hako ka percentage, nikasema sina hela, wakanishawishi nikagoma, wakasema nilipe fine ndo wanirudishie simu yangu.

Tukazozana kidogo pale, yule mgawa card anakaaga ndani ya zile kamba zilizungushwa pale akasogea kidogo usawa wangu nikamtia kabali mithili ya jon cena. Akamwambia yule muweka vocha kwenye kile kigari chao alete simu yangu.

Wakanipa simu pamoja na furushi la matusi, me nkatokomea zangu na kumwacha yule mpumbavu akikohoa kwa lilo roba nililomkwida.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] safi sana
 
Dah nimejisikia uchungu sana sababu kisa chako kinafanana na changu nilipigwa bila kosa nimesingiziwa nimeiba na mmoja wa wapangaji kwenye nyumba tulikua tumepanga siku hiyo nilichezea kichapo kama mbwa koko. Na kwakua ilikua kawaida yao kunisingizia nilionekana mwizi wa familia wakati sikuwahi kuiba asilani niliumiaaa sana nikaweka kinyongo moyoni ilikua mwaka 94 nilikuja samehe 2001 nikiwa kanisani mchungaji alihubiri kuhusu msamaha nilimkalisha Kitako mzee nilimsema akaomba msamaha.Nilichojifunza usimtende mabaya mtoto hata wa miaka 3 ata kumbuka daima
Bado hujasamehe, ungesamehe usingekumbuka
 
Back
Top Bottom