Kisa cha nne .....
Mimi katika kisa hiki najuta sana na pia naumia sana kwa yote niliyoyasababisha kwa jamaa yangu
Nikiwa chuo mwaka wa tatu , kuna bro tulizoeana sana mpaka kiasi cha kuamini nisipo mimi yeye hayupo japo alikuwa mwaka wa mwisho ila bado tulibond vizuri mno .
Kaka huyu alikuwa ni mtu kutoka Geita, lakini mpaka nafahamiana naye , hakika niligundua alikuwa ni wale watu wa masomo na yeye si mtu wa kusema azunguke aujue mji kidogo au ajichanganye ila alikuwa anapenda sana kubeti .
Sasa kubeti ndiyo kulifanya urafiki wetu ukafana sana , na hapa ndiyo wale wakuitwa wahenga wanasema.....ndege wafananao huruka pamoja, basi bro yule akajikuta ameanza kunifuata kwa kila tabia niliyokuwa nayo, mpaka wale wanaojikuta wanasomeshwa na kijiji, daily wanamshauri huyu jamaa hafai kuwa rafiki yako anakupoteza .
Walikuwa wanamshauri haya maana niliwahi zinguana na lecturer sababu ya uonevu aliotaka kunifanyia hivyo habari zikawa zinasambaa na vile nilikuwa nahudhuriaga kwenye kumbi za starehe around hapo chuo basi waliniona mimi ni mhuni sana na sio wa kuwa na rafiki aliyeserious na masomo vile.
Ila jamaa hakuwasikiliza maana alijua in deed sina uhuni kihivyo maana hata pombe sinywi ila ni vile rafiki zangu ni wahuni , ukizingatia nasoma chuo , nyumbani.
Basi jamaa taratibu akaanza naye kupenda kununua vidada Poa sehemu tofauti tofauti kama mimi nilivyokuwa nafanya, yeye alikuwa amepanga geto keko, hivyo mida fulani nikiwaga na time nilikuwa namuibukia tunabeti kama kawaida na tukishinda basi tunaingia viwanja kuwacheki 2watoto wazuri.
Dah nikaja kustuka jamaa angu ashakuwa mlevi, sasa sikuwahi jua alikuwa mlevi kabla au la?
Mara ya kwanza kujua ni mlevi tulienda kuopoa dada poa , mida ya saa saba baada ya UEFA MATCH kuisha usiku huo, tulikuwa na mkwanja mzuri , tulienda maeneo ya LIQUID pale uhasibu , basi kabla ya kuchagua wadada akasema tukapoze koo ikawa hivyo akaagiza pombe na akazipiga nikasema bro keshakuwa chapombe
Maana alilewa sana kiasi cha mimi kuanza kuhangaika usafiri na Demu niliyemnunua ili twende guest wakati huo hajiwezi na ilibidi nimchukulie room bila Demu maana asingeweza kufidia hela tutakayomlipa Demu.
Basi maisha na bro hakika yalifana hayupo geto kwangu basi nipo kwake, maisha yakendelea na utaratibu ni ule ule , ni mwendo wa bata na kula nyapu za dada poa bila kujali ni wala nini.
Siku moja jamaa yangu aliniita niende keko maeneo ya DDC ili tupate kupoza koo japo mimi si mnywaji zaidi ya soda na misosi na kuopoa basi
Sasa mida ya kufika pale alisema nifike saa nne usiku ili twende bar moja inaitwa KING PALACE , maana ilikuwa siku ya jumamosi akadai siku hiyo kunakuwaga na watoto wakali.
Pasipo kumpotezea time mwanangu , saa nne nilikuwa pale nikamcheki kwa simu chap na haraka akatokea maana geto kwake haikuwa mbali na pale , maana aliishi karibu na GEREZA LA KEKO , pale ,kweli tukazama KING PALACE taratibu bro akaagiza vinywaji vyake na mimi nikaagiza misosi na soda , tukaendelea kuburudika.
Mara nikamuona kimwali nikasema bro mimi naishi na huyu leo , maana walikuwa wanazama mle ili kutafuta wateja, nikamsoundisha mrembo akajaa bei na guest tukakubaliana na akanipa kampani japo yeye ni wa vinywaji vikali, hela ikatoka akaendelea kuishi na sisi.
Baada ya mida kidogo naye bro akaendea akaopoa akarudi na malkia wake, naye tukaungana naye kwenye burudani mara tucheze muziki kidogo mara tupigane busu na malaya wale .
Dah laiti ningejua ilikuwa ni siku naenda kumpoteza rafiki yangu that night ningeondoka mapema tu .
Basi mida ya saa nane tukachomoka pale tukaelekea guest fulani ambazo ni kama unaingia keko ndani kidogo , sehemu inaitwa keko torori, basi kila mtu akaendelea na malaya wake mambo mengine vyumbani.
Asubuhi mida ya saa kumi na moja , malaya wangu alihitaji kuondoka nikamruhusu sasa baada ya kuondoka naenda chumba cha bro kumcheki simkuti ila nilikuta vitu vya ndani kama kitanda na visturi vimekaa kama kuna vurugu ilitokea, dah nikawa na mawazo sana , ikabidi niende mapokezi ili niulize kuna nini na jamaa yangu mbona simuoni?
Mapokezi walinijibu mbona huyu jamaa alichukuliwa usiku na wahuni fulani eti amaemchukua Demu wao, dah pale nikawaza sana , ukizingatia keko kipindi hiko si pema sana kwa watu wake , nikawa nawaza tu jamaa angu awe mzima tu , mengine yanasolvika.
Nikatoka pale guest mpka getoni kwake nako wanasema hawajamuona toka jana usiku na chumba kimefungwa.
Nikawa na mawazo sana kwenda chuo kutoa taarifa nasita pia naona aibu nitasema tulikuwa wapi usiku wake mpaka niwe na mashaka hivyo.
Ikabidi niende geto nikapumzishe kichwa kwanza , lahaura , nafika kituo cha polisi ambacho kipo karibu na kituo cha magari pale DDC ndiyo nakuta watu wengi , wamejikusanya pale eti kuna mtu ameuwa amekutwa keko _magurumbasi, hiyo ni mida ya saa mbili kasoro, dah kuulizia alivaaje nikajua ni bro ndiye kauwawa, mara difenda ikaondoka pale kumpeleka _temeke hospitali, niliumia sana tena sana .
Sasa uchunguzi ukaanza na chuo wakawa wananiuliza sana mimi maana nilkuwa close sana ila ilibidi niseme sijaonana naye toka jana hivyo sijui ilikuwaje maana hata simu zangu , siku iliyopita hazikupokelewa na pia nilienda kwake pia ila bado sikumkuta.
Nilihojiwa pia na polisi ila bado sikubatilisha maelezo, mwisho msiba uliendelea na akasafirishwa na chuo mpaka kwao nilienda pia msibani ila ilibaki kuwa hatia moyoni mwangu .
Kila nikikumbuka uwa najutia sana
All in all rest in peace banzoka .