Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Najutia siku nilikua airport mtu akaomba nimsaidie kubeba mzigo kuleta Dar nikapewa mlangoni, kumbe ilikuwa ni poda. Shukuru kipindi iko airport hawajaweka scanner ya wanaofika.
Hii ishanikuta nikiwa nchi moja ya Asia...jamaa mmoja mnigeria ananiambia nisaidie kumpelekea mzigo yule kaka pale ndani. Wakati napokea niksikia sauti inaniambia usikubali kupokea kitu chochote unakuwa unacheck in...ghafla nikakimbia
 
Nilimpenda mdada Fulani hivi advance, lakini kutokana na maisha yangu ya UTAWA[emoji1] nikaona nikomae na yangu nisijue ya Leo sio ya Jana.

Miaka ikaenda, tukamaliza shule bila kumuambia lolote, bila kujua tukaenda college Moja, ilikuwa ni Furaha siku nimeonana nae, hug za kutosha Hadi watu wa pembeni wakawa nashanga, ye alikuwa na mwenzie namie nlikuwa na jamaa angu. Maisha ya college pia sikumwambia lolote but tulikuwa karibu sana kama wapenzi. Room kwake naenda nakaa Hadi night kucheki Korean series etc,

Yule Binti alimaliza mbele yangu, Siku hiyo nipo kwa Mji wa Mkapa nikaona nimtolee uvivu nikamfungukia ukweli wote, Binti akawa anashangaa Kwann sikumuambia mapema had muda ule na alikuwa Hana mtu, akanipea polee lakini akawa tayari na mtu wake. Japo naye alikuwa anahisia namii baada ya ku confess, nikaona sio uungwana kuingilia mahusiano yake na jamaa wake wa sasa, nikaachana nae japo tunaishi kama wapenzi.

Nlichojifunza ukimuelewa mtu usikawie kusema, mwambie akatae mwenyewe na kujifanya unaogopa tongoza kuhofia utapoteza urafiki wenu nimejua ni ujinga.
"A man who hangs around a beautiful girl without speaking his intention ends up fetching water for guests at her wedding," an African proverb
 
Kuna ujinga wa kupita njia ya mkato niliufanya ukaja kuniharibia heshima.

Nilikosa Credit moja tu ili nipate sifa ya kupata nafasi ya Chuo. Kuna rafiki yangu akanisaidia nikapata cheti feki ambacho kilibadilishwa herufi moja tu C badala ya D ya Physics. Kikanisaidia kupata nafasi ya Masomo pale Muhimbili.

Baada ya kumaliza Chuo nilifanya ujinga wa kukitumia kile cheti feki kuombea kazi Serekalini badala ya kukitumia kile halisi. Sasa nikiwa kazini baada ya miaka mitano kazini nilichaguliwa kuwa mfanyakazi bora. Siku ya Mei mosi ambayo JPM alikuwa ndio mgeni rasmi, ilikuwa yeye ndio anikabidhi zawadi ya ufanyakazi bora ndio siku hiyo aliyotutumbua jipu. Aisee!.
 
Aisee!! pole sana
 
Mimi naenda direct najua hata nikitaja shule wengi wamesoma pale, hii ni story ya kwanza.

Nilisoma shule moja inaitwa Shybush au Shinyanga sec, niliingia kidato cha pili msala ukatokea wananzengo wameiba bomba, Hp akakusanya wanafunzi nakwenda sehem inaitwa maganzo ambapo hapohapo na mimi nilikuwa sijui kama wameenda huko maana walikusanyana baadhi wengine tulikuwa hatujui basi sikuiyo namimi nikasema acha niende huko maganzo eeeebwanawee sinikakutana nao alafu huyo Hp alikuwa na misuli balaa si akanilazimisha nijiunge nao.

Basi baada yakujiunga nao na kusaka bomba tukalikosa maana hapo shuleni hatukuoga almost wiki hivi, basi Hp akaanza kupiga sim shule nzima ije ikichafue maganzo maana si unajua wanafunzi walivyo wakorofi? Duh! Hao wanafunzi wakagoma kwenda maganzo aisee Hp alikasirika wakati tunarudi tukaambiwa tuvae kininja tuchume bakora tukawachape waliobaki shuleni [emoji24][emoji24], masikini wengine walikiwa ni walemavu, aisee walichezea kichapo si cha polepole.

Kesho yake ukawa ni msala maana wengine walilazwa, wengine walivunjika vidole vya miguu, tukaitwa parade nakuambiwa tupige kura walioshiriki aisee nilianza kutetemeka huku nikijisemea si nimo kwenye huu msala? Dah! Bahati nzuri sikuwemo aisee niliponea tundu la sindano na walio gundulika wamefanya hivyo walifukuzwa shule aisee.

Pole sana, HP wako Gwamaka wa Simba Dormitory. Mlitutesa sana ule usiku[emoji3]
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa nyumbani hautoshi kabisa.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules.

Sem ya kwanza ikaisha, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakasonga.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau, na ndio hapo unapoingia mtegoni unadakwa na kila kitu kinakua kichungu.

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
We utakuwa my college mate maana huo msala ulimkumba jamaa tukiwa chuoni
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.

Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
[emoji28][emoji28][emoji28]

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi nishushe kisa changu

Form 6 kipindi hiki 2015 shule moja maarufu sana huko kaskazini mwa nchi kipindi cha campaign kijana nina mzuka na siasa huniambii lolote kwa lowassa. Kijana mpenda mabadiliko chadema ndani ya damu.

Mwezi wa 10 tukiwa shule ikaonekana kwamba shule nidhamu ni 0.
Umalaya kati ya wanafunzi kwa wanafunzi ndo balaa.
Wanafunzi wanaishi mtaani wamepanga.
Wanafunzi wanakunywa pombe.
Wanafunzi walikuwa wana tabia zote mbovu.

Kwa akili finyu walimu wakaona tatizo ni wanafunzi so wakaunda kamati ya kufatilia na kumaliza tatizo la nidhamu.

Mimi kwa upande wangu nilikuwa nna matatizo yafutayo
1. Umalaya
Kwa vile nilikuwa alevel nilikuwa nawatia watoto wa olevel kwenye msitu wa shule kama sina akili nzuri.

2.UTORO
nilikuwa mtoro.shule ilikuwa jiran na home so nilikuwa nalala home.

Ukichangia na mzuka wa siasa wazo la riots likanijia.
Siku ya nuksi ikafika..
Ile kamati ikapelekewa majina ya wahuni wote wa shule.
Nikiwa na uhakika na mimi jina langu halikosekani coz nilikuwa natoroka kwa uwazi kabisa.

Siku ya 1 wanafunzi wenye shida wakaitwa kwenye kamati wakafukuzwa shule bila hata kujitetea.

Siku ya pili zoezi lilikuwa linaendelea na aura yangu ilinionyesha hiyo siku sitopona.
Nikawa nimechanganyikiwa.

So siku hiyo nikawa nimesurika.
Usiku tukiwa hostel tunajadiliana inakuwaje sasa mbona wahuni wanafukuzwa..
Sisi wenyewe hatujui kama tutabaki.
Mshikaji wa Senzo akaja na wazo bora zaidi kuwahi kulipokea.

HIVI KWANINI NA SISI TUSIANZISHE RIOTS KWA KUELEZA TABIA MBOVU ZA WALIMU

WALIMU WALIKUWA WAHUNI KULIKO HATA WANAFUNZI.
Tena ndo walikuwa malaya kupitiliza.

Basi mshikaji alivyoleta hilo wazo zikaletwa rim paper tukaanza kuandika changamoto za walimu zote.
Vile vipeperushi tukavisambaza shule nzima usiku huo huo.
Kwenye kipeperushi tulikuwa tunaandika jina la mwalimu na denti anayemla.

Tulionyesha pia tabia zingine za walimu kama uvivu wa kutoingia class etc.

Nikasambaza vipeperushi vyangu kote. Then nkasepa zangu nkaenda home kulala.

Saa 11 mlinzi kashtuka akaviokota vyote akapeleka kwa headmaster.

Mimi saa 2 nkafika skul sina stress wala ikabidi form 6 tuitwe kikao cha dharura.

Ile kamati ikavunjwa ikabidi sasa msala uhamie kwa walimu. Na hapo msala wetu ukawa umeisha

Ninachojutia ni kwamba kuna walimu zaidi ya 5 walipoteza kazi hiyo siku. Coz wale wanafunzi walivyoitwa walikiri kuwa wanatiwa na hao walimu mbele ya kamati.
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.

Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Ungewapa ule mstari wa biblia wa samehe saba mara sabini.

Ila ni ngumu kufuatisha maneno ya vitabu hadi Sista kashindwa?
 
Na mimi nishushe kisa changu

Form 6 kipindi hiki 2015 shule ya mkuu sec kipindi cha campaign kijana nina mzuka na siasa huniambii lolote kwa lowassa.

Mwezi wa 10 tukiwa shule ikaonekana kwamba shule nidhamu ni 0.
Umalaya kati ya wanafunzi kwa wanafunzi ndo balaa.
Wanafunzi wanaishi mtaani wamepanga.
Wanafunzi wanakunywa pombe.
Wanafunzi walikuwa wana tabia zote mbovu.

Kwa akili finyu walimu wakaona tatizo ni wanafunzi so wakaunda kamati ya kufatilia na kumaliza tatizo la nidhamu.

Mimi kwa upande wangu nilikuwa nna matatizo yafutayo
1. Umalaya
Kwa vile nilikuwa alevel nilikuwa nawatia watoto wa olevel kwenye msitu wa shule kama sina akili nzuri.

2.UTORO
nilikuwa mtoro.shule ilikuwa jiran na home so nilikuwa nalala home.

Siku ya nuksi ikafika..
Ile kamati ikapelekewa majina ya wahuni wote wa shule.
Nikiwa na uhakika na mimi jina langu halikosekani coz nilikuwa natoroka kwa uwazi kabisa.

Siku ya 1 wanafunzi wenye shida wakaitwa kwenye kamati wakafukuzwa shule bila hata kujitetea.

Siku ya pili zoezi lilikuwa linaendelea na aura yangu ilinionyesha hiyo siku sitopona.
Nikawa nimechanganyikiwa.

So siku hiyo nikawa nimesurika.
Usiku tukiwa hostel tunajadiliana inakuwaje sasa mbona wahuni wanafukuzwa..
Sisi wenyewe hatujui kama tutabaki.
Mshikaji wa Senzo akaja na wazo bora zaidi kuwahi kulipokea.

HIVI KWANINI NA SISI TUSIANZISHE RIOTS KWA KUELEZA TABIA MBOVU ZA WALIMU

WALIMU WALIKUWA WAHUNI KULIKO HATA WANAFUNZI.
Tena ndo walikuwa malaya kupitiliza.

Basi mshikaji alivyoleta hilo wazo zikaletwa rim paper tukaanza kuandika changamoto za walimu zote.
Vile vipeperushi tukavisambaza shule nzima usiku huo huo.
Kwenye kipeperushi tulikuwa tunaandika jina la mwalimu na denti anayemla.

Tulionyesha pia tabia zingine za walimu kama uvivu wa kutoingia class etc.

Nikasambaza vipeperushi vyangu kote. Then nkasepa zangu nkaenda home kulala.

Saa 11 mlinzi kashtuka akaviokota vyote akapeleka kwa headmaster.

Mimi saa 2 nkafika skul sina stress wala ikabidi form 6 tuitwe kikao cha dharura.

Ile kamati ikavunjwa ikabidi sasa msala uhamie kwa walimu. Na hapo msala wetu ukawa umeisha

Ninachojutia ni kwamba kuna walimu zaidi ya 5 walipoteza kazi hiyo siku. Coz wale wanafunzi walivyoitwa walikiri kuwa wanatiwa na hao walimu mbele ya kamati.
Hongereni sana, "dawa ya msaliti ni kifo "hao walimu walikuwa wasaliti kwa wahuni wenzao.
 
Hii ishanikuta nikiwa nchi moja ya Asia...jamaa mmoja mnigeria ananiambia nisaidie kumpelekea mzigo yule kaka pale ndani. Wakati napokea niksikia sauti inaniambia usikubali kupokea kitu chochote unakuwa unacheck in...ghafla nikakimbia

Yaah ukizubaa unabebeshwa sembe
 
Back
Top Bottom