kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Ilikuwa mbwembwe za hali ya juu kwa rubani mkuu wa shirika la ndege ufipa alipoamua kujiokotea abiria na wengine hakuwajua tabia zao, Aliondoa ndege hiyo uwanja wa ufipa.
Ndege hiyo ya mabua wapo walioshauri rubani watu uliochukua wengine wana silaha wanaweza kukukaba na ni lazima wachunguzwe mienendo na tabia zao huko walikotoka. Rubani alikuwa mzito wa kupokea ushauri, mshauri mkuu akaamua kuachia ngazi,
Rubani akatangaza anabadili gia angani mlio mbaya wa mashine uliotoka kwenye hiyo ndege na moshi ni hatari, tukaanza kushangaa kuona abiria mmoja baada ya mwingine wakishuka kwa maparuchuti kuelekea kule walikotoka.
Ubishi wa rubani umepelekea shirika la ufipa kupata hasara na kufilisika kabisa, wiki moja iliyopita abiria mmoja mzee alionekana mchoovu nae amerudi na kupelekwa hospitali kupata matibabu. Juzi ya ijumaa aliyekuwa mhudumu wa ndege nae amerudi rasmi nyumbani kujivua nyazifa zake zote na kulaumu rubani
Watendaji wakuu wa shirika la ndege la ufipa baada ya kupata taarifa kuwa kisanduku cheusi kimepatikana wamejifungia kwenye ukumbi mmoja kuja na tamko la kutaka wasimamizi wakuu wa anga waje kama wasimamizi huru bila kupendelea mashirika mengine, hivi sasa rubani mkuu na kiongozi mkuu baada ya kubadili uongozi anajitayarisha kwa safari mpya na rubani kutoka ulaya alikokwenda kutibiwa baada ya ajali .
Swali ni jee shirika litamudu baada ya kuwachwa hoi na mtikisiko?
Yetu macho ni ngumu kopo kuligeuza kuwa pipa!