Kisarawe, iliyoko mkoa wa Pwani Tanzania, inakabiliwa na changamoto za barabara mbovu toka miaka ya 60

Kisarawe, iliyoko mkoa wa Pwani Tanzania, inakabiliwa na changamoto za barabara mbovu toka miaka ya 60

Linus w slaa

Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
67
Reaction score
152
Wananchi wanalia kila siku, mfano maguruwe barabara mbovu kama mazingira ya mwezi, lakini DC na TARURA wamejikita kwenye viti vyao vya starehe, wakisikiliza kilio cha wana nchi kama wimbo wa kawaida!

Hii ni dhuluma ya wazi – pesa za walipa kodi zinapotea kwenye miradi ya karatasi, wakati barabara zinawasababishia watu kushindwa kufika mahospitalini, ajali, magari kuvunjika, na biashara kufa. Viongozi hawa wamegeuza jukumu lao la kuwahudumia watu kuwa jukwaa la kulala usingizi, wakidhani wana nchi hawana sauti.

Lakini sisi hatulali – tunasema basi! Miundombinu mibovu ni adui wa maendeleo, na wanaosimamia kama TARURA na DC ni washirika wa mateso haya. Wananchi wamechoka na ahadi za upepo; wanataka barabara, wanataka heshima, wanataka maisha bora sasa!"
 
Back
Top Bottom