Kisa siasa, Wolper aacha kuigiza

Kisa siasa, Wolper aacha kuigiza

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Habari ikufikie kuwa mtoto mtamu anayesumbua katika tasnia ya filamu Bongo , Jacqueline Wolper Massawe ameweka pembeni masuala ya uigizaji kwa muda usiojulikana kwa kile alichodai ni kujipa muda wa kupumzika na kujikita zaidi kwenye mambo ya siasa .

Rafiki wa karibu na Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa Wolper kwa sasa amekolea sana kwenye mambo ya siasa na kuona kama amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye mambo ya uigizaji .

Baada ya kupata ubuyu huo , mwandishi wetu alimtafuta Wolper ambaye alikiri kuamua kupumzika kidogo mambo ya uigizaji huku akishindwa kuweka wazi atajikita kwenye nafasi gani ndani ya ulingo wa kisiasa .

Aah , kila mtu ana mipango na malengo yake , ni kweli kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya kupitia siasa, nimejifunza vitu vingi mno vya msingi na muhimu , nimeweka kando kwa muda uigizaji , muda ukifika wa kuendelea na fani hiyo , nitasema , alisema Wolper .
 
Kumbe siasa inalipa kuliko sanaa aiseee...!
 

Attachments

  • 1447507315820.jpg
    1447507315820.jpg
    8.6 KB · Views: 1,571
  • 1447507327789.jpg
    1447507327789.jpg
    64.4 KB · Views: 1,490
Wamempiga chini kwenye viti maalum lazima atakuwa ameumia or she is just tired. Siasa siyo mchezo ati!
 
ila sometimes ukiona hupati bwana wa maana yakubidi ujipitishe maeneo wanapopatikana eeeh unayifanya uko kwenye siasa kumbe unawinda ukinasa mdege unajifanya umestaafu kwani nini bahna, we ushajua % kubwa ya wanaoenda serena ni wakubwa japo wachovu nao huja mara moja tu kama sehemu ya tour nawewe pendeza nenda hukohuko, eeebo

mpaka ukutane na limbuzi lenye maziwa kwa mama ntilie, disco vumbi utanyoa hadi hadi kipara
 
kina wolper,wema,steve nyerere ndio wanasiasa watakaiokomboa nchi yetu,wako real sana
 
Back
Top Bottom