Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Hutakiwi kujuta maana kilichopita huwezi kukirekebisha lakini kijacho hukijui pia unatakiwa ukomae na wakati uliopo hapo ndo kwenye maisha halisi.
 
Siku ambayo huruma yangu ilitaka kunitokea puani, tuliwapa Askari polis lift aisee jamaa wakataka kutuuzia kesi ya madawa ya kulevya.

Toka siku hiyo niliapa na kuapiza mwanangu siku atakayochagua kuwa polisi ndo siku ambayo nitamkana kama Petro alivyomkana Bwana Yesu.

Bila hatia tulisota sana. Daaaa
Hivi Hawa polisi wanajikuta Nani?
 
Hutakiwi kujuta maana kilichopita huwezi kukirekebisha lakini kijacho hukijui pia unatakiwa ukomae na wakati uliopo hapo ndo kwenye maisha halisi.
Ni vyema tuwe realistic, hakuna anayeishi asiye na regrets.

Unaweza ukasema hauna regrets ila kuna vitu vilivyopita unatamani ungevifanya vizuri zaidi, au kuna watu ambao haupo nao tena ila unawish wakati walikua karibu yako maybe unge care a little more, au kuna vitu vichache ulikosea wakati unalea watoto wako na unawish muda ungerudi nyuma uvirekebishe, au kuna fursa kubwa ulizikosa/zilikupita kwa sababu hukuweka jitihada fulani ambazo zilikua ndani ya uwezo wako, au kuna vitu ulivikubali kwenye maisha yako ambavyo unawish usingevikubali, au kuna matukio ulishayafanya huko nyuma, and you are not proud of kwa sababu yameweka doa katika historia yako.

Kuna mengi yanayofanana na hayo ambayo kila anayeishi anayapitia. Regrets are there, kikubwa tujifunze kupitia hayo. Tunaposema "No Rear View Mirrors in Life" hatumaanishi kutokuangalia nyuma kabisa, bali kutokuangalia nyuma muda wote i.e. kutokuendesha usukani wa Maisha tukitegemea yaliyopita pekee.

All Love [emoji1479]
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Asee pole sana. Bila shaka ulikuwa mwanafunzi wa KIU
 
Lazima tuwe realistic, hakuna anayeishi asiye na regrets.

Unaweza ukasema hauna regrets ila kuna vitu vilivyopita unatamani ungevifanya vizuri zaidi, au kuna watu ambao haupo nao tena ila unawish wakati walikua karibu yako maybe unge care a little more, au kuna vitu vichache ulikosea wakati unalea watoto wako na unawish muda ungerudi nyuma uvirekebishe, au kuna fursa kubwa ulizikosa/zilikupita kwa sababu hukuweka jitihada fulani ambazo zilikua ndani ya uwezo wako, au kuna vitu ulivikubali kwenye maisha yako ambavyo unawish usingevikubali, au kuna matukio ulishayafanya huko nyuma, and you are not proud of kwa sababu yameweka doa katika historia yako.

Kuna mengi yanayofanana na hayo ambayo kila anayeishi anayapitia. Regrets are there, kikubwa tujifunze kupitia hayo. Tunaposema "No Rear View Mirrors in Life" hatumaanishi kutokuangalia nyuma kabisa, bali kutokuangalia nyuma muda wote i.e. kutokuendesha usukani wa Maisha tukitegemea yaliyopita pekee.

All Love [emoji1479]
Aya bhana ngoja na mm niseme langu.
Najutia kuzaa mapema na kushindwa kumlea mtoto wetu kwa pamoja.
 
inauma sana hapo keko toroli kuna ile time inaitwa toroli combine nakumbuka siku moja narudi usiku kama saa nne mtaa umetulia nilikuwa na jamaa yangu mmoja yey alikuwa na samsung s6 ni nina katecno w3 mwaka 2016 mara pakatokea kundi la watu mi nikajua watu wametoka kucheza mpira wanashanglia tu wanakuja mtaa uko kimy halafu bado saa nne tunakutana nao uso kwa uso ukuta mrefu kama uchochoro wa mbele wako safi ila wa kati na nyuma wana mapanga wengine fimbo wangine wako peku ,wako tumbo wazi wamevaa vipensi

jamaa yangu alichezea panga sema ubapa alikuwa kavaa modo simu imejichora kweny mfuko wakampokonya mi niliingia kweny vibanda vya furniture kule palikuwa na mlinzi nae kakimbia nimeacha viatu wamechukua vilikuwa vipya.ila walinipiga fimbo ya uso mateke niliponyoka mbio

kwa makadirio wako kama 50 na kitu ni wengi mno
kipindi Iko keko hukatizi kimama....Kuna wahuni wa kuitwa wasumbufu ao noma....!nashangaa hao Wana eti kiwanja Chao cha kutambia kilikuwa king palace dah....umeacha inferno au uku JJ amani ya kutosha
 
Noma sana kweupe unatemeshwa simu na makofi na mitama juu
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja hivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja.

Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako.

Kifo ni fumbo kubwa.

Tuwajali Sana wanaotupenda, life is too short.
Yamenikuta km yako mi ni mwaka mmoja nyuma tena mke wangu na nina watoto nae tumegombana kwa kisa kdgo tu nikamludisha kwao amekaa km mwaka kwao lkn tunaendelea na mausiano yetu km kawaida siku ya tarehe 1 mwenzi wa 10 saa kumi 11 nampigia cm anapokea mtoto analia ananiambia baba njoo kanisani mama kaanguka nampigia mkubwa wao ananiambi njoo anaendelea vzr yupo hospital nafika naambiwa amefariki njiani.HAWA POPOTE ULIPO JUA BADO NAKUPENDA JAPO NINA MKE MWINGINE NA MTOTO WA KIUME AMBAE MI NAWEWE HATUKUBAHATOKA KUMPATA ILA MAISHA YA WOTOTO NI MAZURI SN MKUBWA YUPO CHANG'OMBE ANAINGIA KIDATO CHA SITA MWINGINE YUPO KIDATO CHA KWANZA NA G YUPO DARASA LA PILA ILA YULE MWANAMKE ULIEMCHUKIA NDO AMEKUWA MKE WANGU NA ANALEA WATOTO VZR PAKA NDUGU ZAKO WANAMWONA KM NDUGU YAO
 
Noma sana kweupe unatemeshwa simu na makofi na mitama juu
hio mitaa Kuna wazawa vichochoroni flani wanakwambia usipite....wahuni wanaruka na wewe hata kama wanakujua....!!

Kuna mwanangu nilikuwa namtembelea pande hizo ni namba nae kashafariki kwa ukishandu alikuwa ananiambia Kuna mitaa na bar flani usilewe sana watu wapo kazini hata kama wanakujua
 
Back
Top Bottom