Kisa wivu wa mapenzi, mume adaiwa kumuua mke kisha kumtenganisha kichwa, kiwiliwili na viungo vingine

Kisa wivu wa mapenzi, mume adaiwa kumuua mke kisha kumtenganisha kichwa, kiwiliwili na viungo vingine

Kutoka gunia mbili za mkaa ikaja risas 7
Haikukaa sana upanga ukeni ukizungushwa 360° mara paaap shingo na mwili vinaachana

Yajayo yanafikirisha wanawake mbadilike lasivyo mtaisha kimasihara
 
Hebu toka hapa. 😂

Tena watu wenye kauli hizi ndo wakuangalia atii.
Sio mimi 😅😅😅

Mie toka nimejiunga jf sijawai pata hiyo bahati na huenda siku ikitokea nitaanzisha thread kabisa.. Au nafail sijui wapi au kwakua sina gari ma nyumba kali
 
Ila ukiona kuna kibaya kizuri kipo, kuna watu wana enjoy hadi kufa kwao na kuna watu yanawatesa hadi kufa kwao
Hakika rafiki japo kwenye hizi mambo za kuuwana siku hizi hazichagui tena wale wenye raha ndo wako hatarini yaani ikitokea mmoja kalikoroga tu basi ujue kama sio gunia za mkaa basi mguu wa kuku utahusika kuondoa uhai wa mwingine.
 
Sio mimi 😅😅😅

Mie toka nimejiunga jf sijawai pata hiyo bahati na huenda siku ikitokea nitaanzisha thread kabisa.. Au nafail sijui wapi au kwakua sina gari ma nyumba kali
Hahahaaa. Lol.
 
Hawa jamaaa wanaroho ngumu sana,Nadhani wakati wa Jemedari Ndio walipewa Tender zakuwatia watu kwenye Sandarusi na kutupwa Baharini...RIP Mawazo
 
Hakika rafiki japo kwenye hizi mambo za kuuana siku hizi hazichagui tena wale wenye raha ndo wako hatarini yaani ikitokea mmoja kalikoroga tu basi ujue kama sio gunia za mkaa basi mguu wa kuku utahusika kuondoa uhai wa mwingine.
Rafiki, kuna chuki na wivu hivi viwili mnapo anza mahusiano lazima mvijue na namna ya ku control. Palipo na upendo wa kweli amani hutawala
 
Rafiki, kuna chuki na wivu hivi viwili mnapo anza mahusiano lazima mvijue na namna ya ku control. Palipo na upendo wa kweli amani hutawala
Sometimes havizuiliki rafiki nadhani kinachotupasa ni kujitahidi ikibidi kuomba kila uchwao ikitokea kuwa na namna bora ya kukabiliana navyo bila kudhuru wengine.

Ikibidi tujifunze kuwaacha waende.
 
Sometimes havizuiliki rafiki nadhani kinachotupasa ni kujitahidi kuwa na namna bora ya kukabiliana navyo bila kudhuru wengine.

Ikibidi tujifunze kuwaacha waende.
Ila pia kupima akili mala kwa mala maana siku hizi magonjwa ya akili yameongezeka unahisi wivu kumbe mtu akili imepuyanga tayari
 
Ila pia kupima akili mala kwa mala maana siku hizi magonjwa ya akili yameomgezeka unahisi wivu kumbe mtu akili imepuyanga tayari
Aisee!!

Hivyo mie nikapimage akili ee maana huwa nina wivu hadi saa ingine najichukia lol. 😂😂

CC. BAK 🙊
 
Kitu cha kujifunza ni kwamba nimegundua pia wanawake licha ya kwamba ni mama zetu lkn ni wapumbavu sana wamekosa weledi...acha wauliwe tu.
R.I.P
Tatizo naloliona hapa ni ile utii kwa dada zetu haupo kabisa hata kama amekosea bado anakuwa mkaidi anakutukana. Unadhani kunamwanaume wakumjeruhi mwanamke mnyenyekevu akikosea hayupo tatizo majibizano.
 
Aisee!!

Hivyo mie nikapimage akili mana nina wivu hadi saa ingine najichukia lol. 😂😂

CC. @BAK🙊
Wivu ni adhabu , ukiwa umepitiliza hapo inabidi ukacheki afya ya akili rafiki usije mpiga mtu tukio 😅😅😅😅
 
Mwanaume mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Lubela, Mtaa wa Nyashimbi, Kata ya Mhongolo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Bundala Mathew anashikiliwa na Polisi, kwa tuhuma ya kumuua mkewe, Rehema Nyamgila kwa kumcharanga mapanga.

Imedaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, alitenganisha viungo vya mwili wa mkewe na kuchukua baiskeli na kuvisafirisha mpaka mbugani usiku wa manane na kuvitawanya ili kupoteza ushahidi.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Magdalena Katambi ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo, alidai kuwa tukio hilo liligunduliwa na mtoto wa marehemu, Ezekiel Bundala tarehe 27 Mei 2022.

"Nilienda kumjulia hali mtoto aliyekuwa anaumwa, ndipo Ezekia akanijulisha kuwa mama yake hayupo funiani.

“Ameniambia aligombana na baba yake kwa kuwa aliona beseni likiwa na damu lakini baba yake akawa anasema hizo ni rangi tu na siyo damu.”

Anasema wakatoa taarifa kwa ndugu, majirani na Polisi, ndipo mtuhumiwa baada ya kubanwa akawapeleka alipoutupa mwili, wakaukuta ukiwa umekatwa vipande.

Alidai ljumaa mwili ulipelekwa kuhifadhiwa mochwari ya Hospitali ya Manispaa ya Kahamana, 28 Mei 2022, Polisi walirudi na mtuhumiwa kuonesha mahali alipohifadhi viungo vingine vya mwili huo, ndipo kichwa kikapatikana kimezikwa juu ya kaburi la marehemu babu yake kwa mama.

Magdalena alidai viungo vingine vya sehemu za siri na matiti vilipatikana karibu na mlango, kwenye mafiga ya jiko, ndipo alipozika, huku akitaka watoto wake wapikie hapo mara kwa mara, kwani ameweka mbayuwayu wake akauke kwa ajili ya kutengenezea dawa.

"Baada ya askari kumhoji tena wapi vilipo viungo vingine, aliwapeleka mbugani ulikookotwa mwili katikati ya majaruba ya mpunga ilipatikana mikono na magoti, lakini wakati huo vidole vya mikono na miguu havikuonekana, kwa kweli tukio hili limetusikitisha na kutuachia simanzi kubwa," alisema Magdalena.

Hata hivyo, mama mzazi wa mtuhumiwa, Mhoja Bundala alidai kupata taarifa kwa watu kuwa mwanawe ameachana na mkamwana wake, hivyo akawa anasubiri taarifa rasmi kutoka kwake, lakini ajabu aliletewa taarifa za tukio hilo la kushitua.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyashimbi, Peter Nzingula alisema tukio hlilitokea usiku wa Mei 27, 2022.

Anasema alipohojiwa chanzo cha kufanya unyama huo, mtuhumiwa alidai alikuwa na wivu wa mapenzi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Boniphace Maziku alidai kuwa tukio hilo lilitokea kwenye kata yake Mtaa wa Nyashimbi, na alishirikiana na viongozi wa ngazi ya mtaa, kutoa taarifa sehemu husika, na sasa uchunguzi wa tukio unaendelea Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wake unaendelea, na sheria itachukua mkondo wake.

Marehemu Rehema ameacha watoto wanne.


Source: MwanaHalisi
Dunia inayumba watu wamekengeuka, bora ukutane na simba mla nyama kuliko binadamu.
 
Kuna watu wa hovyo sana. Kuua tu hajatosheka mpaka kukata kata vipande. Kanda ya ziwa ina historia ya matukio mengi ya kikatili, sijui sababu nini.
Sababu ushirikina mkuu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Hujakutana nayo na omba yasitokee kwako

Hata yakitokea na umri huu tayari machweo yashaingia, watoto washakuwa na wanajielewa, Sidhani kama itakuwa sahihi kuanza vita na mwenzangu ambaye wote tupo kipindi cha pili .
Hapa ni kumcha Mungu na kuitafuta pepo ndicho kilichobaki.
 
Back
Top Bottom