Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kuna wale wajinga wanachezesha bahati nasibu utakuta wamefunga jukwaa wamejaza tv, redio, pasi nk, washenzi saana, naleta kisa soon
Hahahaha Mbwa kabisa na Mimi sitokuja kuwa sahau hao mahayawani

Nilikuwa Mwanza kipindi hicho katika pitapita zangu nikawakuta maeneo, kosa nililofanya ni kusimama kuangalia nafsini mwangu nilikuwa nimejiapiza siwezi cheza michezo yeyote ya kamali wala bahati nasibu, nikajisemea sifa ya macho kuona ngoja nione mchezo unaendaje

Hili likawa kosa kubwa ninalo jutia hadi kesho, sikupanga kucheza nilitaka tu nione then niendelee na issue zangu, sasa wakati bado naangalia kuusoma vizur mchezo si akaja Mama hivi wa makamo akanunua ticket zao zile akacheza akashinda hela na tickets (card), akaambiwa Mama umshinda ticket kadhaa na hela, akapewa hela na ticket aendelee kucheza tena Mama akagoma wakati huo Mimi nilikuwa pembeni yake na jamaa mwingine hivi ambaye pia tulikutana hapo

Yule Mama akachukua hela halafu ananipa Mimi na yule jamaa ticket (card) kwa kuwa card tulipewa bure na Yule Mama ikabidi nikubali kucheza kwa msisitizo toka kwa jamaa ambaye tulipewa wote card na yule Mama, nikaona sio issue as long as sichez kwa hela yangu ni card za offer ngoja nicheze

Mchezo wenyewe huko hivi, unanunua card ambazo ukigeuza kuna kuwa na number kwa hiyo unaangalia card yako inafanana na number gani kati ya number zilizowekwa juu ya vitu (generator, TV, pikipiki, hela n.k)

Sasa nilipoichukua ile card nikaingia kwenye mchezo, kuoanisha ile number na vile vitu vyao nikawa nmeshinda kama elfu 15 hv na nikawa nmeshinda pia card nyingine 3, kweli wakanipa elfu 15 niliyoshinda na
 
Ziwani siwezi kudhubutu. Maana sikua vizuri kwenye kuogelea halafu kulikua na story kuwa lile ziwa lina Mamba!
Tunezama sana huko ziwani sema ukijulikana ndo utajua hujui yaani [emoji58][emoji58][emoji58][emoji58]
 
Kisa cha pili .....

Nikiwa nimemaliza form six , basi ikabidi nitoke dar niende kagera kumsabai bibi yangu , Bibi yangu alikuwa akiishi bukoba mjini mitaa ya town kabisa.

Sasa pale kwake alikuwa na vyumba kama kumi na nne, amevipangisha , hivyo ni kawaida mimi kuonana na wapangaji pindi nitokapo ndani .

Sasa katika wale wapangaji kuna mdada alikuwa amepanga na pia anaishi mwenyew tu , ila story za watu eti ni malaya na pia ameathirika na gonjwa la taifa .

Hata bibi aliniambia hivyo pia , ila siku zilivyozidi pale nyumbani Mazoea na wale wapangaji yalizidi , sasa yakawa yamezidi kwa huyu dada, anayeishi pekee yake , Bibi akaendelea kunikanya kuwa niwe mbali na huyo binti , kwanza kanizidi umri pia ana tabia za umalaya .

Dah shetani , msikie tu , si nikajikuta nishaingia kwenye mazoea na yule dada , mwisho nikawa usiku nafungua geti taratibu naenda nalala kwake, asubuhi na mapema narudi, maisha yakawa safi , ila moyoni nikawa sina amani tena maana nilikuwa napiga kavu , hivyo nikawa najua nishaathirika .

Penzi likanoga kwa siri , Bibi hajui kitu kuwa mjukuu nishaingia kwenye penzi la mpangaji japo baadhi ya wapangaji walijua.

Sasa usiku mmoja kulikuwepo na mechi ya Arsenal na man u , nikamueleza bibi naenda mpirani akasema hapana, si uangalizie hapa , nikagoma akakubali niende atanifungulia mageti.

Sasa kumbe mwenzake sina mpango wa kurudi nyumba kubwa nataka nilale na mchuchu wangu , dah kweli baada ya mechi nilikuwa very frustrated sababu chama langu , man u tulikula nyingi .

Nikasema Ngoja nikamalizie hasira kwa mpangaji wetu bila kuwaza kuwa tayari nina ngoma toka kwake , lahaura , kumbe masikini mbibi wa watu hajalala anawaza mjukuu wake mbona harudi ?

Mida ya saa saba nikasikia mlango wa nyumba kubwa umefunguliwa mda huo nipo juu ya kifua cha dada mpangaji , sasa nikawaza mda huu bibi anatafuta nini ?kumbe mbibi hajalala anamuwaza mjukuu wake , saa ngapi asimgongee mpangaji mmoja hivi amuulize wapi tunaangaliziaga mpira , mda huo nawasikia.

Mara ghafla nikawa siwasikii tena , kumbe yule mpangaji kauza ramani ya vita , kamchana bibi kuwa mpira ulishaisha ila anadhani nitakuwa chumba cha dada mpangaji maana uwa ananiona naingia usiku .

Bibi wa watu , upendo kwa mjukuu ukamzidi uwezo akagonga hodi kwenye chumba chetu, mdada akaanza kutetemeka ni nini afanye, mimi nimeinama nawaza aibu , naiweka wapi?

Mara mdada kafungua mlango , Bibi kaingia anafoka kwanini unataka kumuua mwanangu , mara akague huku mara kule, muda huo nimejificha kwenye vyombo , Bibi aliponiona akaanza kumpiga mdada na ndala kwanini unataka kumuua mwanangu, akitamka hivyo , mdada alivaa kanga tu , mara akakimbia nje

Mda huo nimevaa boksa na shati tu , Bibi alivomfuata nikavaa suruali Chapu, nikavaa sendo nikatoka nakimbia huku aibu , maana watu wameamka ili kuona ni nini kimetokea.

Nikawaza sana njiani sijui wapi naelekea mwisho nikasema siwezi kufa kizembe, nikaenda moja kwa moja mpaka sitende ya mabasi ya mkoani , pale nikakuta kama mchana hivi , fasta nikauliza kama naweza mpata wakala wa mpesa , nikampata.

Nilitoa elfu themanini, maana ilikuwa kwenye simu , nikakata tiketi kwa elfu hamsini na tano , bukoba kwenda dar , baada ya kupewa hela na nikaoneshwa basi, nilienda mle nikakaa nawaza mengi mpaka najionea aibu mwenyewe mda huo , Bibi anapiga simu sipokei mara nikazima.

Nilifika dar baada ya safari , nikakuta bibi alipiga simu anasema hajui alimuudhi nini mjukuu wake maana amekimbia nyumbani hayupo na hajaaga , dah bibi bwana ila hakusema nimefanya nini ?

Dah nilivoambiwa hivyo , nilijikuta nalia tu , nikaishia kusema nilimiss kurudi dar tu , ila moyoni najua bibi aliamua kuvunga ila baada ya siku kadhaa bibi , alinitafuta akanisihi nisirudie hiyo tabia na pia akaomba niende nikapime UKIMWI , alafu nimpe majibu , kweli nilipima nikajikuta negative .

Dah nilipomwambia bibi alifurahi sana , mpaka nikamsikia analia kwenye simu Ila yule Demu sikumtafutaga tena .

Dah bibi yangu mpaka leo ananipenda sana na hajawahi kunitobolea siri hii

Dah wewe mdada kama uko humu nisamehe bure ulikuwa ujana ndiyo maana sijawah kukutafta
Hiyo mitaa itaku2a Kashai mafumbo [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] pole sana jamaa! Na hukawii kukuta ulikuwa waangalia na mimi pale Kashai Centre au pale kwenye ukumbi wenye kaghorofa kwa juu [emoji52][emoji52][emoji52][emoji52][emoji52]
 
Inasikitisha sana , kosa siyo lako ila ukapewa adhabau wewe. Ila msamehe mama wanapitia mambo mengi sana magumu.

Kutoka moyoni kabisa nimemsamehe.. kabsa kabsa wamama wanapitia mengi sana pamoja na utemi wa wababa; pengine alikuwa na mgao kwenye pesa ilee na wao hawakutaka kumpa chochote.. wakaona wanipe msala mimi.. daah
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
Tubu aisee..
 
Kutoka moyoni kabisa nimemsamehe.. kabsa kabsa wamama wanapitia mengi sana pamoja na utemi wa wababa; pengine alikuwa na mgao kwenye pesa ilee na wao hawakutaka kumpa chochote.. wakaona wanipe msala mimi.. daah
Ni kweli.Inauma sana ndio mana mpaka sasa mama bado kinamuuma hicho kitendo.
 
Hiyo mitaa itaku2a Kashai mafumbo [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] pole sana jamaa! Na hukawii kukuta ulikuwa waangalia na mimi pale Kashai Centre au pale kwenye ukumbi wenye kaghorofa kwa juu [emoji52][emoji52][emoji52][emoji52][emoji52]
Anhaaa umenisoma vizuri baharia.
 
Nilibebeshwa mavi mkononi kwa sababu ya upole

Mimi ni mpole ila nilivyokuwa mdogo nilikua mpole kupitiliza ndo maana nilibebeshwa mavi ambayo sikunya mimi.

Kipindi nipo darasa la kwanza nilipelekwa boarding sasa hiyo siku tuko zetu tunacheza mida ya jioni akaja matron akatuita boys wote tulikua kama 30 hivi ambao tunakaa bweni na tulivyokusanyika akatuambia nifuateni tukaona anaelekea chooni basi tukamfwata tulivofika chooni ile sehemu ambayo ipo special kwa ajili ya haja ndogo tukakuta mavi yapo makimba matatu yamejipanga matron akauliza nani kanya hapa ina maana vyoo hamvioni mpaka mtumie sehemu ya haja ndogo nitajieni aliyekunya hapa.

Wote tulikua kimya mara ghafla kuna dogo mmoja mmasai anaitwa Lomnyaki akayasogelea yale mavi akayaangalia afu akanitaja akasema matron huyu Mafian cartel haya mavi yake kabisa yeye ndo kanya hapa mavi yake nayajua dah nilishangaa sana kumsikia Lomnyaki akinisingizia kosa ambalo sikufanya sijui alikua ana malengo gani kunichoma kwa matron

Basi Matron hakutaka maelezo akawaruhusu wenzangu waondoke akabaki na Mimi na kunihoji kwa nini nimekunya sehem ambayo siyo sahihi basi na Mimi na upole wangu ambao ulikua uboya nikawa nalia tu kwa kuonewa matron akasema wewe lia ila haya mavi uyazoe ukatumbukize Kwenye tundu la choo nikirudi nisikute mavi hapa afu akaondoka

Dah sasa nikabaki pale nahuzunika moyoni namlaumu Lomnyaki kwa kunichoma,basi nikachukua toilet paper nikaanza kuokota kimba moja napeleka kudumbukiza Kwenye tundu la choo nikachukua tena lingine hadi nikamaliza kuzoa makimba yote matatu kisha nikanawa na kumwambia matron nishamaliza kuzoa makimba yale.akasema sawa nenda ila usirudie tena.

watu walinicheka sana na kunitania pale shule mpaka Leo natafakari kwanini Lomnyaki alinichoma wakati mimi sihusiki labda yeye ndo aliyekunya n kuamua kuniuzia kesi

Mataccor yako Lomnyaki
Qmmke
 
Hahahaha Mbwa kabisa na Mimi sitokuja kuwa sahau hao mahayawani

Nilikuwa Mwanza kipindi hicho katika pitapita zangu nikawakuta maeneo, kosa nililofanya ni kusimama kuangalia nafsini mwangu nilikuwa nimejiapiza siwezi cheza michezo yeyote ya kamali wala bahati nasibu, nikajisemea sifa ya macho kuona ngoja nione mchezo unaendaje

Hili likawa kosa kubwa ninalo jutia hadi kesho, sikupanga kucheza nilitaka tu nione then niendelee na issue zangu, sasa wakati bado naangalia kuusoma vizur mchezo si akaja Mama hivi wa makamo akanunua ticket zao zile akacheza akashinda hela na tickets (card), akaambiwa Mama umshinda ticket kadhaa na hela, akapewa hela na ticket aendelee kucheza tena Mama akagoma wakati huo Mimi nilikuwa pembeni yake na jamaa mwingine hivi ambaye pia tulikutana hapo

Yule Mama akachukua hela halafu ananipa Mimi na yule jamaa ticket (card) kwa kuwa card tulipewa bure na Yule Mama ikabidi nikubali kucheza kwa msisitizo toka kwa jamaa ambaye tulipewa wote card na yule Mama, nikaona sio issue as long as sichez kwa hela yangu ni card za offer ngoja nicheze

Mchezo wenyewe huko hivi, unanunua card ambazo ukigeuza kuna kuwa na number kwa hiyo unaangalia card yako inafanana na number gani kati ya number zilizowekwa juu ya vitu (generator, TV, pikipiki, hela n.k)

Sasa nilipoichukua ile card nikaingia kwenye mchezo, kuoanisha ile number na vile vitu vyao nikawa nmeshinda kama elfu 15 hv na nikawa nmeshinda pia card nyingine 3, kweli wakanipa elfu 15 niliyoshinda na
Huyo mama Lao moja
 
Kisa cha nne .....

Mimi katika kisa hiki najuta sana na pia naumia sana kwa yote niliyoyasababisha kwa jamaa yangu

Nikiwa chuo mwaka wa tatu , kuna bro tulizoeana sana mpaka kiasi cha kuamini nisipo mimi yeye hayupo japo alikuwa mwaka wa mwisho ila bado tulibond vizuri mno .

Kaka huyu alikuwa ni mtu kutoka Geita, lakini mpaka nafahamiana naye , hakika niligundua alikuwa ni wale watu wa masomo na yeye si mtu wa kusema azunguke aujue mji kidogo au ajichanganye ila alikuwa anapenda sana kubeti .

Sasa kubeti ndiyo kulifanya urafiki wetu ukafana sana , na hapa ndiyo wale wakuitwa wahenga wanasema.....ndege wafananao huruka pamoja, basi bro yule akajikuta ameanza kunifuata kwa kila tabia niliyokuwa nayo, mpaka wale wanaojikuta wanasomeshwa na kijiji, daily wanamshauri huyu jamaa hafai kuwa rafiki yako anakupoteza .

Walikuwa wanamshauri haya maana niliwahi zinguana na lecturer sababu ya uonevu aliotaka kunifanyia hivyo habari zikawa zinasambaa na vile nilikuwa nahudhuriaga kwenye kumbi za starehe around hapo chuo basi waliniona mimi ni mhuni sana na sio wa kuwa na rafiki aliyeserious na masomo vile.

Ila jamaa hakuwasikiliza maana alijua in deed sina uhuni kihivyo maana hata pombe sinywi ila ni vile rafiki zangu ni wahuni , ukizingatia nasoma chuo , nyumbani.
Basi jamaa taratibu akaanza naye kupenda kununua vidada Poa sehemu tofauti tofauti kama mimi nilivyokuwa nafanya, yeye alikuwa amepanga geto keko, hivyo mida fulani nikiwaga na time nilikuwa namuibukia tunabeti kama kawaida na tukishinda basi tunaingia viwanja kuwacheki 2watoto wazuri.

Dah nikaja kustuka jamaa angu ashakuwa mlevi, sasa sikuwahi jua alikuwa mlevi kabla au la?
Mara ya kwanza kujua ni mlevi tulienda kuopoa dada poa , mida ya saa saba baada ya UEFA MATCH kuisha usiku huo, tulikuwa na mkwanja mzuri , tulienda maeneo ya LIQUID pale uhasibu , basi kabla ya kuchagua wadada akasema tukapoze koo ikawa hivyo akaagiza pombe na akazipiga nikasema bro keshakuwa chapombe

Maana alilewa sana kiasi cha mimi kuanza kuhangaika usafiri na Demu niliyemnunua ili twende guest wakati huo hajiwezi na ilibidi nimchukulie room bila Demu maana asingeweza kufidia hela tutakayomlipa Demu.

Basi maisha na bro hakika yalifana hayupo geto kwangu basi nipo kwake, maisha yakendelea na utaratibu ni ule ule , ni mwendo wa bata na kula nyapu za dada poa bila kujali ni wala nini.

Siku moja jamaa yangu aliniita niende keko maeneo ya DDC ili tupate kupoza koo japo mimi si mnywaji zaidi ya soda na misosi na kuopoa basi
Sasa mida ya kufika pale alisema nifike saa nne usiku ili twende bar moja inaitwa KING PALACE , maana ilikuwa siku ya jumamosi akadai siku hiyo kunakuwaga na watoto wakali.

Pasipo kumpotezea time mwanangu , saa nne nilikuwa pale nikamcheki kwa simu chap na haraka akatokea maana geto kwake haikuwa mbali na pale , maana aliishi karibu na GEREZA LA KEKO , pale ,kweli tukazama KING PALACE taratibu bro akaagiza vinywaji vyake na mimi nikaagiza misosi na soda , tukaendelea kuburudika.

Mara nikamuona kimwali nikasema bro mimi naishi na huyu leo , maana walikuwa wanazama mle ili kutafuta wateja, nikamsoundisha mrembo akajaa bei na guest tukakubaliana na akanipa kampani japo yeye ni wa vinywaji vikali, hela ikatoka akaendelea kuishi na sisi.

Baada ya mida kidogo naye bro akaendea akaopoa akarudi na malkia wake, naye tukaungana naye kwenye burudani mara tucheze muziki kidogo mara tupigane busu na malaya wale .

Dah laiti ningejua ilikuwa ni siku naenda kumpoteza rafiki yangu that night ningeondoka mapema tu .
Basi mida ya saa nane tukachomoka pale tukaelekea guest fulani ambazo ni kama unaingia keko ndani kidogo , sehemu inaitwa keko torori, basi kila mtu akaendelea na malaya wake mambo mengine vyumbani.

Asubuhi mida ya saa kumi na moja , malaya wangu alihitaji kuondoka nikamruhusu sasa baada ya kuondoka naenda chumba cha bro kumcheki simkuti ila nilikuta vitu vya ndani kama kitanda na visturi vimekaa kama kuna vurugu ilitokea, dah nikawa na mawazo sana , ikabidi niende mapokezi ili niulize kuna nini na jamaa yangu mbona simuoni?

Mapokezi walinijibu mbona huyu jamaa alichukuliwa usiku na wahuni fulani eti amaemchukua Demu wao, dah pale nikawaza sana , ukizingatia keko kipindi hiko si pema sana kwa watu wake , nikawa nawaza tu jamaa angu awe mzima tu , mengine yanasolvika.

Nikatoka pale guest mpka getoni kwake nako wanasema hawajamuona toka jana usiku na chumba kimefungwa.
Nikawa na mawazo sana kwenda chuo kutoa taarifa nasita pia naona aibu nitasema tulikuwa wapi usiku wake mpaka niwe na mashaka hivyo.

Ikabidi niende geto nikapumzishe kichwa kwanza , lahaura , nafika kituo cha polisi ambacho kipo karibu na kituo cha magari pale DDC ndiyo nakuta watu wengi , wamejikusanya pale eti kuna mtu ameuwa amekutwa keko _magurumbasi, hiyo ni mida ya saa mbili kasoro, dah kuulizia alivaaje nikajua ni bro ndiye kauwawa, mara difenda ikaondoka pale kumpeleka _temeke hospitali, niliumia sana tena sana .

Sasa uchunguzi ukaanza na chuo wakawa wananiuliza sana mimi maana nilkuwa close sana ila ilibidi niseme sijaonana naye toka jana hivyo sijui ilikuwaje maana hata simu zangu , siku iliyopita hazikupokelewa na pia nilienda kwake pia ila bado sikumkuta.

Nilihojiwa pia na polisi ila bado sikubatilisha maelezo, mwisho msiba uliendelea na akasafirishwa na chuo mpaka kwao nilienda pia msibani ila ilibaki kuwa hatia moyoni mwangu .
Kila nikikumbuka uwa najutia sana

All in all rest in peace banzoka .
Daaah [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Nilimpa demu wangu wa utotoni li baruti fulani lenye muundo wa mshumaa nikamdanganya kuwa ukiwasha kale kautambi zinatokea rangi nzuri aisee si akaenda nalo moja kwa moja hadi kwao akaingia jikoni ambapo wapangaji wote hupikia humo na mama yake yupo humo anapika si akaliwasha bwanaaa weeeee LIKAJIBU PWAAAAA kmmke daa wengine walizimia na kulazwa include mama yake ila mmoja aliruka mripuko uliposikika akatua kwenye maji ya moto.Jamani navyoongea hivi kuna mtu ana jeraha lilosababishwa na ujinga wangu MUNGU NISAMEHE.Mi baruti tuliipata kwa dada yangu ambae alikuwa anafanya kazi kwa WaINDI sio jambo la kujisifia ila kilichonikuta baada ya hilo tukio mixer na mapolisi waliingia mama yangu haelewi kwa nini nimekuja kukamatwa aisee.
[emoji23][emoji23]..wee jamaa nmecheka kifala yani , mpaka tumbo na mbavu zinabana
 
Hahahaha Mbwa kabisa na Mimi sitokuja kuwa sahau hao mahayawani

Nilikuwa Mwanza kipindi hicho katika pitapita zangu nikawakuta maeneo, kosa nililofanya ni kusimama kuangalia nafsini mwangu nilikuwa nimejiapiza siwezi cheza michezo yeyote ya kamali wala bahati nasibu, nikajisemea sifa ya macho kuona ngoja nione mchezo unaendaje

Hili likawa kosa kubwa ninalo jutia hadi kesho, sikupanga kucheza nilitaka tu nione then niendelee na issue zangu, sasa wakati bado naangalia kuusoma vizur mchezo si akaja Mama hivi wa makamo akanunua ticket zao zile akacheza akashinda hela na tickets (card), akaambiwa Mama umshinda ticket kadhaa na hela, akapewa hela na ticket aendelee kucheza tena Mama akagoma wakati huo Mimi nilikuwa pembeni yake na jamaa mwingine hivi ambaye pia tulikutana hapo

Yule Mama akachukua hela halafu ananipa Mimi na yule jamaa ticket (card) kwa kuwa card tulipewa bure na Yule Mama ikabidi nikubali kucheza kwa msisitizo toka kwa jamaa ambaye tulipewa wote card na yule Mama, nikaona sio issue as long as sichez kwa hela yangu ni card za offer ngoja nicheze

Mchezo wenyewe huko hivi, unanunua card ambazo ukigeuza kuna kuwa na number kwa hiyo unaangalia card yako inafanana na number gani kati ya number zilizowekwa juu ya vitu (generator, TV, pikipiki, hela n.k)

Sasa nilipoichukua ile card nikaingia kwenye mchezo, kuoanisha ile number na vile vitu vyao nikawa nmeshinda kama elfu 15 hv na nikawa nmeshinda pia card nyingine 3, kweli wakanipa elfu 15 niliyoshinda na
Siti ya mbele kabisa nasubir mwendlezo
 
Back
Top Bottom