Enhe! Em tusimulie,ilikuaje na Regina?
Dah Regina bana, sijui alishaolewa? Sijui hajaolewa? Sijui alisharudi India ? Dah haya maswali yanaishi kichwani mwangu kila siku japo alikuwa tomboy ila nilimkubali kiasi chake .
Turudi nyuma kipindi cha advance pale skuli nilipoleta kisa cha kuhangaikia haki ya wanafunzi wenzangu kwa siri ,mission ikafanikiwa ila niliowahangaikia wakanitenga kwa kudhani mimi ni snitch kwa kujazwa maneno na walimu , huku na walimu wakinigwaya sana .
Basi ni katika mwaka wa kidato cha sita mwanzoni , ndipo napata kumjua Regina akiwa kahamia toka shule ya Saint Anne Marie, alihamia shuleni kwetu baada ya tetesi kuwa alifukuzwa na baadhi ya wenzake, sababu ya utovu wa nidhamu.
Baada ya kufika shuleni zile fununu zilizagaa sasa kutokana na watoto wengi wa o_level kuwa (maspy) wapelelezi wa walimu kutokana na hizo fununu basi wanafunzi wengi walikuwa wanamtenga Regina, back in the story of mine sijawahi kukubali kuona mtu anatengwa au kunyanyapaliwa nivumilie lazima nimcofort.
Kupitia faraja na kheri zangu kwa Regina tukawa marafiki japo kwa siri sana maana mimi si wanafunzi wala walimu wananipenda sababu ya negative perception hivyo pale shuleni ilifika mahali kama ningekufa basi Regina ni mmoja wa watu pale shule angelia labda.
Ukaribu wetu ulichangiwa na kuwa kidato kimoja , maisha yaliendelea kwa kupiga story siku moja moja pale nafasi ikiwepo ya upenyo ila zaidi akiwa na jambo linalomtatiza aliendelea kuniandikia memo hivyo nilijibu kwa memo japo hatukuwahi kuwa wapenzi that time ila ni rafiki wa karibu.
Regina alikuwa ni mtu wa Morocco _AIRTEL, hivyo baada ya kuhitimu kidato cha sita nilifanikiwa kufika kwao na yeye kufika kwetu , by that time aliweza kunitambulisha kwa dada yake mimi kama mpenzi wake , kitu kilichonifanya nikubaliane naye pasipo kubisha japo sikuwahi kuwa na hisia naye .
Sikuwa na hisia naye sababu alikuwa kama vile ana homoni za kiume yaani mjini tunasema , ni tomboy , basi since siku ile charting manner ilibadilika kutoka rafiki wa karibu mpaka mpenzi ,sometimes nilipokuwa naenda kumpitia kwao twende beach basi dada yake alipenda kunitania kuwa ataandika story yetu kwenye gazeti , hii ilikuwa sababu ya yeye kuwa anafanya kazi gazeti la mwananchi kipindi hiko.
Kwa haraka baada ya kufika kwao Regina kwa mtu mwenye akili timamu isingekupa shida kujua kuwa Regina kwao ni wa kishua so akawa anapenda sana kunipa vizawadi zawadi mwisho na mimi nikajikuta nampa zawadi pia , mwisho hisia kati yangu na yeye zikawa zimefana na mwisho nikamla mara kibao sehemu tofauti tofauti za kujistiri (nyumba za wageni) .
Back in my story nilipomjulisha Regina habari ya mimi kwenda bukoba kumuona bibi yangu, na yeye alisema si mda ataenda njombe kumuona mama yake sababu kipindi hiko alikuwa kule na project zake .so ikawa yeye anajiaanda kwenda njombe na mimi najiandaa kwenda bukoba .
One week kabla ya mimi kuondoka nilimsindikiza uwanja wa mwalimu nyerere kwa ajiri ya safari yake kwenda njombe then few day na mimi nikaenda bukoba , mawasiliano yaliendelea sana na ni ukweli masikini Regina alinipenda sana mpaka akawa ananipa mipango kibao ya mimi kufanya na yeye pindi tukienda chuo ila ndiyo hivyo mwenzake , ndiyo ujana umewasha moto nakubali ila akili haiko pale .
Back in my story , baada ya kufika bukoba na kuanzisha penzi na yule mpangaji wa bibi , basi biashara na Regina iliishia pale sikuwahi mpigia wala kumtafuta akawa anapiga napokea ila ni mpaka nijisikie basi masikini Regina wa watu akaona isiwe tabu , akajikataa mazima .
Mwanzo sikuwaza hata kidogo yeye kuniacha maana nilikuwa na mpangaji wa bibi na mda huo penzi limenoga ila baada ya kurudi dar , hisia zilinibana sana nikaanza kuzikumbuka moment zote nilikuwa na Regina ila sasa sina tena namba yake , nikajitosa kwenda kwao morroco _AIRTEL ila nikaambiwa walishahama mda si mrefu ila wako masaki.
Nitafanya jitihada kumpata huko masaki nikagonga mwamba , mwisho nikapata namba yake toka kwa rafiki yake wa mtaani pale morroco, maana classmates wote nikiwaulizia kila mtu namba yake hana .
Baada ya kupata namba nikamtafuta ila bado sikumpata , na maisha yangu yakaendelea kama kawaida, siku nishaingia chuo , Regina alinitafuta kwa namba yenye code za India , akidai ananisalimia tu , nikajibaruguza pale kumuomba msamaha na kutaka kujua anarudi lini bongo ?
Haikuwa rahisi kunipa majibu na akadai mimi ni rafiki yake tu , haitakaa itokee tena mimi kuwa naye , hivyo hata ratiba zake si lazima mimi kuzijua mpka apende yeye, niliumia ila nikajipa moyo maana "TRUE LOVE NEVER DIE" ila ilikuwa ndoto ya mchana kwa Regina maana sikuacha kujibaraguza kwake ila hakuwa hata kuonesha dalili kurudisha moyo nyuma .
Nikasema acha nikamtafuta dada yake pale ofisi za mwananchi , nimpange ni vipi nahangaika na penzi butu la mdogo wake , dah dada mtu mwenye akanichana makavu kuwa nilimzingua mwenyewe mdogo wake hivyo , kama nililianza mwenyewe nilinywe.
Baada ya ile safari kwa dada mtu, nikasema huu upuuzi sitarudi tena na wala sitamtafuta tena , nikaendelea na maisha yangu na vidada Poa vyangu .
Ila siku moja moja uwa namkumbuka hasa zile moment na yeye, mara beach, mara shuleni akijakuvistiwa basi mikuku naifaidi sana ,mara twende club japo wana walikuwa wanashangaa hasa mtaani kwao kuwa napenda nini pale ila dogo alikuwa na true love and true care kwangu .
Regina ulikuwa mtu wa social networks sana , yamkini huko hapa , iam sorry bwana , utoto ule sasa nimekuwa sikutafuti uwe mpenzi tena ila turudishe hata roho ya urafiki wetu ule maana ulikuwa unanifurahisha sana .
Kwako Remigal.