Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Ah mzee wa ruaka....umenikumbusha nilikuwa naishi pale ruaka joyland....mzeya mdogomdogo naingia zangu pale two rivers mall...hatari. i miss that place man.....dah alafu ukiwa unaenda kule limuru shenzi type ningekuwa na mihela ningenunua plot kule...pazuri sana
 
Hapo lazima uka update mwili yani uchange damu nzima ili uanze maisha upya ila me nimeishi na mtu ambaye yakipita masaa kadhaa hawezi bila sigara sijui kwanini.
 
kuwa makini na mambo mengine kabla hujaandika. Jf members wengi tunadhani majina ya uongo ni salama.
KAMA ULIUA BILA KUKUSUDIA NENDA KAWASHTAKI HAO WALIOKULAGHAI.
 
Kama sikosei nilikua nashukia kituo kimoja kinaitwa "kahigo au kahego". Kuna apartments zipo upande wa kulia wa barabara (ukitokea tao/town) ndio nilikua nakaa pale. Long Time!
 
Malizia mkuu, hivi kwanini hela za betting hua zinaisha kimiujiza miujiza?
 
Hapo lazima uka update mwili yani uchange damu nzima ili uanze maisha upya ila me nimeishi na mtu ambaye yakipita masaa kadhaa hawezi bila sigara sijui kwanini.
Noma mwanangu yabi unahisi huwezi fanta chochote bila stimu damu itembee bila hivyo unakua mgonjwa kabisa kimwili hadi kiakili
 
Noma mwanangu yabi unahisi huwezi fanta chochote bila stimu damu itembee bila hivyo unakua mgonjwa kabisa kimwili hadi kiakili
Hapo kujulikana mkiwa ugenini ni rahisi sana na hilo ndilo linakup wakati mgumu sana
 
Umesoma muhas? Hii story ni km ilitokea pale
 
We nakupendekeza kuwa katibu wa Chama cha Bavicha
 
Habarini Ndugu zangu,

Hili sio juto lakini kama lingetimia basi lingekuwa juto la maisha yangu.

Nitakuwa short and clear.

Ilikuwa kipindi cha UE majira ya joto pale mkoa wa Chief Kingalu, ulikuwa ni mtihani wangu wa kujiuliza katika ukumbi mmoja maarufu sana pale chuoni ukifahamika kwa jina sawa na uwanja mkuu wa Mpira mkoa wa Iringa kama sikosei.

Lile somo lilikuwa ni tough kwangu na sikuwa nikilipenda. Dakika chache kabla ya kwenda kwenye mtihani nlikuwa na revise na jamaa yangu ambaye tuliongea tuweke kijiji au formation kwa ajili ya kupeana sapoti.
Yule jamaa alikuwa ni bingwa wa kubashiri maswali, basi akaandka majibu yake na solvings kwenye karatasi nusu ya A4 likiwa na maswali mawili na solvings.

Tumeingia kwa paper,tumekaa nyuma, jamaa kayakuta maswali yake mawili kama yalivyo, akayakopi kama yalivyo, kiufupi huyu jamaa yangu ni mzoefu wa hizi mishee. Advantage aliyokuwa nayo alikuwa amekaa katikati ilhali mie nikiwa nimekaa upande wa kulia mwishon ambako imepita njia na ngazi za kwenda floor ya juu (Kama unaujua huu ukumbi ushanisoma).

Nikaona nsije nikafa na kiu bwawani ,nikaomba anipasie mkeka nicopy chapu chapu huku nikitetemeka. Nimepewa ule mzigo nikpokea kwa mkono wa kushoto nikaukunja kwanza, nikacheki mazingira wasimamizi walipo, nikaona kupo safi lakini nikawa muoga kutoa mkeka pale chini ya dawati kuuweka juu.

Nikamuuliza jamaa yango oyaa vipi kupo safi, jamaa akawa hajibu yuko busy nikamuuliza tena akawa kimyaa.... Nikaona sio kesi nika spin jicho around kidogo nakutana na msimamizi yupo kwa juu ananicheki kwenye ngazi[emoji24][emoji24] nikaona hii ni soo mawazo ya kudisco yakanijiaa akilin mwangu.

Nikaona isiwe kesi ntapambaa kiume nikawa namlia timing aanze tu kushuka ili nitupie mdomoni ,wakati huo mkono wa kushoto unafinyanga kile ki mkeka. Ile anaanza tu kushuka ngazi mie nikatupiaa mdomoni fasta nikatafuna. Jamaa ameshuka amekaa nyuma yangu, akaangailiaa [emoji28][emoji28][emoji120] akaenda upande wa kushoto kwangu akasogea mbele yetu akawa anatuangaliaa akapotezeaa[emoji23][emoji120][emoji120].

Aiseeee ilikuwa ni furaha sana ,kwa ule muda nlikuwa nimewaza naanzaje kusema nyumbani nimekamatwa na cheat kwa paper na sijawahi fanya huu upuuz maisha yote ya shule, aibu yake mtaani, nitaambia nn jamaa zangu rafiki je,..

Msala ukaendeleaa ,wakati ameenda mbele basi akaja msimamizi mwingine, huyu msimamizi mwingine ni jamaa yetu kamaliza chuo pale madarasa ma2 mbele yangu, nlifahamiana naye kwenye tour moja ya kwenda Uluguru Mountain.

Akaja nyuma yangu akawa anaongea na jamaa aliyeko nyuma yanguu, [emoji23][emoji23] nikasema akitoka huko akija anisemeshe basi nimeisha maana nina karatasi mdomon, huwez kulimeza kwa ukubwa wake nitakabwa... Nikawaza nilimeze?? Je nikimeza afu nikabwe sindiyo nitaita attention ya msimamizi ajue shida nn, je vipi akija akute nimekabwa na karatasi mdomoni.... Nikasema simezi kama mbwao iwe mbwai huyu jamaa yangu hawezi nifanyia roho mbayaa...

Mungu sio Benedicto jamaa akanipitaa akaenda zake mbele, nikatoa karatasi nikaweka kwenye sockis huku nikijawa na furaha sana [emoji23][emoji23][emoji120] Nlimshukuru Mungu na kuapa sitorudia kuomba mkeka chumba cha mtihani.

Asante sana sir Mchaki najuaa ulinisevu sana, lile tukio uliliona ukanisevu mdogo wako
 
Haaaaah haaaaah nmecheka balaa hapo ni Samora Mimi ilinikuta mule OC haaaaah madogo Ma TA walininasa sitakuja kusahau
 
Duuu bro kama nakuona kama najiona mpk nimekuhurumia,nikajihurumia pia,anyway wewe ni mwanaume hakuna ambae angeruka huu mchongo tena mweeeupe,hata mie nisengeruka hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…