Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

NAIROBI

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach kimya kimya wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.

Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favor tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.

Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!

Na hilo likawa funzo langu!
Ah mzee wa ruaka....umenikumbusha nilikuwa naishi pale ruaka joyland....mzeya mdogomdogo naingia zangu pale two rivers mall...hatari. i miss that place man.....dah alafu ukiwa unaenda kule limuru shenzi type ningekuwa na mihela ningenunua plot kule...pazuri sana
 
Miakankadhaa nyuma... mida ya jioni niko na wanangu tunazurul tu mtaani ghafla mwana anasema tupite home kwao kidogo kuna nshu kasahau then tuendelee misele kukagua mitaa...

Kwao geti kali wana walinzi wamasai na nini... tumekaa zetu ubarazani tunamsubiri mwana atoke ndani tusepe huku tunapiga story na masai mlinzi..

Story zikiendelea ghafla masai anatoa kichupa kina unga mweusi amaweka mdomoni tunamuukiza oya nini hiyo unaweka mdomoni Masai anasema chkua weka na ww rafiki utafurahi...

daaah sitakuja kisahau hii siku asee since that day i hv been addicted to snuff na inanikwamisha mambo kibao yani...

Hii mambo ya kujaribu jaribu kila kitu sio poa... unaweza haribu future yako yako yote kifala sana
Hapo lazima uka update mwili yani uchange damu nzima ili uanze maisha upya ila me nimeishi na mtu ambaye yakipita masaa kadhaa hawezi bila sigara sijui kwanini.
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
kuwa makini na mambo mengine kabla hujaandika. Jf members wengi tunadhani majina ya uongo ni salama.
KAMA ULIUA BILA KUKUSUDIA NENDA KAWASHTAKI HAO WALIOKULAGHAI.
 
Ah mzee wa ruaka....umenikumbusha nilikuwa naishi pale ruaka joyland....mzeya mdogomdogo naingia zangu pale two rivers mall...hatari. i miss that place man.....dah alafu ukiwa unaenda kule limuru shenzi type ningekuwa na mihela ningenunua plot kule...pazuri sana
Kama sikosei nilikua nashukia kituo kimoja kinaitwa "kahigo au kahego". Kuna apartments zipo upande wa kulia wa barabara (ukitokea tao/town) ndio nilikua nakaa pale. Long Time!
 
BETTING

Waliotutangulia huku duniani waliandika kuwa betting au uwekezaji kwa lugha ya kibiashara dunia ya leo sio kitu cha kutegemea ki uchumi kwa sababu hakitabiriki na huwezi kuwa master katika career hii. Hivyo basi ni muhimu kutafuta kazi inayotumia skills ambayo unaweza kui master kwenye kutafuta pesa kuliko kutegemea mambo ya kubahatisha.

Looh, sikuwahi kuelewa walimaanisha nini kwa kipindi kile. Japo nilikuja kuelewa in a hard way!

Miaka kadhaa nyuma, wakati mambo ya kubet yameanza kutaradadi nakumbuka kulikua na vi ofisi flan town ukipita unakuta watu wamejazana huko hadi wameunga foleni ukichungulia kwa ndani unaona maandishi yanayo wakawaka yanapita kwa juu hata huelewi ni nini. Una amua kuuliza unaambiwa watu wanacheza kamari. Duh, kusikia kamari unachanja mbuga maana kwa wakati ule neno "kamari" lilikua linaogopesha sana sio kama saivi.

Basi bhana, nikawa naishia tu kuangalia kwa mbali. Miaka ikasonga, betting ikazidi kukuwa, makampuni yakaanza kuongezeka, mpaka ikafika mahali karibu kila siku nikiwa kwenye mgahawa nakunywa chai siachi kuona washkaji wana vikaratasi vyeupe virefu (nilikuja kujua baadae sana vinaitwa mikeka).

Punde si punde nikaanza kusikia story za fulani kavunja Milioni kadhaa, fulani kavunja laki kadhaa, Daah. Katamaa kakaanza ku beep kwa mbali. Nikasema kwani nini mbaya kujua hii michezo inachezwaje acha niulize kidogo.

Mwana akanielewesha kuhusu hiyo michezo sema binafsi nikawa interested zaidi na betting ya soccer. Kwa sababu niliona ina uwazi. Mpira hauna longolongo, timu ikishinda kila mtu anajua kwa hiyo si rahisi kutapeliwa.

Muda ukaenda, story za watu kuvunja hela zikawa zinazidi kuwa nyingi. Ikafika mahali nikawa kama naanza kujiskia vibaya. Naona kama ni mimi peke yangu tu ndio nimebaki sina hela. Walivyokuja Meridian na system yao ya online betting, dah nikajikuta na mimi nimo ndani.

Duuh, kumbe nilikua natamani kubet sema nilikua naona aibu kuonekana hadharani. Sasa hii ya online najua hakuna mtu anaweza kunisanukia kama nacheza hata nikishinda ni siri yangu. Heheee! Sijawahi kushinda kitu! Hata mia! Kwaiyo maumivu yakawa ni ndani kwa ndani.

Betting ina addiction mbaya sana. Kwenye Bettng unajua umeanza kuwa addicted pale tu unapoanza ku chase loss. Yani pale unapoanza kuweka hela haraka haraka ili kurudisha pesa uliyopoteza. Nakumbuka kuna kipindi nilikua hadi nakopa pesa nabetia na inaliwa yote. Pesa ya kodi nabetia inaondoka yote. Kila mahali ni madeni. Halafu kibaya zaidi hata nikipokea hela kidogo kazini naona uzito kwenye kulipa yale madeni napata wazo la kuweka mkeka hata wenye odds 4 tu ili pesa ijae nimalize madeni yote kwa mara moja lakini wapi. Yote imeenda na maji. Nikawa depressed!

Walioniamini na kunikopesha wakaanza kuniona mtu wa ajabu sana, nafanya kazi napokea hela, silipi madeni ya watu kwa makusudi. Kumbe hela yenyewe ya kazi inaishia kwenye mikeka. Baadhi ya wadeni wangu wakachoshwa na sound zangu, wakaji organize wakaja ghetto wakabeba vitu hadi simu yangu wakapita nayo na bado wakanipa tarehe ya kumalizia madeni yaliyobaki la sivyo watanishtaki hadi kazini. Dah mambo ya aibu!

Nikaapa naacha kubet rasmi. Of course bado nilikua nataka kuendelea sema hata simu ya kubetia nilishanyang'anywa, na kwenda vibandani siwezi maana nafanya kwa siri. Nikapiga kazi mpaka nikamaliza madeni yote kwa kipindi kirefu sana. Na ki ukweli hakuna kitu kilikua kinaniumiza kama kulipia madeni ambayo sijafanyia kitu. Bora hata zile hela nilizokopa ningekua nimekula. Zote zilipotelea huko kwenye mikeka!

Muda ukaenda mpaka nikafanikiwa kununua simu nyingine ya smartphone. Siku moja napitapita huko Instagram, mara pap nakutana na mtu kashika bango la milioni 30 za Sportpesa, Daah vinyweleo vikasimama tena!

Nikasoma soma comments nikaona kama kila mtu anampa hongera nikaona hawa jamaa watakua legits, nikasahau yaliyonikuta huko nyuma nikaona nijiunge nao chap. Walikua na mchezo wao mmoja wanaita Jackpot, ukikosea mechi kidgo katika zote 13 wanakupa hela. Sa ngapi nisijaribu niotee 12. Duh Milion 10 na ushee hizi hapa. Nikaona kama ni utani.

Mara jamaa wakanipigia simu wakaniambia niende ofisini kwao wakahakiki taarifa zangu wanipe mpunga. Kweli nikafika nikamalizana nao, mpunga ukaingia kwenye account. Nikasema dah, elf mbili tu imenipa Mita 10. Maisha si ndio haya. Heheee.

Kilichonikuta na hizo Mil 10 ni story for another day!
Malizia mkuu, hivi kwanini hela za betting hua zinaisha kimiujiza miujiza?
 
Hapo lazima uka update mwili yani uchange damu nzima ili uanze maisha upya ila me nimeishi na mtu ambaye yakipita masaa kadhaa hawezi bila sigara sijui kwanini.
Noma mwanangu yabi unahisi huwezi fanta chochote bila stimu damu itembee bila hivyo unakua mgonjwa kabisa kimwili hadi kiakili
 
Noma mwanangu yabi unahisi huwezi fanta chochote bila stimu damu itembee bila hivyo unakua mgonjwa kabisa kimwili hadi kiakili
Hapo kujulikana mkiwa ugenini ni rahisi sana na hilo ndilo linakup wakati mgumu sana
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Umesoma muhas? Hii story ni km ilitokea pale
 
Siku niliyokamatwa napiga punyeto na bro:

Wakati nipo shule o-kevel hakuna kitu nilikua nakichukia kama club za masomo. Nakumbuka ilikua kila alhamisi, kilichokuwa kinanifanya nisipende ni maswali mengi kutoka kwa walimu na viongozi wa club husika yaani unapigwa maswali mbele ya madogo na ukikosea kujibu full aibu.
Basi wakulungwa wengi tulikua tunajazana kwenye club za michezo na fema. Mimi nilikua napenda fema coz ya mada nyingi ni za ujana. kule ndo nilipopata ujuzi wa kupiga punyeto. Wale jamaa walikuwa wanagawa na magazeti yao ambayo ndani wanasema njia mojawapo ya kujikinga na ukimwi ni ngono salama mojawapo ni punyeto a.k.a. selfee.

Basi bwana nilikua na mshkaji wangu anaitwa yaseen, huyu bwana anajua stye zote za punyeto na utamu wake, mara akwambie nyingine unapita mkao wa kukata gogo, nyingine unapiga umelala chali na ukikaribia kumwaga unapanua miguu unaanza upya. Hizi style zake zilinikosha kinoma. Huyu bwana alitoa ahadi siku akija kununua pc kitu cha kwanza atajaza video za x mtupu coz ndo starehe yake. Sitasahau kuna siku alikuja geto kuchek x kwenye pc ya bro mvua ikaanza kunyesha akalazimika kutoka hvohvo na mvua kisa anawahi kudowload ( kukumbuka) kabla muda haujapita ili asisahau akadai ili punyeto iwe tamu.

Kupitia huyu jamaa ndio nilikuja kujua kuwa kuna mshkaji wetu alikua mtu wa dini kinoma tena kiongozi alipiga punyeto getoni kwake akazimia akakutwa na bro ake hajitambui, nilicheka kinoma, huyu jamaa tulizoea kumwita kakoba coz alifanana sana na mshkaji mmoja kwenye maigizo ya ITV ya kila jmoc usiku alikuwa anaitwa mjomba kakoba.

Pole pole na mimi nikaanza huu mchezo wa punyeto na full kuapply style za mskaji wangu yaseen the master. Siku zote nilizoea kupigia bafuni, nilikua na mtindo wa kuoga maji ya moto hata kama ni mchana, nyumbani walinishangaa kinoma, kumbe mimi nilikua na lengo langu. Maji ya moto nilikua nayamwagilizia pale nnapokaribia kupiga bao + na lile joto la maji raha yake sio ya nchi hii. Hii style alinipa master wangu yaseen.

Basi bhwana chumbani nilikua nalala na bro sasa kuna siku bro alisema anaenda town nkakumbuka ndo mida sahihi ya kupiga puli coz pc ameiacha. Nkachukua cd yagu ya pilau nkaiweka nkaanza kuangalia baada ya mzuka kupanda nkachukua mafuta nkapaka kwenye mashine nkaanza taratibu kupiga punyeto, nilipata ujasiri wa punyeto ni salama hasa baada ya kushauriwa na fema club shuleni. Sasa ile utamu umekolea mara bro huyu hapa karud gafla na isitoshe mlango sikuufuga, aisee nilistuka balaa nachanganyikiwa nishike kipo nivae nguo coz nilivua zote au nizime pic, so nkabaki tu nimeduwaa sijui la kufanya. Daaah bro alimaind kinoma na isitoshe alikua ananiamini kinoma kila siku ananiona sio mtu wa mambo hayo . Bro ikabid aanze kunishauri kila siku kuwa mchezo huo sio mzuri. Moyoni nilimlaumu sana jamaa yangu yaseen coz alichangia pakubwa kwa mimi kuwa mpiga punyeto maarufu.

Kisa kinachofuata:
nilinusurika kufumaniwa na baba wakati nafanya mapenzi na beki tatu jikoni. Kalituona kadogo kamoja kakaja kusema sebuleni.
We nakupendekeza kuwa katibu wa Chama cha Bavicha
 
Habarini Ndugu zangu,

Hili sio juto lakini kama lingetimia basi lingekuwa juto la maisha yangu.

Nitakuwa short and clear.

Ilikuwa kipindi cha UE majira ya joto pale mkoa wa Chief Kingalu, ulikuwa ni mtihani wangu wa kujiuliza katika ukumbi mmoja maarufu sana pale chuoni ukifahamika kwa jina sawa na uwanja mkuu wa Mpira mkoa wa Iringa kama sikosei.

Lile somo lilikuwa ni tough kwangu na sikuwa nikilipenda. Dakika chache kabla ya kwenda kwenye mtihani nlikuwa na revise na jamaa yangu ambaye tuliongea tuweke kijiji au formation kwa ajili ya kupeana sapoti.
Yule jamaa alikuwa ni bingwa wa kubashiri maswali, basi akaandka majibu yake na solvings kwenye karatasi nusu ya A4 likiwa na maswali mawili na solvings.

Tumeingia kwa paper,tumekaa nyuma, jamaa kayakuta maswali yake mawili kama yalivyo, akayakopi kama yalivyo, kiufupi huyu jamaa yangu ni mzoefu wa hizi mishee. Advantage aliyokuwa nayo alikuwa amekaa katikati ilhali mie nikiwa nimekaa upande wa kulia mwishon ambako imepita njia na ngazi za kwenda floor ya juu (Kama unaujua huu ukumbi ushanisoma).

Nikaona nsije nikafa na kiu bwawani ,nikaomba anipasie mkeka nicopy chapu chapu huku nikitetemeka. Nimepewa ule mzigo nikpokea kwa mkono wa kushoto nikaukunja kwanza, nikacheki mazingira wasimamizi walipo, nikaona kupo safi lakini nikawa muoga kutoa mkeka pale chini ya dawati kuuweka juu.

Nikamuuliza jamaa yango oyaa vipi kupo safi, jamaa akawa hajibu yuko busy nikamuuliza tena akawa kimyaa.... Nikaona sio kesi nika spin jicho around kidogo nakutana na msimamizi yupo kwa juu ananicheki kwenye ngazi[emoji24][emoji24] nikaona hii ni soo mawazo ya kudisco yakanijiaa akilin mwangu.

Nikaona isiwe kesi ntapambaa kiume nikawa namlia timing aanze tu kushuka ili nitupie mdomoni ,wakati huo mkono wa kushoto unafinyanga kile ki mkeka. Ile anaanza tu kushuka ngazi mie nikatupiaa mdomoni fasta nikatafuna. Jamaa ameshuka amekaa nyuma yangu, akaangailiaa [emoji28][emoji28][emoji120] akaenda upande wa kushoto kwangu akasogea mbele yetu akawa anatuangaliaa akapotezeaa[emoji23][emoji120][emoji120].

Aiseeee ilikuwa ni furaha sana ,kwa ule muda nlikuwa nimewaza naanzaje kusema nyumbani nimekamatwa na cheat kwa paper na sijawahi fanya huu upuuz maisha yote ya shule, aibu yake mtaani, nitaambia nn jamaa zangu rafiki je,..

Msala ukaendeleaa ,wakati ameenda mbele basi akaja msimamizi mwingine, huyu msimamizi mwingine ni jamaa yetu kamaliza chuo pale madarasa ma2 mbele yangu, nlifahamiana naye kwenye tour moja ya kwenda Uluguru Mountain.

Akaja nyuma yangu akawa anaongea na jamaa aliyeko nyuma yanguu, [emoji23][emoji23] nikasema akitoka huko akija anisemeshe basi nimeisha maana nina karatasi mdomon, huwez kulimeza kwa ukubwa wake nitakabwa... Nikawaza nilimeze?? Je nikimeza afu nikabwe sindiyo nitaita attention ya msimamizi ajue shida nn, je vipi akija akute nimekabwa na karatasi mdomoni.... Nikasema simezi kama mbwao iwe mbwai huyu jamaa yangu hawezi nifanyia roho mbayaa...

Mungu sio Benedicto jamaa akanipitaa akaenda zake mbele, nikatoa karatasi nikaweka kwenye sockis huku nikijawa na furaha sana [emoji23][emoji23][emoji120] Nlimshukuru Mungu na kuapa sitorudia kuomba mkeka chumba cha mtihani.

Asante sana sir Mchaki najuaa ulinisevu sana, lile tukio uliliona ukanisevu mdogo wako
 
Haaaaah haaaaah nmecheka balaa hapo ni Samora Mimi ilinikuta mule OC haaaaah madogo Ma TA walininasa sitakuja kusahau
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Duuu bro kama nakuona kama najiona mpk nimekuhurumia,nikajihurumia pia,anyway wewe ni mwanaume hakuna ambae angeruka huu mchongo tena mweeeupe,hata mie nisengeruka hakika
 
Back
Top Bottom