chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Ni kama vile DC Magoti anaona kama wananchi wanadhani yeye sio DC, lakini kawadhihirishia kwamba yeye sio DC wa Mpeche Mpeche, ni DC wa kimataifa, na kwamba wasidhani kwa umbile yeye ni mtoto, bali ni mtu mzima, na Rais kamteua.
N.B: nadhani anaweza kufanya tukio kubwa, pengine baya, ili wananchi waamini yeye ni DC, lakini naona wananchi tayari wanajua yeye ni DC.
Namuona kama anatamani afanye kitu kibaya ili watu waamini kama yeye ni DC, lakini akifikiri aina ya uongozi wa CCM na serikali uliopo, ni kama anajizuia akijua watamla kichwa, sasa angekuwa DC awamu ya tano, nadhani OCD angekuwa na kazi ya kusomba watu na kuwaweka rumande kila siku.
Magoti anatoa kauli hizi wakati muda mfupi tu uliopita, Nape Nnauye "kateleza" kwenye kauli, akaliwa kichwa.
Pia jamii ya watu wa Pwani ni moderate sana kitabia, wasiopenda kauli kali na rabsha, ni watu wa staha na subra, hivyo anapoteza uwiano wa tabia ya jamii na uongozi wake. Hata Samia hajawahi kutangaza kuwakata visogo watanzania, hata kama wamekosea, ila anahimiza utawala wa sheria na "4R"
Labda wangemtumpa Serengeti au Tarime huko akakutane na nginjanginja zenye uso mkavu kama zimemeza nusu kilo ya pilipili kichaa, ukiweka wanaweka.
Wengi wa watu wa Pwani hawana asili ya kuwa na visogo virefu kama ndugu zetu waha au wachaga, sasa akivikata hata hivyo vilivyopo, sijui wataonekanaje